singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
RAIS John Magufuli amepiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi bila idhini ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuvilinda viwanda vya kuzalisha bidhaa hiyo nchini.
Kutokana na hatua hiyo, viwanda vya ndani ya nchi sasa vitatakiwa kuboresha huduma zake na kuongeza uzalishaji, kwa kuwa vitakuwa na uhakika wa soko hapa nchini, lakini pia vitatoa ajira kwa Watanzania na kuongeza mapato kwa Serikali.
Katika kuhakikisha viwanda hivyo vinapata uhakika huo wa soko, pamoja na agizo la Rais, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa mkoani Tanga, alimuagiza Mkuu wa Mkoa huo, Mwantumu Mahiza, akutane na Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Jeshi la Polisi, watafute mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.
Majaliwa alieleza kuwa ana taarifa za uwepo majahazi yanayoleta sukari kutoka Brazil na kuagiza bandari zote ndogo ndogo hadi Pangani zidhibitiwe. Sisi pamoja na kumpongeza Majaliwa kwa uamuzi huo, tunamuomba awe mkali kwa watendaji wa mikoa yote nchini yenye bandari ndogo zinazotumika kupitisha magendo ya sukari.
Ingawa tunaambiwa TRA na Polisi hufanya doria kukamata sukari hizo za magendo, sisi tunaona bado kasi yao ni ndogo na kunahitajika kuongezwa nguvu kwa upande wa boti, magari na hata maofisa.
Pia usimamizi kwa maofisa hawa wa doria na ukamataji unahitaji kuboreshwa, mfano kwa Dar es Salaam kwenye bandari bubu eneo la Mbweni kuna taarifa kuwa bidhaa za magendo na hasa sukari zimekuwa zikiingizwa kiurahisi.
Taarifa zinaeleza kuwa majahazi hushusha mizigo usiku na kuingizwa kwenye magari ambayo huegeshwa kwenye makazi ya watu, kisha sukari na bidhaa nyingine hupakuliwa na kuhifadhiwa kwenye nyumba zisizomalizika halafu bodaboda maalumu hupakia magunia ya sukari na kuyapeleka kwenye maeneo wanapoelekezwa hasa Tegeta.
Bodaboda zile zimekuwa zikipishana na mamlaka mbalimbali barabarani, hazikamatwi wala kuhojiwa kiasi kwamba hali hiyo imekuwa ni kama mazoea, watu asubuhi wanapokwenda kazini wanapishana nazo tena zinatia mbwembwe zinapokuwa barabarani.
Tumeona matukio machache sana ya kukamatwa kwa shehena hizo za sukari za magendo kutoka nje kama hivi karibuni mkoani Lindi, ambako kulikamatwa mashua ikiwa na sukari mifuko 3,725 yenye thamani ya Sh milioni 127 iliyoingizwa nchini kutokea Brazil.
Vilevile sukari hizo haziuzwi kwa kificho, zimejaa kwenye maduka na wahusika wanaziona kama si kuwa miongoni mwa wateja, lakini tunashangaa inakuwaje kuwa na ugumu kwenye kudhibiti.
Sasa Serikali imedhamiria kukomesha uingizwaji huu wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu viongeze uzalishaji, hivyo ni vema pia wauzaji wakamatwe na kutozwa faini na ikibidi wasaidie kutaja wanapozitoa sukari hizo.
Sukari hii ya nje kwanza inaingia sokoni na kutumiwa na watu bila kujulikana ubora wake na hata Shirika la Viwango Tanzania (TBS) au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kuzikagua sukari hizo.
Wakati yote yanafanyika katika kudhibiti sukari hizo kutoka nje, ni vema wananchi wapewe elimu ya kuwa wazalendo na kupenda sukari ya Tanzania, ili washhiriki kugomea kununua sukari ya nje na kushiriki kutoa taarifa pindi wanapoona sukari ya nje inauzwa au kuna sehemu inapitishwa kuingizwa nchini.