Njombe: Hivi yale mashamba makubwa ya chai yanamilikiwa na nani au kampuni gani?

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Kwanza kabisa nipende Kutoa Pole kwa Watanzania wote kwa Kuondokewa na aliyekuwa Rais wa JMT, pia niwape pongezi SADDIST wote waliofurahia kifo cha Hayati JPM.

Baada ya kusema hivyo naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kwa wale ambao walishasafiri kutoka Makambako kwenda Mjini Njombe,katikati ya eneo lote hilo Kuna mashamba makubwa ya CHAI ambayo kila nikipita nakuta yako safi kabisa.

Pia,Kutoka Njombe Mjini kuelekea wilaya ya Ludewa,kuna mashamba makubwa yaliyopangwa kwa majina ya Vitalu ya Zao hilo la Chai.

MASWALI:

1. Mashamba hayo yanamilikiwa na mtu gani au Kampuni gani?

2. Ni akina nani wanashughurika kuhakikisha yapo safi mda wote? Ni watu au Mitambo?

3. Je,Zao hilo linaongezewa Thamani hapahapa nchini kwa viwanda vipi? Au linapelekwa nje katika mtaifa gani?

EWE MTANZANIA MZALENDO SHIRIKI KATIKA HARAKATI ZA KUWEKA SHINIKIZO LA KUDAI KATIBA MPYA KWA WATAWALA WALIOKO MADARAKANI.
 
Sorry but for the status.. upande wa JPM kulikuwa na SADDIST na ali wa support bila yeye kujua.
 
Yalikua majizi yanatumwa na mabeberu,ntahakikisha matajiri wanaishi kama mashetani (wafie wanu wasigare wanu)
 
Yanamilikiwa na chai bora na product n hii chai bora tunayokunywa siku zote 😋😋😋
 
Yanamilikuwa na Mufindi Tea Company - ni wahindi walinunua toka Serikali ya Tanzania - hatujui ni kwa % ngapi share au ndiyo Tanzania haina chake inasubiri kodi tu.
 
Wahindi wamenunua kampuni toka kwa mwingereza wameshindwa kuiendesha kampuni wanazurura na kumywa chai ofisini
Wameharibu kila lililoachwa na mwingereza
Hakuna uzalishaji wanaganga njaa na vishirika vya ovyo ovyo vya kilimo in other words kuna schemes nyingi zimeanzishwa kuwadhulumu wakulima
 
Naona majibu ni mengi sana hata sijaelewa mmiliki halali ni nani?
 
Mashamba ni ya Unilever Tea Tanzania Limited.. Kampuni Binafsi ya Uingereza.. Pia kuna baadhi ya Mashamba Madogo ambayo ni ya watu binafsi ambao huuzia chai zao UNILEVER.

Last time natoka Pale kulikuwa na Tetesi wanataka kumuuzia Mhindi.
 
Yale mashamba ya kibena estates yanamilikiwa na unilever(T)ltd wazungu kutoka uingereza na yale kama unaenda ludewa yanamilikiwa na Mufindi tea company ltd ni mali ya mzungu anaitwa Gawi ana mashamba mengi mufindi kuanzia itona ila haieleweki kama serikali ilimuuzia au kumkodishia maana mashamba yalikuwa ya serikali
kuhusu kuchakata viwanda vipo lugoda,luponde na itona chai grade one yote husafirishwa uingereza haya hakuna mtu mweusi wa kawaida hujatumia ni kwa matumizi ya ulaya tu makapi huchukuliwa na kupelekwa mafinga huchakatwa upya na ndo haya tunayatumia
 
Back
Top Bottom