TANZIA Njombe: Anthony Mwandulami Afariki Dunia. Alijijengea kaburi la mamilioni ya shilingi

Jamaa alikuwa kajisahau akawa anapanga mipango yake taratibu wakati maandiko yanasema hivi,"maana ninyi wenyewe mnajua yakini yakuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku".1Wathesolanike 5:2...
Alijisahau vipi ikiwa alitambua kuna kifo na IPO siku yeye pia atakufa na kuamua kujijengea kaburi lake na wake zake watatu. Ni Nani Kati yako na yeye ambaye amejisahau?
 
View attachment 1840225View attachment 1840223

Dokta Anthony Mwandulami mganga maarufu kutoka Kijiji Cha Itunduma kitongoji Cha wangama Kata ya Mtwango mkoani Njombe Afariki Dunia usiku wa Jana jijini Dar es Salaam.

Mganga huyo aliyejipatia umaarufu nchini baada ya kujijengea kaburi lake la mamilion ya fedha ambalo alisema atazikwa yeye na wakeze watatu.

Dokta Mwandulami alichukua uamuzi huo wa kujiandalia makazi ya milele kitendo kilichowashangaza wananchi wengi hapa nchini.

Taarifa zaidi nitazileta Kwa update!

Zaidi, soma: Njombe: Mganga wa kienyeji Mwandulami ajijengea kaburi la mamilioni, anamiliki magari ya kifahari

Mwanaye nilisoma naye naye alifariki kwa upenzi siku hiyo simba ilishinda akaenda kulala kwenye reli pale yombo
IMG_7519.jpg
 
Kwahio hela ya ubwabwa nayo aliacha au tutachangishana?
mkuu ngoja nitakuletea mrejesho Kama ubwabwa wamechangia ila marehemu aliwekeza Sana kwenye kilimo Cha mpunga huko ubaruku mbarali district nahisi watabeba tu kwenye maghala yake ndugu zangu wa pale Mtwango wale wavimbiwe washushie Ulanzi na ughimbi murua!

Nadanganya wana Njombe?
 
View attachment 1840225View attachment 1840223

Dokta Anthony Mwandulami mganga maarufu kutoka Kijiji Cha Itunduma kitongoji Cha wangama Kata ya Mtwango mkoani Njombe Afariki Dunia usiku wa Jana jijini Dar es Salaam.

Mganga huyo aliyejipatia umaarufu nchini baada ya kujijengea kaburi lake la mamilion ya fedha ambalo alisema atazikwa yeye na wakeze watatu.

Dokta Mwandulami alichukua uamuzi huo wa kujiandalia makazi ya milele kitendo kilichowashangaza wananchi wengi hapa nchini.

Taarifa zaidi nitazileta Kwa update!

Zaidi, soma: Njombe: Mganga wa kienyeji Mwandulami ajijengea kaburi la mamilioni, anamiliki magari ya kifahari

Poleni sana...Hilo jumba halitamsaidia chochote
 
Back
Top Bottom