Njia zinazotumika kufunga Simu na usalama wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,858
2,000
NJIA ZA KUFUNGA KIOO CHA SIMU NA USALAMA WAKE (SCREEN LOCK)

SLIDE TO UNLOCK: Hii ni njia rahisi na isiyoshauriwa kutumika. Kuweka hii ni sawa na kufunga mlango kisha unaweka jiwe dogo ili usifunguliwe

PIN CODE LOCK: Hizi ni namba zinazotumika kufunga screen ya simu yako. Ni njia kongwe zaidi ya ulinzi wa simu ambapo mmiliki anapaswa kuzikumbuka namba hizo wakati wote

PATTERN LOCK: Hii si njia kongwe bali imetokana na Maendeleo ya Teknolojia. Njia hii imekuwa ikikosolewa sana na wataalam wa #UlinziWaKidigitali. Inaelezwa ni rahisi kwa mdukuzi kukariri mchoro ama 'pattern' zako.

FINGER PRINT LOCK: Njia hii inahusisha matumizi ya alama za vidole vya mmiliki wa simu. Kila anapotaka kuitumia simu yake basi lazima aguse kwa kidole alichosajili ili simu ifunguke. Njia hii ni bora ingawa ina changamoto kadhaa. Mdukuzi anaweza kujaribu vidole vya mhusika awapo usingizini au akiwa kwenye hali ya kulewa

FACE ID LOCK: Utambulisho wa sura unatumika kufungua screen ya simu. Teknolojia hii kwa kiasi kikubwa ilianza kutumiwa na Kampuni ya Apple. Hii si maarufu na hakuna ushahidi wa wazi kuhusu udukuzi unaoweza kufanywa dhidi ya 'Face ID'

EYE LOCK: Kila mwanadamu ana jicho la tofauti na mwengine. Utofauti huu ni nyenzo inayotumika katika ulinzi wa simu. Matumizi yake si makubwa ingawa inatajwa kuwa na usalama wa juu

PASSWORD LOCK: Hii ni njia rahisi na maarufu zaidi. Ni salama na inashauriwa zaidi ingawa mmiliki anapaswa kufuata vigezo vyote vya utengenezaji wa nywila
 
Uwezo wa Kawaida

JF-Expert Member
Sep 22, 2015
801
1,000
PASSWORD LOCK: Hii ni njia rahisi na maarufu zaidi. Ni salama na inashauriwa zaidi ingawa mmiliki anapaswa kufuata vigezo vyote vya utengenezaji wa nywila
kuhusiana na password pita hapa
 
Gushlevivan

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
2,194

Eye Lock ipo kwenye simu ipi?
 
Masseto

JF-Expert Member
May 14, 2020
585
1,000
Huo mfumo wa face ID niliwahi kufungua simu ya HUAWEI kwa kutumia picha ya mmiliki iliyopo kwenye screen ya simu ingine nikaionesha tu na ikafungunga,

Nonsense
 
SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,483
2,000
Mimi patterns zangu zinawaachaga watu hoi na hata wakati nafungua huwa sifichi simu yani nampigia mkorogo mpaka anaona kizunguzungu

Unasikia tu mtu anasema, "eeee" huyu jamaa ana signature ya hatari hata huwezi iba aisee.

Sent from my cupboard using mug
Screenshot_20210918-202301.jpg
Screenshot_20210918-202352.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom