Njombe: Mjamzito Abakwa na wanaume 4

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Mwanamke ambaye ni mjamzito Mkazi wa Mtaa wa Joshoni Halmashauri ya Mji wa Njombe amebakwa na Wanaume wanne kwa masharti ya kutokupiga kelele akiwa ametishiwa kuuawa huku akiwa amefungwa kitambaa mdomoni pamoja na kamba mikononi.

Mwanamke huyo amesema tukio hilo lilimtokea July 10,2022 majira ya saa saba usiku nje ya nyumba anayoishi huku Wanaume hao wakihitaji fedha kabla ya kufanyiwa ukatili huo.

“Nilikuwa nimelala nikasikia komeo inachezewa, nilipofungua mlango Watu wanne wakaingia wawili wakiwa wameshika panga na wawili wakiwa wameshika visu wakapekua kwenye pochi na kuchukua hela pamoja na simu iliyokuwa kitandani”

Aidha Mwanamke huyo amesema mara baada ya kupekuliwa kwa lengo la kuhitaji fedha zaidi na kushindwa kuzipata kwa kuwa hakuwa na kiasi kingine ndipo walipomuamuru kutoka nje kwakuwa ndani alikuwa amelala na Mtoto wa jirani yake na kumfanyia ukatili huo akiwa amefungwa kitambaa mdomoni na baada ya kumaliza kitendo hicho waliweza kuondoka na nguo zake za ndani.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Joshoni, Amon Swale amekiri kutokea kwa tukio hilo katika Mtaa wake na kusema Serikali ya mtaa imejipanga kuitisha mkutano wa dharura ili kujadili kwa pamoja kwa kuwa licha ya tukio hilo lakini siku za karibuni kumekuwa na matukio mengine yakiwemo ya uporaji na uvunjaji wa nyumba nyakati za usiku.
 
Ina maana hao wabakaji hawajakamatwa

Watu wa iringa vp tena mbona mtatuaangusha

Ova
 
Ukikamata watu kama hawa na kujiridhisha ni wenyewe wahusika, huhitaji kupepesa macho bali unatoa figo zao na kuziuza, kiasi cha hela apewe mhanga na fedha nyingine zikajenge shule watu wasome wapate maarifa.

Jela sasa tuwe tunahifadhi wezi wa hela kwa kutumia akili tu, tuwe tunahifadhi wezi wa teknolojia, tuwe tunahifadhi wezi wa kwenye mabenki. Wapumbavu wengi hakuna kututia hasara ni risasi tu na kutupa maiti kuozesha miili yao kwa ajili ya research au watolewe figo na viungo viuzwe tujenge nchi.
 
Mwanamke ambaye ni mjamzito Mkazi wa Mtaa wa Joshoni Halmashauri ya Mji wa Njombe amebakwa na Wanaume wanne kwa masharti ya kutokupiga kelele akiwa ametishiwa kuuawa huku akiwa amefungwa kitambaa mdomoni pamoja na kamba mikononi.
Ingekuwa ni CHADEMA wamefanya mkutano mpaka leo wangeshakamatwa.
 
Back
Top Bottom