kilagalila
JF-Expert Member
- Nov 8, 2018
- 320
- 154
Bibi mjane ambaye amefahamika kwa jina la TULAHUMBA KILAMILA mwenye umri wa miaka 80 na mama ambaye amejitambulisha kwa jina la DORICY MWINAMI mwenye miaka 46 wote wakazi wa kijiji cha ilembula wilayani wanging'ombe mkoani njombe wamekilalamikai chama cha mapinduzi ccm kwa kujumuisha nyumba zao kuwa ni mali za chama hicho.
Akizungumza na kituo hiki bibi huyo amesema kuwa hali hiyo imetokea pindi zoezi la uhakiki wa mali za chama hicho ukiendelea wilayani wanging'ombe ,ambapo ameshangazwa kuona nyumba yake ambayo ameijenga kwa ajili ya vibanda vya biashara ambayo amejenga kwenye eneo lake halali ambalo amelimiliki mwaka 1961 limejumuishwa kuwa ni mali ya chama hicho bila ufafanuzi wowote.
"Tulionaga maandishi tu mimi nimefika hapa tangu stini na moja tukanunua jengo hili tukanunua juu na chini sasa ilipofika 73 ulianza ujamaa wakaomba wajenge godauni akawapa wakajenga sehemu huku kwingine nikawa na lima ujamaa ukaisha wakapangisha mtu sasa tunaona juzi tena wameandika ccm mnisaidie jengo langu sasa wakati mimi najenga mlikuwa wapi"alizungumza bibi
Aidha DORICY MWINAMI amesema kuwa eneo hilo ni mali yao kwa kuwa awali walilianzimisha eneo hilo kwenye ofis za serikali kwa ajili ya ufugaji wa kuku lakini baada ya serikali kushindwa kuendeleza mradi huo eneo hilo lilirejeshwa kwao na mpaka sasa wanalimiliki lakini anashangazwa kuona chama hicho kwa sasa kinasema ni eneo lao.
Naye katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani wanging'ombe REUBEN NYAGAWA amethibitisha kufanyika kwa zoezi hilo la uhakiki wa mali za chama hicho na kueleleza kuwa zoezi hilo linafuata taratibu zote kulingana na mali ambazo zipo kwenye orodha kwa makatibu wa chama hicho.
"ni kweli kuna zoezi la uhakiki wa mali za chama linaendelea kila kata na vijiji lakini kuna vitu ambavyo vinazingatiwa maana kulikuwa kuna watu kujitaifishia mali za chama cha mapinduzi na tunapofika kila eneo tumekuwa tukitoa elimu kwamba tunahakiki mali za chama kwa kuzingatia mwongozo na tumekuwa tukishirikisha wazee wale waasisi wa chama cha mapinduzi kwa hiyo kwa katibu wa chama kata tunaorodha za mali zote za chama kwahiyo tunajiridhisha kama mtu amejenga kwenye kiwanja cha chama basi huyo anakuwa amevamia eneo la chama"alisikika katibu Nyagawa
Hata hivyo katibu mwenezi huyo amesema kuwa licha ya zoezi hilo kufanyika lakini kwa baadhi ya maeneo ambayo wananchi washajenga nyumba za kuishi hawewezi kuhamishwa katika nymba zao ,japo kwa wale ambao wamejenga vibanda vya biashara katika maeneo ya chama hicho watapewa muda,Pindi fedha zao za ujenzi zitakapo patikana basi majengo hayo yatakuwa chini ya chama hicho.
MWISHO
mr.mtaani
SAUTI HIZI HAPA CHINI