Njia ya kupambana na wizi wa atm: Haraka tutumie tehama kikamilifu na kwa upeo wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia ya kupambana na wizi wa atm: Haraka tutumie tehama kikamilifu na kwa upeo wake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BabuK, Jul 31, 2009.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Nduguu wana JF na watanzania wenzangu,
  Nimefuatilia kwenye vyanzo mbalimbali vya habari kwa makini juu ya matukio ya wizi ulitokea wa mamilioni ya mapesa uliotokea kwenye mabenki yetu ambapo wateja wamejikuta wakipoteza pesa kwenye akaunti zao kwa mbinu za hali ya juu…(Japo sio sana maana zinahuisha na walinzi wa vibanda hivyo) na zenye mashaka juu ya ulinzi wa vibanda vya kuchukua pesa maarufu kwa jina la kiingereza ATM ( Automated Teller Machine).

  Miexi kama sita liyopita kulikuwa na onyo kwenye mtandao juu ya wenye akaunti za VISA cards toka USA na Canada wajihadhari kuchukua pesa kwenye ATM za DAR, Tanzania kwani kulikuwa na aarifa za kupoteza pesa zaidi ya zile zilizochukuliwa na na mwenye akaunti. Uvumi huu hivi karibuni umethibitishwa na kukamatwa kwa raia wawili wa kigeni wakiwa kwenye kurina asali kwenye mizinga ya watu ( ATMs) Nukuu:”
  [FONT=&quot]Wazungu wa ATM kortini leo…….[/FONT]
  [FONT=&quot][​IMG][/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Raia wa Bulgaria, Neldko Lazarov Stanchev na Stela Peteva Nadelcheva wanaodaiwa kuiba fedha za Benki Barclays iliyopo katika maeneo ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam[/FONT]
  [FONT=&quot]Raia wawili wa Bulgaria, Neldko Lazarov Stanchev (35) na Stela Peteva Nadelcheva (23), leo wanatarajiwa kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hatua hiyo inafuatia mahakama hiyo kulazimika kuahirisha kesi hiyo wiki iliyopita baada ya washtakiwa hao kumkataa mkalimani.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Washtakiwa hao wanadaiwa kuiba Sh milioni 70 katika mashine za kutolea fedha za Benki Barclays iliyopo katika maeneo ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kumkataa mkarimani huyo, Hakimu Mkuu Mkazi, Warialwande Lema, aliamuru warudishwe Kituo cha Polisi Kati na kufikishwa mahakamani hapo leo[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]CHANZO: NIPASHE [/FONT]
  [FONT=&quot]“[/FONT]
  Taarifa hii na nyinginezo ambazo hazijawahi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari ni kielelezo cha mianya ya jinsi teknolojia mpya ya TEHAMA inavyoweza kutumiwa kufanya madhara na uhalifu kwa jamii….

  Je Tufanyeje kupambana wizi huu na faida zake ni nini??: Naomba wadau wachangie hoja hii lakini wazo langu ni kwamba tunahitaji Full Inter-Banking Services kwa wateja wote kwa benki zote. Hii maana yake ni kwamba:
  ·[FONT=&quot] [/FONT]Mabenki lazima yawe na mtandao wa kushirikiana taarifa ya wateja na akaunti zao kupitia Bank Clearing House ( Nimekosa neno kamili ya Kiswahili)– ambayo itafanya kazi kuwezesha kushirikishana taarifa za kibenki, wateja,mikopo na madeni pamoja na kuwa ndio pekee watoaji wa WATOAJI wa ATM cards, Credit na Debit cards na kufanya shughuli ambazo zitawezesha ufuatiliaji wa mwenendo wa uchukuaji, uwekaji, ulipiaji wa huduma na uhamishaji wa fedha kutoka akaunti moja kwenda nyngine katika benki moja na hata mabenki mengine yaliyo ndani ya clearing house hio. ( Wataalamu wa Benki mnaweza kufafanua hili).

  ·[FONT=&quot] [/FONT]Clearing House itakuwa na jukumu la kutoa hundi zote kwa mabenki yote hivyo kuondoa uwezekano wa kugushi hundi…. Chukua mfano mdogo tu wa vocha za kupigia simu… isivyokubali kutingizwa kwenye simu zaidi ya mara moja… ( IT Systems integration watusaidie kwa hili..nami nina kamchango kadogo..)

  ·[FONT=&quot] [/FONT]Kuweka miondombinu ( Platform & Infractructure) kwa ajili ya kuunganisha wigo wa huduma za kibenki na wadau wa utoaji huduma zitakazowezesha na kurahisisha ulipiaji wa huduma kama vile maji, umeme, simu, kodi, ada, nauli na kadhalka. Eneo hiIi muhimu katika kusukuma maendeleo ya uchumi mbele. ( wataalamu wa Mindombinu ya ujasiriamali – micrifinancing and credit regulation wajikunje kuchangia hli).

  ·[FONT=&quot] [/FONT]Miundombinu hii lazima iwekwe kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano na kusimamiwa na Wizara ya Fedha. Ni aibu kwamba kikundi cha watu wachahe wanavunja usiri wa akaunti za watu na kujichotea mapesa watakavyo bila kudhibitiwa hata kwa uwepo wa askari walindao kweye hizo ATM….

  Faida zake:
  1.[FONT=&quot] [/FONT]Urahisishaji wa huduma za kibenki - kwa mfan nikipaa cheki yangu ninaweza kulipwa mara moja kwenye tawi lang au tawi lolote ili mradi kuna pesa toka kwa aliyenilipa
  2.[FONT=&quot] [/FONT]Mawasiliano ya ufuatiliaji na udhibiti wa mienendo ya kibenki,kiashara,mikopo na mapambano juu ya fedha haramu – Jambo ambalo Mh. Rasi Kikwete amewapa changamoto wana usalama kupambana na uhalifu wa kimtandao… (Cyber crimes… Tunahitaji kuweka msukumo mkubwa na kasi kubwa kwani teknolojia hii inabadilika haraka mno).
  3.[FONT=&quot] [/FONT]Kujenga uwezo wa kuweka akiba kwa watanzania.
  4.[FONT=&quot] [/FONT]Kujenga uwezo na nidhamu ya uwajibikaji juu ya masuala a kifedha kwa wananchi na taasisi. Kwani kosa moja linaukliwa na mtandao mzima wa mabeki….. Hii kaszi a kufuatilia akaunti za mafisadi na wahujumu uchumi mbona ina rahisishwa mno na inadhibitiwa mara moja iwapo miundombinu itafanya kazi inavyotakiwa na kuendeshwa na watu walifundishwa wakaelewa. Hujumu wowote katika mtandao huu utatoa kiashiria ( Alarm) kwa wahusika wote ..jambo ambalo ni MUHIMU kwenye kudhibiti mtandao.
  5.[FONT=&quot] [/FONT]Kuwezesha kutambulika kimataifa na kuwapa wananchi wetu njia ya kupata huduma nje ya mipaka yetu kwa kutumia ATM kadi zetu. Hudma kama vile za e-bay, kulipia ticketi za ndege na malipo ya aina yeyote ambayo Benki Kuu itaridhia kuuatana na sheria zake.
  SAA YA KUPAMBANA UHALIFU WA KIMTANDAO NI SASA..TUSISUBIRI LITOKEE JINGINE..TUJIPANGE KWENDA NA SAYANSI NA TEKNOLOJIA…… JE WIZARA HUSIKA ZA FEDHA NA USALAMA WA RAIA ZINA MKAKATI GANI???
   
Loading...