Njia ya kuongeza kipato: Kilimo cha pilipili kichaa kinavyoweza kumfaidisha kijana wa Kitanzania

Thesis God

Senior Member
Jul 16, 2021
139
275
Habari wanajamvi wenzangu!

Tatizo la ajira limekuwa sugu lakini nimekuja na suluhisho ambalo litaweza kuongeza kipato kwa sisi watu wa chini na hasa waliomaliza chuo na kukosa posts.

Naeleza hiki kutokana na Experience yangu na jinsi nilivyofanikiwa kwa kilimo hiki cha pilipili kichaa (African birds eyes chills).

Kwa sasa mimi nauza pilipili hizi madagascar na nachukua Tani 4 mpaka Tano ila kwa mkulima anayetaka kuanza anaweza akaingia mikataba na hawa wannunuzi wa ndani (na ntajikita zaidi kwa wanunuzi wa ndani).

images (10).jpeg

Picha: Pilipili kichaa ikiwa imetoka kuvunwa

BEI YA SASA KWA WANAOUZA PILIPILI:
Kuna makampuni mengi sana yananunua pilipili kichaa ila kuna kampuni moja ambayo mimi ilinitoa hvyo naiamini sana inaitwa BREDAS TRADERS AND GENERAL SUPPLY CO.ltd
Ambao kwao unaingia nao mkataba kuhusu ukishalima wao ndo watanunua Bidhaa zako na wananunua kwa gharama ya Kilo moja Tsh 5000/=

Kwa heka moja unaweza kutoa Kilo 400 kwa mwezi.

Na ukiweka mkataba nao mbegu watakupa na utakatana nao kwemye manunuzi (bei ya mbegu ni Tsh 200,000/=)
.
400x5000= 2,000,000/= ambayo utaipata kwa heka moja kila mwezi na bidhaa hii baada ya kupandwa hudumu kwa miezi 18 sio uongo ni ukweli nilioupitia mpka sasa naweza kuuza mwenyewe Madagascar.

images (15).jpeg

NINI CHA KUFANYA ILI UFAIDIKE NA FURSA HII
  • Uwe na shamba la heka 3 au muungane watu mtimize heka 3
  • Shamba liwe sehemu yenye kuweza kufikika maji (kwaninkilimo hiki kinaweza kuhitaji maji kwa ajili ya kumwagilia
  • Weka mkataba na mashirika kujihakikishia ununuzi wa bidhaa zako baada ya kulimo
  • Mkataba wako utakufanya upate ushauri wa jinsi ya kulima kwa ubora na ufatiliaji wa mara kwa mara kutoka shirikani

MAZINGIRA YA KILIMO HIKI
Zao la pilipili/pilipili kichaa hupendelea mazingira yenye joto la wastani kuanzia nyuzijoto 18°C - 30°C, joto likiwa chini ya nyuzijoto 16°C au zaidi ya nyuzijoto 30°C huathiri utengenezaji wa matunda. Pia kitu muhimu cha kutilia maanani hapa ni kwamba pilipili kichaa hufanya vizuri maeneo yenye joto. Kadiri joto linavyokua kubwa (mpaka kufikia nyuzi joto 30°C) ndivyo jinsi pilipili inavyozidi kuwa kali na yenye ubora zaidi. Ili kupata pilipili yenye ubora inatakiwa joto lisipungue chini ya nyuzi joto 15°C.

Pia mwanga wa jua ni muhimu sana kwa ukuaji wa mazao mengi ikiwemo zao la pilipili kichaa, hakikisha unapanda zao hili mazingira yenye mwanga wa kutosha, usipande mazingira yenye kivuri, zao hili halitafanya vizuri.

Zao hili hufanya vizuri kwenye udongo tifutifu usiotwamisa maji na wenye kiasi cha tindikali kuanzia pH 5.5 - 7.5

Vilevile hufanya vizuri kwenye maeneo yenye muinuko wa mita 1500 kutoka usawa wa bahari.

Kiasi cha mvua kinachohitajika kwa mwaka ni mm 600 hadi mm 1250. Pia njia mbalimbali za umwagiliaji zinaweza kutumika kuzalisha zao hili kama kutumia mifereji (Stream irrigation), njia ya matone (Drip irrigation), mithiri ya mvua (Sprinkler irrigation) n.k. Chamsingi hapo ni kwamba hakikisha shamba lako lina unyevu wa kutosha wakati wote, maji yakizidi shambani au kukiwa na ukame uzalishaji utaathirika kwa kiwango kikubwa.

AINA YA UDONGO
Hufanya vizuri katika aina tofauti za udongo, lakini zingatia usiwe udongo wa kutuamisha maji.Mmea huu hufanya vizuri unapotumia samadi.

MBEGU
Tumia mbegu iliyothibitishwa na kampuni Utalayoweka nayo mkataba .

KUTAYARISHA KITALU
  • Weka kitalu mita moja upana kwa urefu upendao kulingana na mbegu yako.
  • Elekeza kitalu chako upande ambao jua lisiunguze miche.
  • Piga mistari ya 10 cm na weka mbegu, funika udongo kidogo. Weka manyasi makavu na nyunyizia maji asubuhi na jioni.Zinapoanza kuota, ondoa nyasi na weka kivuli mita moja juu na endelea kunyunyizia maji.

KUPANDA
Panda kachachawa miche ikiwa na majani halisi manne. Itakuwa imefika wiki sita.

PALIZI
Palilia mara mbili kwa msimu kuapata mavuno mengi zaidi
Kwa mazao bora panda mmea huu pekee yake 1 meter x 1 meter. Lakini ukitaka unaweza kuchanganya na mmea mingine.
Weka samadi na baada ya wiki moja weka DAP kuongeza rutuba ya udongo. Pia weka CAN baada ya wiki tatu zaidi.

KUHIFADHI UNYEVU
Tandika manyasi makavu ili kuhifadhi unyevu na kuthibiti hali ya joto la udongo.

MATUMIZI YA PILIPILI KICHAA
Umejiuliza kwanini iwe ni zao la gharama sana wakati wengi tunatumia kuongeza kionjo kwenye Chakula (mboga)
Matumizi ya pilipili dunia ni kama ifuatavyo-
1. Hutumika (Baada ya kufanyiwa chemical production) kuwa kitunzio cha vyakula vya watoto
2. Hutumika katika kutengenezea mabomu ya machozi
3. Hutumika katika kutengenezea maji ya kuwasha kwa polisi
4. Hutumika kutengeneza Dawa za kuua wadudu shambani
Na mengine mengi

SOKO LA PILIPILI BADO KUBWA SANA HIVYO TUJIKITE HUMO
 
Ni fursa Asante sana nina swali kwa maeneo kame na yenye udingo wa kichanga inakuwaje.

2. Risk factors or contributors zingine kama wadudu nk inakuwaje?
3. Je, soko ni hilo tu au kuna masoko mengine?tunaomba connection.
4. Kuna mabwana au bibi sham a unaowafahamu kwa ushauri zaidi hasa kwenye maeneo yenye acid ya udongo kubwa ya 7 au chini ya 5.5
 
Kwa mtu atakayelima chini ya hekari 3,anaweza kuuza wapi?ni mbegu gani inafanya vizuri sokoni?
 
Kwa tz ni maeneo gani ambayo nikilima kampuni/wanunuzi watafika kununua mazao au popote ndani ya tz au ni jukumu la mkulima kusafirisha mazao yake
 
Kilimo cha mitandaoni ni rahisi sana na kina faida kubwa sana. Ingia sasa field uonje joto ya jiwe
Niliendesha gari mpaka tanga kuangalia hizo pilipili, ndugu nilikuta hata wanaoniita nao wamefunga shamba. Wakawa wanatafuta mzembe wamtandike😂😂😂😂. Bad enough aliyenipeleka ni rafiki yangu mzungu yeye akashawishika ,akanishawishi. 9ml in a month. Nikasema weeeee.. twendeee tukachukue shamba hili. 😂😂😂.

Jamani kilimo sio lele mama. Asikuite mtu kwenye kilimo. Ingia mwenyewe tena kutokana na mapenzi yako na kilimo cha aina flani.
 
Niliendesha gari mpaka tanga kuangalia hizo pilipili, ndugu nilikuta hata wanaoniita nao wamefunga shamba. Wakawa wanatafuta mzembe wamtandike😂😂😂😂. Bad enough aliyenipeleka ni rafiki yangu mzungu yeye akashawishika ,akanishawishi. 9ml in a month. Nikasema weeeee.. twendeee tukachukue shamba hili. 😂😂😂.
Jamani kilimo sio lele mama. Asikuite mtu kwenye kilimo. Ingia mwenyewe tena kutokana na mapenzi yako na kilimo cha aina flani.
Duh
 

Similar Discussions

17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom