Alexander The Great
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 4,502
- 23,581
Habari Wana Jamvi,
Zaidi ya biashara 140 zimefungwa Njombe ndani za siku 90, kuanzia January 2021 mpaka March 2021, kutokana na sababu tofauti tofauti, miongoni mwao madeni na masoko kufa.
Kwa ufupi,
Taarifa hii imewekwa wazi na Manager Msaidizi Wa Mamlaka Ya Mapato Mkoa Wa Njombe, Bwana George Mapunda, katika kikao cha Ushauri Wa Mkoa kilichofanyika Njombe.
Amesema; Biashara nyingi sana zimefungwa ndani ya muda mfupi wa siku 90, kwasbabu ya wananchi kuwa na elimu ndogo juu ya ulipaji kodi, licha ya TRA kuwa na kitengo maalum cha Ushauri Kwa Walipa Kodi. Sambamba na kuwa na mikopo mibaya.
Nukuu; "Team kutoka Makao Makuu na hapa mkoani zimekua zikienda nyumba kwa nyumba kutoa elimu ya ulipaji kodi, wamekwenda Ludewa, Makambako na Njombe, na muendelezo bado upo, kwa madhumuni ya kuendelea kutoa elimu ya ulipa kodi kwa wananchi".
Amesema, biashara ndogo ndogo hutozwa kodi kwa kulingana na kumbukumbu za mauzo (Sales Record) ambayo ipo kisheria, kwa kutumia mashine za EFD wanauwezo wa kujua ni kiasi gani wanapaswa kulipa kama kodi stahiki.
Lakini, amesema kama mlipa kodi hato ridhika na makato ya kodi basi ana haki ya kwenda kupeleka malalamiko yake ngazi za juu, ili yafanyiwe kazi.
Amesema, nukuu; "Tuweke wazi, kwamba TRA haifungi biashara za watu, kuna watu wanadaiwa na TRA ila hatuwafungii biashara zao. Tunachofanya ni kuwaita na kuingia nao mikataba walipe madeni kwa awamu".
Nae RC wa Mkoa Wa Njombe, Engineer Marwa Rubirya, amewaasa TRA kufuata misingi na mapendekezo ya Rais Samia Suluhu kuhusiana na jinsi ya kukusanya kodi na mapato mengine.
Amesema, TRA wanapaswa kufuata taratibu na busara kwenye kukusanya kodi na kuwashawishi wananchi kulipa kodi kwa njia rafiki, sio kutumia nguvu na mabavu.
Amakweli "WAFANYABIASHARA (Wakubwa & Wadogo)" wameishi kama mashetani katika utawala wa Awamu Ya 5.
- Shukrani The Citizen.