Njombe: Wahitimu wa vyuo walazimika kuolewa ili kuepuka ugumu wa maisha

Kuna mmoja alikuwa ananipanga ahamie kwangu
Kila siku akawa anajisemesha "maisha magumu sana wengine tuolewage tu "..
Nikamzoom nikaona hamna kitu hapa, imagine mtu anakuja kwako kupunguza makali ya maisha.
Siku makali yakiisha anaanza nyodo sio za nchi hii πŸ˜…!!! Wanawake wenye njaa ogopa sana yani huwaga wepesi sana kujisahau endapo hali ikiwa shwari tena usijiroge ukampa pa kushika hela au ukamtaftia mchongo atakovyabadilika ghafla hutaamini πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Siku makali yakiisha anaanza nyodo sio za nchi hii !!! Wanawake wenye njaa ogopa sana yani huwaga wepesi sana kujisahau endapo hali ikiwa shwari tena usijiroge ukampa pa kushika hela au ukamtaftia mchongo atakovyabadilika ghafla hutaamini
Ha ha ndo hivyo.. wanakuwa wapole sababu ya njaa!
 
WANAWAKE waliohitimu vyuo vikuu nchini wamesema wanalazimika kuingia kwenye ndoa ili kujikwamua na ugumu wa maisha wanapofika mtaani baada ya kukosekana kwa ajira licha ya kuwa na elimu ya juu.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wadau mjini Njombe wakati wakitoa maoni yao juu ya mwenendo wa elimu ya Tanzania huku wakitoa wito kwa wanafunzi waliochaguliwa kwenda kujiunga na vyuo vikuu kuchagua fani zitakazoweza kuwapa nafasi za kujiajiri mtaani pindi wanapokosa ajira.

Tofana Pascali ni mmoja wa wanawake wasomi aaliyesoma maendeleo ya jamii anasema wanawake wasomi baada ya kumaliza vyuo vikuu wanalazimika kuishi na wanaume watafutaje watakaowawezesha kupata chochote katika maisha yao.

β€œMwanaume atahangaika ataleta chochote kile nyumbani tule tulale ili maisha yaende kwasabau hata wazazi mtaani wamechoka kuombwa ndio maana tumeona ni bora tujiegeshe kwa wanaume hata kama hawajaonekana na mwisho wa siku wanatokea hata watoto wa mtaani”alisema Tofana

Emmanuel Ngelime na Johnson Mgimba ni miongoni mwa wadau wa elimu wanatoa wito kwa wanafunzi kuwa na machaguo sahihi wanapokwenda vyuoni ili wafanikiwe kuwa na shughuli za kufanya mtaani.

β€œWasomi wengi sana wako mtaani kwa kukosa ajira,ninaomba wanafunzi wawe makini na hizi taaluma wanazozichagua lakini pia serikali iongeze nguvu kwenye vyuo vya maendeleo na VETA ili tuweze kupata wataalamu zaidi”alisema Ngelime

Naye Mgimba amesema β€œTunaiomba serikali kwasababu ya changamoto hii ya ajira basi yale masomo ambayo tunajua motto akimaliza anweza kujiajiri basi wajaribu kuyapa kipaumbele kwenye swala la mkopo ili watoto wahamasike waweze kwenda kwenye yale masomo ili akimaliza na akakosa ajira basi aweze kujiajiri”alisema Mgimba.

Alatanga nyagawa ni mhadhiri wa chuo cha Amani mjini Njombe ameiomba serikali kubadili mtaala wa elimu ili wanafunzi waweze kusoma masomo yatakayoendana na mazingira ya Tanzania na kujiajiri.

β€œTunakwenda na masomo ambayo yanahitaji ukimaliza utembee na bahasha uombe ajira kwenye ofisi ya mtu,nadhani tuna changamoto kubwa kwenye silabasi zetu. Jambo hili tunahitaji kuliangalia upya ili tuhame na kwenda kwenye uhalisia wa maisha yetu”alisema Alatanga Nyagawa.
Afrika tumekuwa na maneno mengi kuliko vitendo, porojo kuanzia kwa wasomi aka wataalamu mpaka wanasiasa.suala la mtaala hakuna umakini kwani kuna baadhi ya taasisi zinafanya maboresho lakini bado hakuna mabadiliko
 
Kwa hali ilivyo sasa bora hao wamewahi nafasi mapema! Nyio mnaochelewa hali ya Solidarity Funds inavyoelekea mbele huko mtakuja kuwalegezea viuno walamba lips πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… japo wawahifadhi tu
πŸ˜€
Hao walamba lips ndio wakoje?
 
nchi inahitaji mabadiliko ya fikra.

umaskini wa nchi hii unatoka kizazi kimoja mpaka kingine kwa sababu tuliaminishwa huko nyuma kwamba ukisoma lazima uajiriwe,kilimo watu hawataki kwa sababu wakulima wanaonekana ni watu maskini na bei ya mbolea inapanda kila siku DAP iliyokuwa inauzwa 52,000/ imepanda mpaka 92,000/=

tubadilike kunusuru vizazi vijavyo.
 
nchi inahitaji mabadiliko ya fikra.

umaskini wa nchi hii unatoka kizazi kimoja mpaka kingine kwa sababu tuliaminishwa huko nyuma kwamba ukisoma lazima uajiriwe,kilimo watu hawataki kwa sababu wakulima wanaonekana ni watu maskini na bei ya mbolea inapanda kila siku DAP iliyokuwa inauzwa 52,000/ imepanda mpaka 92,000/=

tubadilike kunusuru vizazi vijavyo.
Kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom