Njombe: Rais Samia Awahutubia Wananchi Katika Mkutano wa Hadhara, Asema Serikali Imezuia Kupandisha Hadhi na Kukata Maeneo ya Utawala

10 August 2022
Njombe, Tanzania

Rais Samia Hassan asema kukatiana maeneo ya kiutawala huongeza gharama za uendeshaji serikali


Hivyo badala ya kuunda manispaa ya mji wa Njombe, mheshimiwa rais ataka fedha hizo ziende ktk afya, elimu na kilimo maana bajeti ni finyu na masuala ya msingi ni huduma kwa wananchi badala ya kuunda manispaa
Source : mwananchi digital
 
Hii nchi ukikaa ukatafakari shida sio vingozi, shida ni raia ambao ni sawa na wafu. Raia badala ya kuomba elimu bora kwa watoto wao au mifumo bora ya afya, wao wako busy wanataka mikoa na wilaya mpya na wapo ambao huomba hadi kata mpya.

Hawa watu kweli ndio waje kuingia barabarani kudai haki zao? Hakuna kitu kama hicho.​
 
Hii nchi ukikaa ukatafakari shida sio vingozi, shida ni raia ambao ni sawa na wafu,Raia badala ya kuomba eliklmu bora kwa watoto ao, au mifumo bora ya afya wao wako busy wanataka miko mipya na wilaya mpya, wapo ambao huomba hadi kata mpya.

Hawa ndo kweli waje kuingia barabara i kudai haki zao? Hakuna kitu kama hicho.
Wanaoshinikiza hayo maombi ni wale wanaojitengenezea fursa. Unapokuwa na wilaya au halmashauri mpya, manaake unakuwa na utawala unaojitegemea kama mkuu wa wilaya, DAS, DED, na watumishi wengine kadri ya uhitaji.

Wenzangu na mie wanaunga tu hoja wakati pengine hata sifa za huo uteuzi hawana. Halmashauri nyingi ni mzigo kwa taifa. Bora hata tungekuwa na majimbo kadhaa makubwa yanayoungaunisha mikoa mingi.

Sema kuna wazee wa fursa hapo watakasirika vyeo vyao kuporwa! Halmashauri nyingine hazina hata vyanzo vya mapato vya uhakika, ndio maana TAMISEMI inageuka kuwa wizara mzigo kwa serikali.
 
Hii nchi ukikaa ukatafakari shida sio vingozi, shida ni raia ambao ni sawa na wafu,Raia badala ya kuomba eliklmu bora kwa watoto ao, au mifumo bora ya afya wao wako busy wanataka miko mipya na wilaya mpya, wapo ambao huomba hadi kata mpya.

Hawa ndo kweli waje kuingia barabara i kudai haki zao? Hakuna kitu kama hicho.
Wanaoomba hizo halmashauri wanasaka tonge, maana halmashauri zilizopo tuu zingine zimeshindwa hata kukusanya mapato na kufikia malengo ya serikali kuu. Lakini wengine wanaziomba ili kuendelea kupata subvention kutuko serikali kuu na ili watusumbue huku mtaani sisi watumishi wa rank za chini
 
Back
Top Bottom