Njia ya kuendesha nchi bila kodi hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia ya kuendesha nchi bila kodi hii hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RICHEST, Jul 28, 2011.

 1. RICHEST

  RICHEST Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wengi wanaamini nchi ili iende unahitaji utoze kodi.Si kweli.Korea ya Kaskazini inaenendeshwa bila kodi kwa miaka mingi sasa .Na ni marufuku kulipa kodi ya mapato korea.Wanachofanya wao wanaamini serikali haziwezi kuendesha nchi kwa kujiamini kama haina vitega uchumi vyake vya maana ambako itapata mapato yake ya uhakika.Sababu ukitegemea private sector wana matatizo waweza kupeleka puta.Au wakafunga biashara kukukomoa ukubaliane nao.Ndio maana Korea Kaskazini hadi leo ina kiburi cha ajabu haiigopi hata marekani inao uwezo wake kama serikali wa kujiamini.

  Hivyo serikali ya korea kaskazini hutegemea mapato toka mashirika yao ya umma yaliyozagaa kila kona na ya kila sekta.Na ukiharibu uendeshaji wa shirika ukiwa meneja au mtumishi wanakunyonga.Nasikia na Nyerere alipoanzisha mashirika ya Umma alishauriwa hivyo na Abdulahman Babu akiwa waziri wake wa mipango ili aelekee huko pa kuifikisha serikali ijitegemme isitegemee kodi.Na Nyerere alitangaza Siasa ya kujitegemea ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya kujitegemea mtu binafsi lakini pia kwa ajili ya serikali isiwe tegemezi .Lakini viongozi wengi wanasikiliza propaganda za kilevi za nchi za magharibi kuwa nchi haiwezi endeshwa bila kodi na serikali isiwe na vitega uchumi ili makampuni yao yaje yapeleke serikali puta.Hivi kama huna kitega uchumi uwe mtu binafsi au serikali hutakujwa usumbuliwe mbeleni kimaisha au kiserikali?

  Katika jambo ambalo kwa moyo wangu wote naamini Marehemu Mwalimu Nyerere hajatendewa haki na serikali zilizomfuata ni kuua mashirika ya umma.Alianzisha misingi ya kusaidia serikali ifikie mahali ije ijitegemee isitegemee mapato ya kukimbiza machinga na virungu barabarani eti hawalipi kodi. Hivi siku walipa kodi wakubwa wakiamua kufunga biashara zao na kuondoka zao kama ilivyotokea Zimbabwe

  Nafikiri suala la serikali ya Tanzania kuwa na mashirika ya umma lifikiriwe upya kwa usalama wa serikali yenyewe.

  Na mimi nangoja kwa hamu Siku TRA watakapoambiwa hawana kazi maana yake hawa jamaa kiboko kabla hata biashara hujafungua mlango wa duka na hata kabla hujauza hata kibaba kimoja cha unga wameshakukadiria kodi unayotakiwa kulipa serikali.Siku wakiondoka nitacheza CHAN CHAN ngoma ya kihindi na kupiga fataki hewani kusherekea.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  safi sana ushauri wako!tra wamekua miungu watu wananyanyasa sana raia.Tatizo serikali yetu inasema haifanyi tena biashara!
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mungu aepushie mbali hilo maana kwa hii nchi tungebaki wachache sana maana wengi wangenyongwa katika vyeo vya chini kabisa, hebu fikiria leo tungekuwa na kikwete si angenyongwa akiwa level ya umeneja tuu, au leo hii tungemfahamu wapi Chenge?
   
 4. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  inawezekana kufanyika hayo lakini kwa kizazi hichisijui. toka zile enzi za mwalimu alikuwa asilegeze aweke misingi hiyo pale pale. Ama sasa kama haya wote tunayakubali kwa moyo mmoja tuhakikishe yanawekwa ndani ya katiba kuwa mtu yeyote atakaye kabidhiwa kuongoza shirika la umma na likafilisika kizembe afungwe maisha
   
 5. RICHEST

  RICHEST Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana na wewe kuwa Nyerere ilibidi aweke misingi kuanzia mwanzoni lakini naamini Uongozi wa nchi ni kama mbio za kukimbizana vijiti anayepokea inabidi aanzie mwenzie alipoishia na kutimua mbio zaidi ikiwezekana kuliko aliyetangulia.Nyerere alianzisha wengine walitakiwa waendeleze alipoishia.Asingeweza kufanya yote.

  Leo hii aibu kubwa walioua mashirika haya ya umma wako barabarani wanakenua meno na kujiishia kwenye majumba yenye viyoyozi hakuna wa kuwabana.Walau serikali zilizofuata zingewabana hata kwa kupiga kamarufuku kuwa hawaruhusiwi kuajiriwa tena wala kugombea nafasi za kisiasa wala kupewa vitenda serikalini kama wana vikampuni vyao vya sebuleni.
   
 6. Eddy Love

  Eddy Love JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2014
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 12,883
  Likes Received: 6,328
  Trophy Points: 280
  kumbe hii kitu ipo halafu naona itasaidia kupunguza ufisadi
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2014
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hivyo unaona Korea Kaskazi ni best model kweli Akili ni nywele!
   
 8. k

  kajima JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2014
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 867
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  kwa nchi yetu ilipo tunahitaji mifumo yote miwili....
   
 9. East African Eagle

  East African Eagle JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2014
  Joined: Jul 26, 2013
  Messages: 3,768
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 135
  Uchambuzi wako ni mzuri nimeupenda.Lakini kwa taarifa yako tu mashirika ya umma mengine bado yapo na yanafanya vizuri mfano shirila la bandari lakini pia serikali imeanzisha mashirika mengi tu ya umma ila hayaitwi mashirika ya umma yanaitwa wakala wa serikali (agencies) nafikiri serikali iliyopo kwenye mkondo sahihi.

  Mashirika haya yalikuwa yanatoa ajira kwa watu wengi sana iko haja ya kuyarudisha mashirika ya umma na kutokana na shida za ajira zilivyo sasa naamini watakaopewa watashika adabu na kuyasimamia vizuri.
   
 10. k

  kajima JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2014
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 867
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  nafikiri mawazo yapo yako kwenye siasa za nchi hiyo...mada ipo kwenye uchumi bila kodi Fulani....
  umeelewa?
   
 11. TEKNOLOJIA

  TEKNOLOJIA JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2014
  Joined: Jan 6, 2014
  Messages: 4,306
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri ila lina matatizo yake.Nchi ikiendeshwa katika misingi kikomunisti kama ilivyo Korea ya Kaskazini italeta matatizo makubwa mawili kulingana na ufahamu wangu mdogo.Moja,itazuia innovation & creativity;Pili itauwa competition katika masoko ambayo huchangia kuzaliwa kwa innovation.Bado free market na private sector ni players muhimu mno katika kuleta ustawi wa nchi.Uzuri wa private sector ni kwamba zina-bring the best out in individuals as it promotes potential realization by individuals as they fight to achieve higher successes.With the public sector in the driving seat the story will be different,everything will be under the tight control of the government and it has to be done in accordance with the ruling party ideas & ideology and not in accordance with the individuals' innovative & creative ideas.
   
 12. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2014
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Na hapa ndipo palipo na muarobani wa kukata mirija ya kuomba omba....naunga mkono hoja. TUJITEGEMEE
   
 13. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2014
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Unauhakika kweli na unachokisema...!? Kwahiyo Korea ya Kaskazini wao ni watu wa ku'copy' and 'paste' ...ebu watake radhi aisee..!
   
 14. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2014
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Hii nayo kali...agencies ni shirika la umma. Ebu angalia tu Mission na vision za agences na zile za mashirika ya umma zikoje?
   
 15. KeyserSoze

  KeyserSoze JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2014
  Joined: Feb 26, 2014
  Messages: 1,835
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kodi ni Mapato yanayoweza kuendeshea nchi.., kwahio kama kuna njia nyingine ya kupata hayo mapato its well and good, hata haiitaji kuyapata kwenye mashirika ya UMMA, yanaweza kupatikana hata kwenye Makampuni makubwa, migodi na maliasili zetu..., Libya waliweza kuwasomesha watu na kuwapa huduma tofauti kutoka kwenye mapato ya mafuta.
   
 16. uvugizi

  uvugizi JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2014
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,037
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  nafikiri mleta mada ume dadavua vizuri , ni wakati sasa na sisi kujiwekea utaratibu wa kujitegemea lakini tukisubiri hawa wawekezaji na sera za biashara huria kwa mantiki ya kuleta inovations , tutakuwa tunawatajirisha wenzetu na sisi tukiendelea kuwa omba omba , ushindani wa wenzetu ni mkubwa mno , hata tukiimarisha misitu tu tutakuwa tupo juu, na kuuza mbao.
   
Loading...