Njia ya mwongo fupi. Sheria msumeno, unakata kote kote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia ya mwongo fupi. Sheria msumeno, unakata kote kote

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mkeshaji, Aug 3, 2011.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mzee mmoja alikuwa na kijana wake ambaye alikuwa akisoma sekondari fulani ya bweni hapa nchini. Kijana huyo alikuwa ni mvivu na mtoro wa shule hivyo kusababisha yeye kushika nafasi ya mwisho darasani kila mtihani unapofanyika. Baba yake aligundua hili lakini kila alipomuuliza kijana alijigamba kuwa yeye ndiye anayeshika nafasi ya kwanza darasani.

  Likizo nyingine ikawa imewadia na safari hii kabla ya kijana kurudi nyumbani baba yake alikuwa amenunua mtambo. Mtambo huu kazi yake kubwa ilikuwa ni kumkamata na kumtikisa mtu pindi anaposema uongo. Kijana akarudi nyumbani na baada ya salamu mazungimzo kati ya kijana na baba yake yalikuwa hivi:

  Baba: Mwanangu safari hii umekuwa mtu wa ngapi?
  Kijana: Kama kawaida baba, mtu wa kwanza. Limtambo likamdaka mikono.
  Baba: Sema ukweli mwanangu.
  Kijana: Nimekuwa wa pili baba. Limtambo likamdaka miguu. Wa tatu. Limtambo likamdaka mbavu....Mtambo ukaendelea kujiviringisha mwilini mwa kijana hadi alipokiri kuwa amekuwa mtu wa mwisho tangu aanze masomo yake.

  Baba akaanza kumwasa kijana wake:
  Mwanangu zingatia masomo kama mimi baba yako, nilikuwa nasoma na kila mtihani nikuwa mtu wa kwanza. Limtambo likamdaka baba mtu. Wa pili...likaendelea kumdaka...wa mwisho likaendelea kujiviringisha.... Likamdaka na kujiviringisha mwilini hadi dingi alipokiri kuwa hakuwahi kusoma shule.
   
 2. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Kwikwikwikwiiiiiiiiiiiii
   
 3. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hahhaaaaaaaa haaaaaaaaa!!!!!!!!!
   
 4. S

  Shery Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha ha! Ya ukweli hii nimeipenda!
   
 5. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Duuuuh!!! inafurahisha sana hii mkuu,
  ndo maana wanasema ukiwa muongo usiwe msahaulifu.
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dingi alitaka kumtia nishai dogo wake, akajisahau kuwa limtambo halina cha dingi wala nani..!
   
 7. Bambanza jr.

  Bambanza jr. JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazee pia mwache uongo! Ukipata div2 mzee anasema alpata div1 oooOH! "Mimi nlikuwa nashika namba moja darasani....!'' je wa mwisho alkuwa nani? Kama wote mlkuwa wakwanza.?
   
 8. egbert44

  egbert44 JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2006
  Messages: 361
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hahahahahahahah dingi kaumbuka imetulia
   
 9. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  dingi ni nouma,,,vp limtambo lenyewe linajuaje kama unadanyanya? hii kali aisee
   
 10. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Wazazi kwa fix hasa dingi ni noma
   
 11. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #11
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Dahhhh
  Kungekuwa na kitu kama hii BUNGENI
  ............. ................. .................
   
 12. K

  Karry JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  duh hii balaaa mdingi naye hakujua masharti ya mtambo
  bo
   
 13. O

  Omary sebene Member

  #13
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka limtambo lingekuwepo serikalini 2singekuwa masikini hata rais angekula kichapo fasta
   
 14. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Najua inapouzwa AD.
  We ni-pm tu tujadili namna ya kuliingiza pale mjengoni.
  Wataumbuka watu!
   
 15. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dingi alijisahau.
  We hujui kuwa kuna madingi huwa wanawaadhibu watoto wao kwa makosa ambayo wao pia wanayafanya..?
   
 16. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,880
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Hadithi yako inatufundisha nini?
   
 17. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "A great thinker" wnt ask such a stupidly qn.
   
Loading...