Njia ya dini kuongeza mauzo ya bidhaa nje hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia ya dini kuongeza mauzo ya bidhaa nje hii hapa

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by RICHEST, Jul 26, 2011.

1. RICHEST

RICHEST Member

#1
Jul 26, 2011
Joined: Jun 23, 2011
Messages: 25
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Tanzania ina dini kubwa nyingi ambazo makao yao makuu yako Asia,Ulaya na Marekani ambako kuna matajiri wakubwa ambao wamekuwa wakileta misaada kila mwaka nchini.Lakini misaada hii imekuwa katika vitu vidogo ambavyo havisaidii sana kuondoa umaskini wa mtu mmoja mmoja.

Njia moja nzuri ya kuondoa umaskini ni kwa viongozi wa dini kwenda kwenye nchi hizo dini zilikotoka na kuwaambia tunaomba waumini wenu wawe wananunua bidhaa za waumini wenzenu wa tanzania.

Mfano sheikh mkuu aende uarabuni akatembelee nchi za kiislamu awaombe wawe wananunua bidhaa za waislamu wa Tanzania wanazolisha au kulima ili wawaondolee umaskini waislamu na uislamu Tanzania.

Kadinali Pengo naye atimke aende ulaya kwa wakatoliki awashawishi na kuwaomba kuwa wanunue bidhaa za wakatoliki wenzao wa tanzania ili wawaondelee umaskini na walipe nguvu kanisa katoliki la Tanzania.

Askofu mkuui wa Anglikana naye atimuke aende Uingezereza akamone huyo bishop of Cantebury amwombe awashawishi waangalikana wa uingereza wanunue bidhaa zinazozalishwa na waangilikana wenzao wa tanzania.

Maaskofu wa kibaptist na kilokole nao watimukie Marekani na huko nchi yalikotoka makanisa yao wawaombe walokole wa huko nchi makanisa yao walikotoka wanunue bidhaa wanazolisha walikole wenzao watanzania kuwasaidia badala ya kuwaletea misaada ya mitumba.

Viongozi wa Wahindu nao watimkie India wakawaombe wahindu wenzao wanunue bidhaa za wahindu wenzao wa Tanzania.

Bila kusahau wajahidina watanzania nao waende huko kwa wajahidina ulikokomaa ujahidina wawaombe wanunue bidhaa za wajahidina wenzao wa Tanzania badala ya kulta misaada ya  tende za kula mwezi wa Ramadhani.

Na dini zingine zi fanye hivyo.Hata waabudu waiombe mizimu iwe inanunua bidhaa za waabudu mizimu badala ya kusubiri kupelekewa kafara za kuku,kondoo,mbuzi na pombe.

Naamini kama viongozi wa dini wakijipanga vizuri mauzo yetu yaweza ongezeka nchi na uchovu wa ulofa wa waumini wengi kwenye dini utapungua.

Naomba kutoa hoja.

2. IGWE

IGWE JF-Expert Member

#2
Jul 26, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 7,753
Likes Received: 1,326
Trophy Points: 280
Nimeipenda sana hii,...ni kama kuna ukweli fulani hivi

3. dudus

dudus JF-Expert Member

#3
Jul 26, 2011
Joined: Feb 28, 2011
Messages: 7,780
Likes Received: 6,114
Trophy Points: 280
Sijakuelewa:-

(1) Mimi nafahamu bidhaa zinazozalishwa na watanzania; sijui za waislamu, za wahindu, au za wakristu. Kama una mifano, nitajie tafadhali.

(2) Kwa maeneo mengine sijui, ila kwa Ulaya na Marekani the trick won't work; kwanza wanabanwa na Katiba zao. Ni katiba ambazo hazimtazami mtu kidini na hata hao maaskofu wao sijui kama watakubali hoja dhaifu kiasi hicho eti za kununua bidhaa za "watu wa dini yetu".

4. RICHEST

RICHEST Member

#4
Jul 26, 2011
Joined: Jun 23, 2011
Messages: 25
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Inafanya kazi.Mfano ukiwa na kiwanda cha kusindika nyama Tanzania usahau kupeleka hizo nyama kama hazijachinjwa kiislamu( halal food).Hivyo muislamu anaweza market vizuri kuliko mfanyabiashara ambaye si muislamu.

Kuhusu Katiba hakuna katiba duniani iwe ya ulaya au marekani inayoagiza kuwa mnunuzi anunue wapi.Hiyo katiba sijaiona.Naweza nunua matunda jamatini nikitaka kila siku na hakuna wa kuniuliza wala kunifunga hivyo mtu wa ulaya au marekani akiamua kununua bidhaa kanisani tanzania au msikitini Obama hawezi mfanya lolote anatumia hela yake aliyopata kwa jsho lake na aliyoilipia kodi.

5. dudus

dudus JF-Expert Member

#5
Jul 26, 2011
Joined: Feb 28, 2011
Messages: 7,780
Likes Received: 6,114
Trophy Points: 280
Hoja ya msingi ilikuwa kuwashawishi wanunue kwa misingi kwamba bidhaa zimezalishwa na watanzania wa dini yao. Ninachokitilia mashaka mimi ni "ushawishi kwa misingi ya kidini" ambao sidhani kama hao maaskofu wa huko au akina Obama watakubali; yaani umshawishi Obama kwamba "tunaomba tuuze Marekani kwa Ukristo wetu au mje mnunue Tanzania kwa Uislamu wetu! Forget about that; hata Iran nina mashaka kama mbinu hii itafanya kazi. Otherwise hapo kwenye red ni kweli mnunuzi mmoja mmoja halazimishwi pa kununua.

6. Shedafa

Shedafa JF-Expert Member

#6
Jul 26, 2011
Joined: May 21, 2008
Messages: 802
Likes Received: 16
Trophy Points: 35
Hata hivyo hizo bidhaa za Tanzania za kuuza nje ziko wapi?. Mwishowe utasema sigara na bia.

7. RICHEST

RICHEST Member

#7
Jul 27, 2011
Joined: Jun 23, 2011
Messages: 25
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Kwa nini wasijaribu kwanza kuwaona viongozi wenzao wa dini.Waone kama watakubali au watakataa.Sisemi wakamwone OBAMA wala wala kiongozi wa kiserikali nataka watumie ushawioshi wa kidini ku-win soko.Mbona kawaida vitu hivi.Hata Mabenki yanatumia (Islamic Banking) kuuza product zao kidini.hATA MAREKANI ZIPO.

8. m

mabogaz Member

#8
Jul 28, 2011
Joined: Jul 9, 2011
Messages: 7
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

Loading...