Njia za kutatua matatizo mbalimbali katika nchi za Afrika

Mar 8, 2021
14
7
Habari wanajamii,

Huu ni ukurasa ambao utakua ni maalumu kwaajili ya kutoa taarifa na maarifa kuhusiana na matatizo yanayozikabili nchi nyingi za Afrika na njia mbalimbali ambazo zinaweza kupunguza au kuondoa kabisa changamoto hizo. Hivyo basi natumai kwamba nitapata ushirikiano katika kupitia maandiko haya kwani hii ni jamii ambayo naamini inapenda kuona jamii ikiendelea. Kwa siku ya leo nitaongelea kuhusu tatizo linalowakumba wananchi wengi na jinsi ya kutatua kama ifwatayo;-

1. Tatizo la tozo za miamala ya simu kuwa juu
Hii ni moja ya changamoto ambayo ambayo inawakabili watanzania wengi kwa sasa ambapo kuna ongezeko la kodi katika miamala inayofanyika katika simu ambayo ilianza kutekelezwa mwezi July 15 ikiwa nu mabadiliko yaliyoletwa na bajeti mpya ya 2021/2022.

Tutaangalia njia mbalimbali kwa kuwahusianisha waathirika wakibwa wa badiliko hilia ambao kwa kiasi kikubwa ni wananchi wa kipato cha chini na kipato cha kati ambapo kwa asilimia kubwa hawajaafikiana na badiliko hili.

Zifuatazo ni baadhi ya njia mbadala zitakazoweza kutumiwa na wanachi hawa ili kuweza kuwaponya na maumivu wanayoyapata;-

(1) Kutumia teknolojia ya blokchen (blockchain)
Nini maana ya teknolojia ya blokchen(blockchain)? Teknolojia ya blokchen (blockchain) ni teknolojia ambayo ilianza kupata umaarufu mkubwa katika miaka ya 2008 ikiwa na dhumuni ka kuubadilisha ulimwengu kutoka katika mfumo wa katikati(decentralized) kwenda katika mfumo usio katikati(decentralized). Mfumo wa katikati(centralized system) ni mfumo ambao lazima kuwepo na kiuongo katikati katika mambo mbalimbali yanayofanyika. Mfano, Unapotaka kutuma fedha kupitia mtandao wa simu ni lazima makampuni ya simu yanayohusishwa katiaka kuratibu mitandao yao wauhakiki na wachukue makato katika kazi yanayofanya kama ilivyokua kwa tigopesa,mpesa na halopesa.

Na hiyo ni njia ambayo wanajipatia mapato yao na kwa ujumla wote wapo chini ya serikali ya nchi husika. Mfumo usio katikati(decentralized) upoje? unafanyaje kazi? Nitakueleza. Mfumo huu hauna mtu au watu wa katikati(middlemen) ambao watahusika katika kuangalia muamala huo na kukata makato makubwa kwakua wana mamalaka ya kufanya hvyo.

Mbadala wake ni kwamba kitu pekee kitakachoweza kuhakiki miamala hiyo ni kompyuta ambazo ni nyingi na hakuna makato makubwa katika kufanya hivyo. Mfumo huu pia unaweza kutumika katika kusaini mikataba mbalimbali ambayo haitohitaji mtu wa katikati kama mwanasheria amabaye atahusika katika kuhakiki mkataba huo na wahusika wakuu ni wale tu wanaosaini. Pia wasanii wanaweza kuwa na uwezo wa kusimamia kazi zao vizuri ambapo hamna mtu amabye atakua na uwezo wa kupata kazi zao kama haijalipiwa tofauti na sasa ambapo mtu mmoja anaweza kupakua wimbo katika mitandao na kuweza kumtumia mtu mwingine na kufanya msanii kutoweza kunufaika na mapato hayo.

Je, ni vipi inaweza kutatua tatizo la miamala kua juu? Teknolojia ya blokchen(blockchain) imeleta aina mpya ya fedha ambayo ipo katika mlolongo wa fedha kutokea kubadilishana bidhaa kwa bidhaa hadi mfumo wa kriptokarensi(cryptocurrency) Ni nini hizi kriptokarensi(cryptocurrency) twende sawa utaelewa. Kriptokarensi (cryptocurrency) ni fedha ambazo ni zao la mfumo wa blokchen(blockchain).

Na hizi ni fedha za kimtandao ambazo hazionekani kwa macho ila zina thamani. Fedha hizi zilianza kujilikana mnamo miaka ya 2009 ambapo mtu asiyejulikana kwa sura aitwaye Satoshi Nakamoto aliakuja na fedha ya kimtandao yaani kriptokarensi (cryptocurrency) iitwayo bitcoin na akaweza kutoa njia ambayo aliitumia katika kuleta bitcoin na ikatumiwa na wataalamu wengine na kuleta aina zingine kama cardano,dogecoin,ethereum na aina nyingi mbalimbali zitapatazo 1000. Je kabla ya Satoshi Nakamoto hakukua na aina ya fedha kama hizi? Jibu ni kwamba zilikuepo lakini hazikua katika mfumo wa blokchen (blockchain) ambapo kulianzishwa kampuni ya DigiCash Amerika mwaka 1989 na chini ya David Chaum.

Kampuni hii ilileta fedha ya kimtandao(digital money) lakini ilihusisha mabenki katika kuhakiki miamala yake. Ilishindwa kuendelea ilipofika mwaka 1998 baada ya kufilisika na ikauzwa kwa kampuni ya eCash. Swali linakuja kama mfumo huu unaweza kutumika katika nchi ya Tanzania. Jibu ni ndiyo kwani kuna baadhi ya watu ambao wanamiliki fedha hizi kwa kuwa nazo katika pochi (bitconi wallets) ambapo wanaweza kutuma na kupokea kwa makato madogo.

Mfano unaweza kutuma bitcoin zenye thamani ya milioni sita(6,000,000) za kitanzania na kuwa na makato ya elfu moja na mia tano(1,840) ambayo ni madogo ukilinganisha na makampuni ya simu. Na ukihitaji kubadilisha bitcoin kwenda Tanzania Shillingi inawezekana kwani kuna mawakala wanaoweza kufanya hvyo.

Hivyo watanzania tunaweza kutumia njia hii kuepuka makato yaliyo makubwa. Andiki lijalo litaangazia katika njia nyingine ya kupunguza ukali wa changamoto ya miamala kuwa juu
 
Back
Top Bottom