Njia ya kupata moyo wa mwanaume ni kupitia tumbo lake

ambae haachi hela unachana nae .ila wapo wanaoacha hela wanakutana na wali mchuzi tu
Alafu pia mwengine mfanyakazi alafu huku anasoma evening anarudi saa tatu. Huyu asubuhi anamka saa 11 alfajir. Wanachooka pia

Hayayote yanatokea kwenye jamii yetu. Kwahyo huenda kuna factors nyingi.
Lakini kama anamda na pesa basi hayo ni makosa
 
tageti yangu ya kwanza kuoa ni mwanamke anaejua kupika nitamuoa hata kama yupo ovyo ovyo tu
 
The Way to a Man's Heart is Through His Stomach! Hii ni methali ya kizungu haipo kwenye methali za wahenga wetu wa kiswahili ila ina make sense hata huku kwetu uswazi.

Ni aibu wanawake wengi hawajui kupika, hata kama ni kupika tunapika kwa mazoea yale yale, alipika bibi,mama akarithi na wewe unaendeleza.

Pamoja na mabadiliko na fursa zilizopo wengi hawataki kujiongeza. Asubuhi ratiba ya mama ilikuwa ni chai mkate blueband au kiporo na wewe miaka hii unaendeleza hivo hivo asubuhi unarusha limfuko la mkate, lichupa la chai hata majani hayajakolea na sukari nyiingi na liblue band la kichina pale mezani.

Mume akitaka chai afungue limfuko la mkate achukue anywe chai? Kweli? hamjawai kujiuliza kwanini wanaume wengi ndo wapenzi wa supu kwa mama ntilie? Unadhani hawana nyumba wale, wamechoka mamikate yenu.

Asubuhi weka chai mezani, mkate kidogo, matunda kidogo, maji, juice mayai kidogo, viazi vitamu au magimbi, supu kidogo, nyama kidogo kuku au fishi yaani mtu akifika mezani apumue kabisa.

Niwashauri kina mama hebu tubadilike jamani tuzifunze milo mizuri kwa familia zetu. Ukimpikia mume vyakula vizuri wala hatohangaika. Tatizo uvivu umewajaa wengi muda wa jikoni hawana, hatupo creative. Vyakula ni vilevile wali, pilau tambi kila siku wakati halafu mimafuta miiingi hadi wababa wa watu visukari vinawatesa, vibamia vinaongezeka halafu mnaanza kuchepuka.

Mungu katubariki vitu vingi mno hapa nchini tena bei rahisi ukienda masokoni na elf 20 unarudi na kiroba cha week. Wengi wavivu kazi kununua magengeni bei ni mara tatu elfu 20 unaishia kula kwa siku.

Na nyie wanaume mtununulie majiko mazuri mimi ikitokea nikapata mtu wa kunioa mahari yangu ni awe tayari kununua jiko kali. Kama huna mahari inayotosha kununua jiko wala sitokufikiria.

Miss Natafuta mi huwa si mchangiaji sana humu. Ila kwenye hii mada, nimeshindwa kuvumilia, yaani umenipa somo la nguvu. Kwa kweli wanawake kutoenda sokoni ni janga la kitaifa. Utashangaa vigenge kila kukicha vinaibuka kama uyoga, kumbe chanzo ni uvivu wa kina mamsap wetu?

Kwa kuanzia natafuta jiko la ukweli, baada ya hapo ............... nitaleta mrejesho
 
Bila shaka kuwa njaa huzusha mapungufu katika mwili wa mwanaadamu na huathiri hata namna ya kufikiri kwake, huenda akapata dhiki au wakati mwengine furaha, katika hali kama hizo nafsi ikipata inachokitamani na kukipenda miongoni mwa aina za vyakula hufurahi na kwa hiyo humpenda aliyekitengeneza chakula kile.

Katika wasia wa Umaamah binti Al-Haarith kwa mwanawe wakati wa ndoa yake:
“Angalia kwa makini wakati wa kula na kulala kwake: kwa hakika njaa nyingi huchoma na kukosesha usingizi na hutia ghadhabu”

Kwa hakika mwanamke mwenye kujali wakati wa chakula cha mumewe na akajitahidi kuandaa chakula kizuri zaidi kwa kadiri ya uwezo wake ndie mtu wa karibu zaidi kuupata moyo wa mume wake na heshima yake. Sikusudii wala sipendelei kusema kuwa mwanamke apoteze masaa mengi katika kuandaa chakula, bali apike kile anachokipenda mume wake bila ya kuharibu majukumu yake mengine.

Pindi anaporudi mumewe kutoka kazini na wakati huo huo njaa inamuunguza anakuta chakula kilishaandaliwa na nyumba ni safi na mkewe anamsubiri ili ashirikiane naye chakula, kwa hakika katika hali kama hii ni juu ya Mwenyezi Mungu kuwabarikiri katika mazingira haya mazuri ya kiimani na hii ndio familia iliyobarikiwa.
 
sasa Miss Natafuta si inabidi ujifunze mapishi ili uwezepata mwanaume sasa.... au wewe hutaki fanyia kazi maneno haya?

The Way to a Man's Heart is Through His Stomach! Hii ni methali ya kizungu haipo kwenye methali za wahenga wetu wa kiswahili ila ina make sense hata huku kwetu uswazi.

Ni aibu wanawake wengi hawajui kupika, hata kama ni kupika tunapika kwa mazoea yale yale, alipika bibi,mama akarithi na wewe unaendeleza.

Pamoja na mabadiliko na fursa zilizopo wengi hawataki kujiongeza. Asubuhi ratiba ya mama ilikuwa ni chai mkate blueband au kiporo na wewe miaka hii unaendeleza hivo hivo asubuhi unarusha limfuko la mkate, lichupa la chai hata majani hayajakolea na sukari nyiingi na liblue band la kichina pale mezani.

Mume akitaka chai afungue limfuko la mkate achukue anywe chai? Kweli? hamjawai kujiuliza kwanini wanaume wengi ndo wapenzi wa supu kwa mama ntilie? Unadhani hawana nyumba wale, wamechoka mamikate yenu.

Asubuhi weka chai mezani, mkate kidogo, matunda kidogo, maji, juice mayai kidogo, viazi vitamu au magimbi, supu kidogo, nyama kidogo kuku au fishi yaani mtu akifika mezani apumue kabisa.

Niwashauri kina mama hebu tubadilike jamani tuzifunze milo mizuri kwa familia zetu. Ukimpikia mume vyakula vizuri wala hatohangaika. Tatizo uvivu umewajaa wengi muda wa jikoni hawana, hatupo creative. Vyakula ni vilevile wali, pilau tambi kila siku wakati halafu mimafuta miiingi hadi wababa wa watu visukari vinawatesa, vibamia vinaongezeka halafu mnaanza kuchepuka.

Mungu katubariki vitu vingi mno hapa nchini tena bei rahisi ukienda masokoni na elf 20 unarudi na kiroba cha week. Wengi wavivu kazi kununua magengeni bei ni mara tatu elfu 20 unaishia kula kwa siku.

Na nyie wanaume mtununulie majiko mazuri mimi ikitokea nikapata mtu wa kunioa mahari yangu ni awe tayari kununua jiko kali. Kama huna mahari inayotosha kununua jiko wala sitokufikiria.
 
Aisee furaha ya nyumba ni mwanamke asikwambie mtu...
Mwanamke ni kila kitu nyumbani...

Mzuka wangu nikute menyu ya maana hom.
 
Back
Top Bottom