Njombe walia ahadi za Kikwete kuchelewesha Mkoa wao

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Jakaya%2BKikwete%2Bna.jpg

Raisa Jakaya Kikwete

RAIS KIKWETE AKUMBUSHWA AHADI YAKE YA
MKOA WA NJOMBE KUANZA KABLA YA JANUARI 2012



WANANCHI na viongozi wa mkoa mpya wa Njombe wamehoji sababu ya Rais Jakaya kikwete kushindwa kutekeleza ahadi yake ya kuanza kwa mkoa mpya waNjombe kabla ya januari 2012 . Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe alisema kuwa alitegemea ahadi yaRais Kikwete aliyoitoa wakati wa ziara yake mkoani Iringa mwishoni mwa mwaka jana kuwa maandalizi ya mkoa mpya wa Njombe yamekamilika na kuwa kabla ya Januari 2012 mkoa huo utakuwa umeanza ingetekelezwa kwa wakati ili kuwapa matumaini wananchi wa mkoa huo.

Filikunjombe alisema kuwa matumaini ya wana Ludewa kuanzishwa kwa mkoa huowa Njombe kwa kuwa na mkuu wa mkoa kutasaidia kumaliza kilio chao cha ubovuwa miundo mbinu kwa serikali kuanza ujenzi wa lami katika barabara ya Njombe- Ludewa pia huduma zaidi kwa wananchi wa Ludewa kusogezwa. Kwani alisema kuwa upo uwezekano mkubwa wa wilaya ya Ludewa kupiga hatuazaidi katika maendeleo iwapo ahadi hiyo ya Rais ya kuanza kwa mkoa huo wa Njombe ikatekelezwa haraka zaidi . kuendelea kuchelewa kizindua mradi wa maji wa tovemtwango katika kata yamtwango, wilayani Njombe mnamo Novemba 11 mwakajana aliwaahidi wananchi kwamba utaratibu ukikamilika ikiwemo talatibu za kuteua mkuu wa mkoa na viongozi wengine, Njombe ingekua mkoa Rasmi pamoja na wilaya mpya ya wanging”ombe januari mosi,2012.

Huku mkazi wa Njombe John Haule akidai kuwa ahadi ya Rais aliyoitoa mwaka jana aliwahakikishia wananchi wa mkoa huo mpya kuwa uteuzi wa mkuu wa mkoawa Njombe na katibu tawala pamoja na mkuu wa wilaya ya Wanging’ombeungefanyika mapema kabla ya Januari ila hadi sasa kimya na kuwa inashangazasana kuona ahadi kama hiyo inashindwa kutekelezwa .

Taratibi zinafanyika za kumhamisha DC (mkuu wa wilaya ya njombe) kutoka bomani Ofisi zake za sasa) na atahamishwa katika sehemu ya ofisi za Halmashauli ya uilaya anasema mkuu wa kitengo mojawapo katika halmashauli ya wilaya (jina limehifadhiwa)
Wakati rais Kikwete akizindua mradi wa tovemtwango mwishoni mwa mwaka jana alisema kuwa zoezi hilo lingekuwa limekamilika kwa kuipata timu nzima ya mikoa na wilaya mapema kabla ya Januari 2012

Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake, Ibara ile ya 2(2) inampa nguvu rais ya kuigawa jamhuli ya muungano katika mkoa wilaya namaeneo mengineyo kwa kufuaata utaratibu uliowekwa nasheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. Kutokana na fulsa ambayo kiongozi huyo mkuu aliyonayo mwaka jana alitoa notsi ya kusudio la kuanzisha mikoa mine na wilaya 19.

Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha sheria ya uanishaji wa mikoa na wilaya sura 397 ya Toleo la 2002 ilichapishwa kupitia tangazo la selikari Na. 285 septemba 9, 2011 kwa ajili ya unzishaji wa wilaya. Katiba inaeleza lengo la kutoa mamlaka hiyo nikusaidia utekelezaji bora wa shughuli za serikali ikiwa pamoja na kubolesha utendaji wa serikali kuu kwa kupunguza ukubwa wa maeneo ya mikoa mama ili wananchi wapate huduma katika ngazi za kiutawala kwa karibu.
 
Tatizo la waafrika ni moja kubwa ambalo husababisha maendeleo kurudi nyuma si shauri ya ujuzi na uwezo tu, ila kutaka kufanya mambo mengi kwa mkupuo hali ambayo hufikia kutofanyika yote kwa mkupuo na kubaki tulipo aku kurudi nyuma zaidi.

Mfumo mzuri wa kujenga maendeleo ni huu:
Do one thing on a single time, when you done go ahead for the next one. Vinginevyo tutaendelea kutoa ahadi za kuwaridhisha wananchi na ukishaondoka nyayo zako zikifutika na kila ulichokisema kitaondoka na nyayo zako.
 
Eh! Kumba jamaa ni Msahaulifu? Basi Kazi Mnayo Watanganyika... Mmechagua Raisi Msahaulifu

Vipi hakuwahaidi Kuwaletea Kivuko cha Nchi Kavu?
 
Walidanganywa kwa T shirts na Khanga wakamchagua na sasa wanalia. Uvumilivu unahitajika katika hili, wawe wapole tu!
 
Mi simshangai Kikwete na ahadi zake anazotoa kwa Wananchi, kwani si mara ya kwanza kutoa ahadi kama hizo zisizotekelezeka kwa wakati, Siku zote Wajinga ndio waliwao, Watanzania tumekuwa watu Wakuchezewa na kuonekana wajinga, kwa Njombe, Wabena mkidanganywa na Mbolea basi mpo tayari kwa lolote hata kama ni baya, sasa niwakati wa kuamka na kujua haki zenu kama Watanzania, mambo ya utulivu na amani tumeyachoka tunataka mabadiliko yenye kuleta Maendeleo.
 
Back
Top Bottom