Njombe: Wananchi wataka wanaotupa watoto kuchukuliwa hatua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,865
Wakazi wa Kijiji cha Matiganjola wilayani Njombe wameiomba Serikali ya wilaya kufanya oparesheni ya kuwasaka wazazi wanaotelekeza watoto wao na kuwachukulia hatua kutokana na kukidhiri kwa vitendo hivyo.

Wamesema hayo leo Agosti 8, 2021 katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa Lupembe, Edwin Swale uliofanyika katika vijiji vya Nyombo na Matiganjola wilayani Njombe.

Wamesema matukio ya kutupa na kutelekeza watoto yamekithiri katika kijiji hicho, hivyo Serikali ya wilaya inapaswa kuchukua hatua kwa wahusika, ili kutoa funzo kwa wote wenye tabia hiyo.

Wamedai baadhi ya wazazi wamekuwa wakifanya vitendo kwa madai ya hali ya kiuchumi na migogoro ya kifamilia baina ya wanandoa.

"Matukio kama haya yamekuwa yakijirudia, tunaiomba Serikali kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo" amesema Machael Salingwa.

Awali Mtendaji wa kata ya Ikuna, Alestadia Naza na Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya CCM Wilaya ya Njombe, Kasanga Makweta wamesema kitendo hicho kina athari kubwa kwa vizazi vijavyo na kwamba chama hakitafumbia macho.

Mbunge wa Lupembe, Edwin Swalle amesema kutupa mtoto kunakiuka haki za msingi za mtoto ikiwemo ya kuishi na kuagiza vitendo hivyo vidhibitiwe mara moja.

CHANZO: Mwananchi
 
Back
Top Bottom