figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Heshima kwenu wakuu,
Usiku wa kuamkia leo, Polisi Mjini Makambako wameua Jambazi baada ya kurushiana risasi.
Polisi wa Doria walipata taarifa kwamba majambazi wanataka kuiba katika kituo cha Mafuta Makambako ndipo walipoenda.
Walipofika wale majambazi wakaanza kurusha risasi ovyo ovyo, ndipo polisi Mmoja mwenye shabaha alipomlenga jambazi mmoja risasi na kufa hapopo.
Nawapongeza Jeshi la polisi kwa jinsi wanavyokula shani moja na Wahalifu, Wanalala nao mbele haswaa
Nawashauri wale wenye Tabia za Ujambazi waache kwani siku zao zinahesabika. Zama zimebadilika pia.
Ni wakati wa Makonda kuwapa hawa Askari wa Makambako Milioni yao.
==================
Jambazi auawa na Polisi Njombe
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu.
Mtu anaye daiwa kuwa ni jambazi ameuwawa katika majibizano ya risasi na jeshi la Polisi katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambako majambazi hao walitaka kufanya tukio la uvamizi katika kituo cha mafuta.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu, amesema jeshi la polisi lilibaini kuwapo kwa watu wanaohisiwa kuwa ni majambazi majira ya saa 3:30 usiku ambao walikusudia kuvamia kituo hicho ambapo polisi walifika eneo la tukio na kuanza kufyatuliana risasi.
Polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema walifika eneo la tukio lakini watuhumiwa hao baada ya kuona gari ya polisi walianza kurusha risasi hovyo ndipo askari walipoanza kujibu mashambulizi na kumpiga risasi mmoja kati ya watuhumiwa hao aliye kuwa na silaha
Katika majibizano ya silaha baina ya polisi na watuhumiwa hao polisi walimpiga mmoja kati ya watuhumiwa hao na ambaye alikimbizwa katika hospitali ya halmashauri ya mji wa makambako ambapo mtuhumiwa alifariki dunia kabla hajafikishwa hospitalini.
Aidha, Temu amebainisha aina ya silaha waliyoikamata kuwa ni Long Life Caliber 22mm yenye namba za usajili A 194300 ambayo ina Darubini ya kuona mbali na kuongeza kuwa silaha hiyo imetengenezwa nchini Czech na ilikutwa ikiwa na risasi tano zilizo kuwa kwenye magazine.
Chanzo: Blogs