Njia za kupata SUMU mpya

fenisher

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
340
707
Kutokana na bado kuendelea na kutumia SUMU ya 1977 ambayo kimsingi sehemu kubwa inakosa kuendana na kipindi kilichopo sasa, Tunahitaji SUMU mpya na si marekebisho ya sheria ndogondogo. Kama kijana nilifikiria ni kwanini watu wanalalamikia mfumo mbovu lakini hawadai mfumo mpya, hasahasa wanaharakati wengi nchini wao ni kulalamika kuhusu mfumo na si kudai mfumo mpya. Vyama vya upinzani vimekosa nguvu na ushawishi kwa wananchi na hili ndio lilikua kundi la kwanza lililokuwa lategemewa katika kudai mfumo mpya.

Katika Harakati za kutafuta njia za kudai SUMU mpya nilipata kundi lingine ambalo lina nguvu kubwa katika jamii na lenye ushawishi mkubwa kweny jamii, Na lenye kuwafikia wananchi kwa haraka.
Ni WASANII NA WATU MAARUFU MITANDAONI...Hilo ndio kundi ambalo linaweza kusaidia kwa asilimia 90 katika kuwezesha kupata SUMU mpya na baadhi yao wanaonyesha utayari kama ukifuatilia mitandaoni, watu hawa wana ushawishi mkubwa na wao wanaweza kutuleta katika mfumo mpya. Usingoje upatwe na tatizo ndo uanze kulalamika, Wasanii kwa pamoja mnaweza kusaidia jambo hili.

Mawazo Huru....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom