Njombe bus terminal jimboni kwa Makinda aibu tupu inalalamikiwa kwa ubovu

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
IMG_8897.JPG IMG_8904.JPG IMG_8906.JPG IMG_8909.JPG IMG_8913.JPG IMG_8914.JPG IMG_8911.JPG IMG_8912.JPG
Madereva na abiria wanaotumia stendi ya Njombe mjini ambayo ni stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani wamelalamikia ubovu wa stendi hiyo na kumwomba mbunge wa jimbo hilo Anne Simamba Makinda kushughulikia tatizo hilo.

Wakizungumza na mtandao huu wa Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima:: madereva hao na wananchi walisema kuwa ubovu wa stendi hiyo umekuwa ni kero kubwa kwao na kuiomba Halmashauri ya mji wa Njombe kulishughulikia suala hilo

John Sanga ni mmoja kati ya madereva eneo hilo la stendi alisema kuwa wameshangazwa na hatua ya mbunge wao ambae ni spika wa Bunge kushindwa kuwajibika kwa kusimamia utengenezaji wa stendi hiyo.

Kwa alisema wakati wa jua eneo hilo limekuwa likiongoza kwa kuwa na vumbi na wakati wa masika linaongoza kwa kuwa na tope sana .

Hata hivyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya Njombe umekuwa ukitoa ahadi ya kutengeneza stendi bila kutekeleza kwa wakati na pale madereva wanapotaka kugoma wamekuwa wakitumia polisi kuwakamata waanzilishi wa migomo hiyo.

Huku Sarah Ndelwa ambae ni mmoja kati ya abiria waliohojiwa akimtaka mbunge Makinda kusaidia kuondoa aibu hiyo ya ubovu wa stendi nyumbani kwake
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
yupo bungeni anazima hoja za upinzani,.

Kati ya wabunge wa muda mrefu bunge ambao walianza vijana na sasa wamezeekea bungeni Makinda ni mmoja wapo, lakini kwa miaka yote ameshindwa hata tu kuboresha bus terminal wakati mabasi hayo hulipia ushuru yatumiapo kituo hicho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom