TANZIA Njombe: Anthony Mwandulami Afariki Dunia. Alijijengea kaburi la mamilioni ya shilingi

Kuna story nilisikiaga kua jamaa alifika.makambako alikua anataka aende iringa sasa kuna kuna mpga debe mmoja kihelehe kikamshika kamnyanganya begi jamaa bila kuuliza anakoenda aise jamaa akamwachia begi likapelekwa kwenye gari inayoenda mbeya aise unaambiwa ile gari ikawa haiwaki
 
View attachment 1840225View attachment 1840223

Dokta Anthony Mwandulami mganga maarufu kutoka Kijiji Cha Itunduma kitongoji Cha wangama Kata ya Mtwango mkoani Njombe Afariki Dunia usiku wa Jana jijini Dar es Salaam.

Mganga huyo aliyejipatia umaarufu nchini baada ya kujijengea kaburi lake la mamilion ya fedha ambalo alisema atazikwa yeye na wakeze watatu.

Dokta Mwandulami alichukua uamuzi huo wa kujiandalia makazi ya milele kitendo kilichowashangaza wananchi wengi hapa nchini.

Taarifa zaidi nitazileta Kwa update!

Zaidi, soma: Njombe: Mganga wa kienyeji Mwandulami ajijengea kaburi la mamilioni, anamiliki magari ya kifahari
Hatimaye kafa kweli ...bado JDee
 
Mbona siku hizi hawaji au madini yameisha? Bro uliongea pumba mbaya sana hadi niliona aibu mimi.
wewe jamaa buana Kama niliongea pumba kwanini hukufanya utafiti unijibu Kwa fact
Wale wameadvance kwenye technology Leo huwezi waona Kwa macho kwani hujawahi sikia juu ya viumbe Alien kuja juu ya uso wa dunia?

Ndio hao hao ila jina limebadilika tu!
 
Mleta uzi amemuelezea huyu jamaa utafikiri ni daktari wa kisayansi,kumbe ni mganga wa kienyeji

Ova
mkuu hapana nilivyomwelezea ndio hivyo hivyo anafahamika na wengi yeye anafahamika Kama Dr sababu ana mbaka Clinic ya tiba Asili Kama kina Dr Mwaka ukienda kikawaida unapata huduma ya kawaida maana alikua na ofisi ya kisasa kabisa
Ila ukienda kindumba ndumba hapo sasa ndio anakupeleka kilingeni kwake akaone upande wa pili !
 
Hatimae mwili umewasili Leo mchana ukitokea Dar es Salaam nimepata taarifa baada ya kuufikisha nyumbani Kijiji Cha Itunduma kitongoji Cha wangama Sasa wanautoa na kupeleka huko inakodaiwa ndio Kuna taratibu za kiganga wanaenda mfanyia Kwa wakuu wa vilinge ndipo Sasa hatua za mazishi zifuate
 
So story yake imeishia hapo.Anatukumbusha kwamba sisi ni Binadamu tuu. "Memento Homo".Tusije tukasahau,kwamba sisi ni binadamu tuu.Fedha na Dhahabu ni mali ya Bwana Full stop.

So hata lingekuwa kaburi la trilioni halina masaada wowote kwake kwa hapo alipofikia

Polen wafiwa wote na wote walioguswa
MEMENTO MORI.
 
Back
Top Bottom