Njombe: Wastaafu tumeendelea kuumia kwa kukaa nyumba za serikali bila kazi kwa kuwa hatupati kwa wakati nauli na mafao yetu

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
Na.amiri kilagalila
Kutokana na Serikali Kucheleweshea Nauli na Mafao kwa sisi Walimu Wastaafu Pindi tunapofikia Ukomo wa Umri Kazini Kumeongeza Mzigo Mzito kwetu kwa kuwa tumeendelea Kuishi Kwenye Nyumba za Serikali Ilihali Hatuingizi Chochote.

Kauli Hiyo Imetolewa na Walimu Wastaafu Toka Kata ya Ulembwe Wilayani Waging'ombe Akiwemo Mwalimu Mstaafu Yotham Mwalongo na Mwalimu Mstaafu Kassim Mlanga Baada ya Uongozi wa Kata Hiyo Kuwawekea Hafla fupi ya Kuwaaga Ambao Wamesema Kuwa Kucheleweshwa Kwa Nauli Zao Kumeendelea Kuwadhoofisha Kiuchumi Siku Hadi Siku.

"imekuwa ni kilio kwetu kwa kuwa changamoto kubwa tunayoipata katika kustaafu kwetu ni kucheleweshewa nauli ya kurudi makwetu kwa mfano mimi nimestaafu tangu mwezi wa saba mbaka leo sijapata chochote naishi kwenye nyumba ya serikali na kazi sifanyi ni bora hata hayo mafao yangetoka kwa wakati ili tuweze kumudu maisha yetu na swala la kupewa nauli imekuwa msamiati kwetu tungeiomba serikali itekeleze haya ili tuweze kupisha katika nyumba hizi waishi wengine"alisema mmoja wa wastaafu

Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu CWT Wilaya ya Wanging'ombe,Mwalimu Andrew Lovela Ametumia Fursa Hiyo Kuwataka Wastaafu Hao Kwenda Kuzitumia Kwa Malengo Fedha za Mafao Ya Ustaafu Pindi Watakapozipata Badala ya Kuzitumia Ovyo Huku Akiwataka Kumrudia Mungu Katika Umri Walionao.
"niwaombe ninyi wazee mkawe wachungaji mkawe wainjilishaji na fedha mtakapozipata basi mkazitumie vizuri katika uzee wenu"

Akizungumza Kwa Niaba ya Askofu wa Jimbo Katholiki la Njombe Padre Exavely Mlelwa Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Amewataka Watoto wa Wastaafu Hao Kuona Namna ya Kuwawekea Mazingira Rafiki Katika Kuendelea Kuwatunza Wazazi Wao Badala ya Kuwatelekeza.

"lakini ndugu zangu niwaombe watoto tunampango gani na hawa wazazi maana baadaye watakuwa hawana fedha za kununulia nguo wala mavazi hata weza kujipikia chakula hivyo ndugu zangu tujue sasa wajibu wetu kwa hawa wazee"alisema Padre Mlelwa

MWISHO
 

Attachments

  • REPORT WANGING'OMBE SAFIII.MP3
    4.7 MB · Views: 7
Hizo ndizo athari za umasikini wa kufikiri. Mlikuwa hamjui kama kazi muifanyayo ni muda na muda ukifika mtapumzika?

Je, endapo mafao hamtapewa ndio kusema mtatopea kwenye lindi la ufukara?

Vipi kuhusu mshahara mliokuwa mnapokea ndio najua ni mdogo lakini hakuna mshahara mkubwa duniani kote, mlishindwa kujibana na kujenga hata vibanda tu?

Kulilia mafao ni haki yenu ila kutegemea mafao yakukwamue kimaisha hiyo hesabu iliyoshindikana.
 
Hizo ndizo athari za umasikini wa kufikiri. Mlikuwa hamjui kama kazi muifanyayo ni muda na muda ukifika mtapumzika?

Je, endapo mafao hamtapewa ndio kusema mtatopea kwenye lindi la ufukara?

Vipi kuhusu mshahara mliokuwa mnapokea ndio najua ni mdogo lakini hakuna mshahara mkubwa duniani kote, mlishindwa kujibana na kujenga hata vibanda tu?

Kulilia mafao ni haki yenu ila kutegemea mafao yakukwamue kimaisha hiyo hesabu iliyoshindikana.
hakika
 
Back
Top Bottom