Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mganga aliyeuawa ametambuliwa kuwa ni mkazi wa Kafundo - Ipinda Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Dotto Mwaipopo (41) ambaye amechomwa kisu ubavuni kwa madai ya kumtapeli fedha mfanyabiashara huyo
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukuka, amesema mauaji hayo yametokea juzi saa nane usiku
Amesema mtuhumiwa huyo alifanya tukio hilo kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kutotimiziwa ahadi yake
Lukuka amesema katika tukio hilo, mtuhumiwa alijeruhiwa kwa kupigwa na wananchi na amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa matibabu huku akiwa chini ya ulinzi
Amesema mtuhumiwa alikuwa na wenzake wawili ambao wote wanadaiwa kufanyiwa utapeli na mganga huyo lakini baada ya mauaji hayo walikimbia.
Chanzo: Mwananchi