Njombe: Mchungaji awatandika viboko waumini kama njia ya kutubu

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
132
1,000
Kanisa hilo la Baptist mkoani Njombe linatumia viboko kama sehemu ya waumini kutubu na kusamehewa dhambi zao.

Aidha siri imevuja baada ya muumini mmoja kujeruhiwa kwa viboko.

Baada ya waumini kukiri dhambi zao ,lazima watandikwe viboko kama sehemu ya utakaso.

Haya mambo ya viboko kumbe ni msingi wa Imani za watu, Tutegemee Taifa la kucharazana bakora kuanzia mwakani.

Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,213
2,000
Ni sawa tu kwa maana unapoenda kutubu dhambi zako kwa Padree au Mchungaji mwishoni atakupa malipizi ya dhamibi ulizo fanya sasa inategemeana, anaweza kukuambia ukafyeke uwanja wakanisa kila siku asubuhi na jioni kwa siku 30, au usali sala fulani mara kumi kila siku ama ufagie kanisa kwa mzwezi mzima au akutandike bakora kama alivyoamua huyo mtumishi ... na ili toba yako iwe kamili lazima utimize malipizi uliyopewa.

Yeye aliona atoe malipizi hayo kwao tatizo liko wapi na hulazimishwi kama hutaki unaacha. Sasa mtu anakuja kutubu kamsaliti mumewe/mkewe, au kaiba au kaua mtu si bora umkung'ute hizo mboko kadhaa akujutie dhambi zake huko na familia yake usifanye tena dhambi ..... Congole kwake mchungaji
 
GKado

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
616
1,000
Zamani katoriki kulikuwa na dhambi za malipizi zinahesabiwa Kama una dhambi 10 unapatiwa adhabu ya kufyatu tofali, kujenga na kazi mbalimbali.

Kumbe wamisionali walikuwa wanatumia ujanja wa kupata vibarua ili kujeng mkanisa yao.​
 
Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
7,608
2,000
Ukisikia ujinga ndiyo huu, yaani mtu mzima kabisa na pumbu zilizojaa mvi ukiwa na akili zako timamu unakubali kudanganywa namna hii? Hizi dini za kisanii ndizo zimepotosha watu akili sana hapa Afrika.
 
ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,189
2,000
Nadhani ile dhana ya kuchapa kazi imeeleweka vibaya inabidi potus itoleee ufafanuzi
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
1,761
2,000
Ni sawa tu kwa maana unapoenda kutubu dhambi zako kwa Padree au Mchungaji mwishoni atakupa malipizi ya dhamibi ulizo fanya sasa inategemeana, anaweza kukuambia ukafyeke uwanja wakanisa kila siku asubuhi na jioni kwa siku 30, au usali sala fulani mara kumi kila siku ama ufagie kanisa kwa mzwezi mzima au akutandike bakora kama alivyoamua huyo mtumishi ... na ili toba yako iwe kamili lazima utimize malipizi uliyopewa.

Yeye aliona atoe malipizi hayo kwao tatizo liko wapi na hulazimishwi kama hutaki unaacha. Sasa mtu anakuja kutubu kamsaliti mumewe/mkewe, au kaiba au kaua mtu si bora umkung'ute hizo mboko kadhaa akujutie dhambi zake huko na familia yake usifanye tena dhambi ..... Congole kwake mchungaji
Msamaha unaotolewa na Mungu ni free of charge.Ndiyo yale yale yaliyo semwa na martini Luther.Wokovu haunuliwi,tumepata bure tutoe bure.

Huu ni upotoshaji uliofanywa na kanisa la zamani sana,kwamba unapewa cheti cha msamaha wa dhambi na padre
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom