Njia ya kupata moyo wa mwanaume ni kupitia tumbo lake

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,558
45,829
The Way to a Man's Heart is Through His Stomach! Hii ni methali ya kizungu haipo kwenye methali za wahenga wetu wa kiswahili ila ina make sense hata huku kwetu uswazi.

Ni aibu wanawake wengi hawajui kupika, hata kama ni kupika tunapika kwa mazoea yale yale, alipika bibi,mama akarithi na wewe unaendeleza.

Pamoja na mabadiliko na fursa zilizopo wengi hawataki kujiongeza. Asubuhi ratiba ya mama ilikuwa ni chai mkate blueband au kiporo na wewe miaka hii unaendeleza hivo hivo asubuhi unarusha limfuko la mkate, lichupa la chai hata majani hayajakolea na sukari nyiingi na liblue band la kichina pale mezani.

Mume akitaka chai afungue limfuko la mkate achukue anywe chai? Kweli? hamjawai kujiuliza kwanini wanaume wengi ndo wapenzi wa supu kwa mama ntilie? Unadhani hawana nyumba wale, wamechoka mamikate yenu.

Asubuhi weka chai mezani, mkate kidogo, matunda kidogo, maji, juice mayai kidogo, viazi vitamu au magimbi, supu kidogo, nyama kidogo kuku au fishi yaani mtu akifika mezani apumue kabisa.

Niwashauri kina mama hebu tubadilike jamani tuzifunze milo mizuri kwa familia zetu. Ukimpikia mume vyakula vizuri wala hatohangaika. Tatizo uvivu umewajaa wengi muda wa jikoni hawana, hatupo creative. Vyakula ni vilevile wali, pilau tambi kila siku wakati halafu mimafuta miiingi hadi wababa wa watu visukari vinawatesa, vibamia vinaongezeka halafu mnaanza kuchepuka.

Mungu katubariki vitu vingi mno hapa nchini tena bei rahisi ukienda masokoni na elf 20 unarudi na kiroba cha week. Wengi wavivu kazi kununua magengeni bei ni mara tatu elfu 20 unaishia kula kwa siku.

Na nyie wanaume mtununulie majiko mazuri mimi ikitokea nikapata mtu wa kunioa mahari yangu ni awe tayari kununua jiko kali. Kama huna mahari inayotosha kununua jiko wala sitokufikiria.
 
Back
Top Bottom