Njia ya namna ya kusafisha miguu nyumbani; Pedicure at Home!!

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Leo nakuletea njia ya kuosha miguu nyumbani mara mbili kwa mwezi, kwamba unaosha wiki hii unasubiri wiki nyingine inapita... kisha unaosha tena kwa staili hii. Hii si kwa wanawake tu, hata wanaume wanaweza kufanyiwa haya na wenzi wao kama sehemu ya kuimarisha mahusiano yao. Usione tabu kumfanyia mwenzio pedicure home mbona sio kazi sana! Sasa hebu tuangalie nini cha kufanya

1. ONDOA RANGI KWENYE KUCHA ZAKO.
Nail polish remover na pamba vinahusika hapa. ondoa rangi yote uache kucha chako zikiwa safi. Kama unazikata kucha zako zikate na ulinganishe kulingana na urefu unaotaka. ondoa vinyama nyama kando kando ya kucha kwa kifaa maalumu nadhani unavijua au wembe safi na mpya...

download (9).jpg

Toa uchafu chini ya kucha na kama kucha zimefubaa sana zisugue na ule msasa kifaa kama hii unaweza tumia kusugulia kucha vipo saizi tofauti na maumbile tofauti... Vipo vyembamba ambavyo vinafaa zaidi kwa kusugulia kucha unasugua kwenye kucha na kucha zitatoa unga unga flani hivi ambao ndio unaofanya kucha ionekane imefubaa... Ukiridhika unaingia hatua ya pili.

images (6).jpg


2. LOWEKA MIGUU YAKO
Ndio hivyo hata wanaume wanaloweka hahahahaaaa Hapa unahitaji beseni pana sasa lenye maji ya uvugu uvugu.... Kwenye hayo maji weka mafuta ya Olive oil kidogo... au mchaichai... nilikwambia ndio umuhimu wa kuwa na haya mafuta ndani... Ukiyahitaji nitafute!... ukishaweka mafuta yako...dumbukiza vidonge viwili vya ASPRIN.... hahahahaa kama nakuona ulivyoguna! Yes! Asprin dear!.... Vidumbukize humo kisha sasa unaweza weka tea bag/ filter ya green tea au lavender...zipo madukani teeele!!.... wengine huweka shower gel zao...sio mbaya! loweka miguu kwa dakika 15!!

Foot-soak.jpg


3. SAFISHA MIGUU

Sugua gaga tools!....vifaa ndio hivyo na brashi ndogo juu Tunaita kuremove dead skin!.... tumia tupa zile za kusugulia miguu na brashi kila kona. Sugua unyayo wako barabara hakikisha zagamba zimetoka kabisaaaaaa na mguu hata ukiuangalia unaona ni msafi machoni mwako na mlaini... then unahitaji Sukari ya brown ile...nasisitiza brown!.... weka chumvi kiasi sawa na sukari na miminia Asali utapata uji mzitooo! sugua kwenye miguu hadi karibu na magoti.... sugua kama unachua hivi ...sugua kwenye sugu zote kwa nguvu kidogo sio unapaka paka tu! mchanganyiko uwe hivi ukiridhika, osha miguu yako na maji saaafi! na ukaushe kwa taulo saaaafi

img_0973.jpg


download (7).jpg

4. LAINISHA MIGUU YAKO
Ukishamaliza paka losheni yako au mafuta unayotumia kikubwa yawe na moisturizer!... au unaweza ukapaka kiglycerine chako kwenye miguu... sikushauri hizi gylcerine za kibongo feki nyingi mnooo na zinanata mnooo!

Fanya hivi kwa mwezi mara mbili...ugoko utakuwa msafiiiii, mlainiiii.... utasema na wewe unatoa elfu 30 zako kuosha miguu hahahahaaa ila siku moja moja sio mbaya jamani lakini bajeti kama haziruhusu kujiachia hivyo kwanini usijipe raha mwenyewe... aliyeshindwa kununua meli alitengeneza mtumbwi.... kazi kwako sasa!

MWISHO...
Kama ni mwanamke basi paka rangi zako unavyopenda... nakushauri uwekeze kwenye rangi zenye quality...hata ukiwa nazo chache lakini unazo zenye quality...sio dressing table inajaa marangi ya mia tano mia tano siku mbili tatu imeganda na bado yajaza nafasi kwenye dressing table hahahahaaa... cheap quality inaharibu kucha mwenzangu!



Laura Pettie
 
Nimeipenda hii na ni njia bora kabisa ambayo pia ni salama sana sababu haina kuchangia vitu.
 
Back
Top Bottom