Njia za kudhibiti, kukamata mafisadi, changamoto ambazo hukumbana nazo mwalimu wa zamu na mwalimu anayepokea darasa la mtihani wa taifa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,298
8,206
Kusema ukweli maisha yangu nayamegubikwa na historia inayovutia sana na hii ni kwasababu tu imenifanya niwe kijana imara na mwenye kujituma sana.

Nianze kuwarudisha nyuma kidogo kipindi naajiriwa katika shule fulani na kukabidhiwa kufundisha somo la Hisabati kidato cha pili na cha nne. Wakati mwingine nilipangiwa kushika zamu za pale shuleni ambapo katika wiki yangu mimi ndio nilisimama kama kiongozi wa shule, wanafunzi, na mazingira yote yanayozunguka shule.

Mimi ndio nilihakikisha nawatuma viranja wa shule ili wawasimamie wanafunzi wenzao katika shughuli mbalimbali pale shuleni, nilihakikisha wanafunzi wote wanawahi namba kwa lazima, wanafanya usafi wa mazingira yote yanayozunguka shule, wanakua wasafi, na wakati wakiwa madarani wanatulia na kuwasikiliza walimu. Kwenye zamu zangu shule ilikua inakua kimyaaaaaaa. 🤫🤫🤫🤫 Kwenye zamu yangu mwanafunzi aliyekosa namba hakuweza kukaa kwa amani darasani.

Bila kusahau nilisimamia ugawaji sawia wa chakula kwa wanafunzi. Wakati mwingine walimu walipokosekana ilipelekea kuwepo ufisadi wa chakula shuleni. Baadhi ya walimu walifanya ufisadi wa gunia za mahindi, msharage wakati mwingine Hadi matunda yalifanyiwa ufisadi.

Siajabu kunafisadi mmoja kiongozi msosi enzi hizo anajisomea huu uzi hawa ndio mafisadi wa kesho nakwambia. Wanafunzi nao hasa viranja wakati mwingine wanawadhulumu na kuwapunja wanafunzi wenzao vyakula ili wao wajigawie vyakula vingi. Mara nyingi hili linatokea sana kwenye vipindi vya nyama na wali.

Kwa hiyo ilihitaji usimamizi mzuri ili kuhakikisha kuna usawa na haki kuanzia, stoo ya chakula, jikoni hadi kwenye ugawaji sawia wa chakula hicho kwa wanafunzi. Kunawafunzi wengine walidiriki hadi kufisadi uji usio na sukari kisha wao kujigawia mwingi.

Pamoja na yote hayo niliyoyaelezea hapo naweza kusema kazi ya uwalimu wa zamu huwa inachangamoto nyingi sana. Wakati mwingine inakubidi utumie nguvu ili uhakikishe wanafunzi wanakusikiliza lasivyo unaweza jikuta wanafunzi wote wanapiga kelele madarasani, shuleni wanachelewa kufika na usafi wa mazingira ya shule hawafanyi.

Ni kazi ya kuchukiza sana hasa pale unakutana na mwanafunzi mtukutuku alafu anakugomea adhabu huku akiwa tayari kuzichanga nawewe😂😂😂😂😂. Hiyo imewahi nitokea nilipokua zamu ya usiku na asubuhi nimezama zangu kuwaamusha wanafunzi bwenini kuna dogo nilimwasha kiboko cha mgongoni akiwa kwenye blanketi. Dogo, akanigeuzia kibano na kunikunja shati na tai yangu huku ameshikilia kiboko changu. Khaaaa pale sikua na jinsi zaidi ya kupoa tu. 🤗🤗🤗🤗🤗🤗🤗

Hizo zote ni changamoto nilizokumbana nazo kwenye fani ya ualimu. Sasa nikirudi darasani kwanza nakumbuka nilikuta watoto wa form four wamesoma topic moja tu ya form three hisabati, kuna topic inaitwa 'relation' kila topic nikiwauliza watoto wanasema hii hawajasoma ni shida. Ilinibidi nianze kuwapiga msasa upya kuanzia vitopiki vya form two, nikawagonga log kwanza ilikuwaweka sawa, nikajaga nikawagonga set, ilinibidi nitumie hadi muda wa ziada ili kuwanusuru watoto na pepa la NEKTA basi. Na ubaya wa ile shule watoto wakifeli tu lawama zote zinaangukia kwako mwalimu.

Kwa hiyo ilibidi nijitume sana. Mpaka pepa la mwisho linafika nilikuwa nimekata mapindi yote maana nilitumia mbinu moja matata sana, ilinibidi nitumie na hela yangu ya mfukoni ili kuweza kuwahamasisha kuisoma mathe.

Nakumbuka nikaendaga steshonari moja pale mjini nikaburuza tuvitini twa topic zote za hesabu form three nikasambaza darasani watoto walisoma balaa yaani. Watoto muda wote wakawa wanawaza hesabu tu. Pepa wakaja wakafanya, vitoto viribuluza A za kutosha. Lakini kazi niliyokua nayo ilikua ngumu kweli.

Sasa mara nyingi nimekua nikimlinganisha mwalimu na kiongozi wa serikali. Na hiyo ni kutokana na changamoto wanazokutana wakati wa kutimiza majukumu yao kwasababu wote wanawaongoza binadamu. Kuwaongoza binadamu ni kazi ngumu kwasababu kila binadamu huwa anakua na mtazamo wake binafsi. Wakati wewe unamwambia apite njia hii ili afike pale yeye anawaza kupita njia nyingine. Sasa unapokua na kundi kubwa la watu kama analokua nalo mwalimu na kiongozi wa serikali kidogo inakua nichangamoto lazima utajikuta inahitaji kutumia nguvu, uwezo na mamlaka uliyonayo ili kuweza kufanikisha kuingiza mtazamo ulionao kwenye kundi lako.

Nikiwa shuleni nilijikuta muda mwingine natuma kundi la wanafunzi wakanichumie rundo la fimbo za misyeda na misyeda upepo ilikuweza kuwadhibiti wanafunzi watoro, watovu wa nidhamu, wanaochelewa shule na wale ambao hawafanyi usafi wa mazingira. Wakati mwingine nilikua namtandika mwanafunzi asiyesikia viboko hadharani ili abadirike. Na wakati mwingine unakutana na mwanafunzi wako anakueleza kabisa ticha pale kama sio wewe sisi tusingeweza kufaulu, tusingechomoka. Hizo zote ni changamoto.

Changamoto ni nyingi viongozi wetu wanakutana nazo. Na tena usiombe kiongozi awe anaipenda nchi yake na wananchi wake yaani hapo lazima akubali kukutana na changamoto. Kwanini kwasababu anawapenda wananchi wake, na anaipenda nchi yake.

Utakuta moyoni amebeba mawazo mazito ya kuwafanya Wananchi wake waishi maisha ya mazuri katika nchi yao, utakuta labda anapenda nchi nzima izagae miradi ya maana, nchi izagae hospitali zenye vifaa na madawa. Utakuta hata akilala usingizi kitandani anawaza tu wananchi wake, anawaza kulinda fedha za umma, anawaza akusanye kodi nyingi ili apate fedha za kujenga miradi mbalimbali, kutoa ajira na kulipa mishahara mbalimbali. Bado hapahapo nayeye anawaza maisha yake wakati mwingine utakuta anawaza ajenge barabara za rami nchi nzima.

Na ukirudi kwa mwalimu utakuta anawaza wanafunzi wake wote wapate A, lakini utakuta hapohapo kuna mwanafunzi hata D, hawezi kupata, kunawakati mwingine utakuta wanafunzi wako wanapata makalai wote kwenye mtihani wa taifa lakini yote unaendelea kupiga kazi tu.

Ukirudi kwa kiongozi wakati anawaza yote hayo niliyoyaandika utakuta muda huohuo anakumbana na changamoto nyingi sana zinazomzuia kukamilisha hayo. Mafisadi wa mapato, mafisadi wa kodi, wahujumu uchumi, waiba madini, wasaini mikataba ya hovyo na hewa. Vyote hivi ni vizuizi vinavyo mzuia kiongozi kukamilisha mipango yake.

Changamoto ni nyingi sana. Mimi wakati mwingine ukinieleza nielezee vizuizi vinavyopelekea nchi zetu za kiafrika zisiendelee, mm huwa nafikiria nitazitaja hizi point:
1Uwepo wa wala rushwa
2 Uwepo wa wahujumu uchumi
3 Uwepo wa mafisadi ya kodi
4 Uwepo wa mafisadi ya mapato

Mimi ningetoa hizo na point, ya mwisho ingekua ni.

5 Mfumo wa serikali upoje?
Mimi naweza kusema mfumo mzuri wa serikali ni ule mfumo wenye viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa unao msikiliza kiongozi mkuu pamoja na wananchi waliowachagua.

Kumsikiliza kiongozi mkuu ni kutekeleza yale yote yaliyo agizwa na kiongozi wako mkuu.

Na kuwasikiliza wananchi ni kutekeleza zile ahadi zote ambazo uliwaahidi wananchi wako.

Sasa ni njia zipi unaweza zitumia kuwadhibiti na kukamata mafisadi, wala rushwa, na wahujumu uchumi hata kabla hawajavamia fedha za umma. Fuatana na mimi.

Ili kuweza kupambana na fisadi, ni lazima utumie mbinu ya "Mtu/Watu (viongozi wa taasisi)" nyuma yake kuwe na mtu (mfuatiliaji), nyuma ya mfuatiliaji wa kwanza kuwe na mfuatiliaji wa pili na nyuma ya mfuatiliaji wa pili kuwe na mfuatiliaji wa tatu (1 /3).

Sharti ni moja, katika safu ya hao watu watatu hakikisha hawajuani (Yaani nikiwa namaana kwamba hawa wote hawapaswi kujuana) inakua ni siri.

Kisha kila mtu kwa wakati wake akabidhi ripoti ya kazi uliyomtuma kwako na pia hakikisha repoti zote zinashughurikiwa kwa uharaka.

Kwa kutumia mbinu hii ndani ya mwaka mmoja tu ufisadi ndani ya Taifa la utakua ni historia.

Moja ya sifa kubwa ya mbinu hii, inapunguza kulindana. Kwasababu asilimia 98 ya watanzania hasa watumishi na wanasiasa hupenda hulindana kwa kiasi kikubwa hasa ikitokea kuna upotevu wa fedha.

Mwisho nipende kumalizia hivi, kiongozi mzuri ni mwalimu mzuri na mwalimu mzuri ni kiongozi mzuri. Binadamu wanatamaa na mali nyingi, binadamu wana tamaa na fedha nyingi, binadamu wengine wanashinikizwa na watu wao wa karibu ili waibie fedha za kodi au mapato ya serikali. Hivyo panahitajika kujitoa kwelikweli. Naomba huu uzi uwaendee walimu wote wa shule za binafsi za sekondari, wao wanaelewa vizuri nini nimeandika hapa.
 
Back
Top Bottom