Njia wanazotumiaga kuiba kura na jinsi ya kukabiliana nazo

Didia

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
719
258
Kuna mbinu kadhaa vyama tawala Africa, hasa CCM, hutumia kuiba kura na au kubadili matokeo ili vishinde. Zifuatazo ni baadhi na mbinu CDM inaweza kutumia kukabiliana nazo

1. Kuhonga mawakala (poll agents) na kusaini matokeo feki, pia kupoteza fomu za matokeo. [Njia hii hutumika kama mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi ni wachache]
 • Jinsi ya kutatua: CDM inashirikiane na mgombea wa chama kisicho na nguvu ilmuwekee mawakala hivyo kuwa na wakala zaidi ya mmoja kila kituo. CDM inakikishe kila wakala analipwa na anatoka na fomu ya matokeo. Fomu zikusanywe na makamanda mara tu baada ya matokeo kutanganzwa. Kila kijiji kiwe na center ya kukusanya fomu hizo. Wapiga kura waambiwe kumdhibiti wakala yeyote wa CDM atakayetoka ndani ya kituo bila fomu ya matokeo

2. Msimamizi wa uchaguzi (MKurugenzi) kuwasilisha fomu feki za matokeo ya vituo kwa majumuisho.
 • CDM iandae E-xel sheet ya matokeo ya kila kata na vituo vyake. Matokeo ya kila kituo yanaposomwa wawakilishi wa CDM wawe makini kwa kulinganisha, yakisomwa tofauti waweke objection na kutaka kuiona fomu ya matokeo, kwa vile walikuwa tayari wana support ya mgombea mwengine walinganishe fomu zao na ya msimamizi , na wakatae matokeo hayo kuwa sio fomu halali
3. Msimamizi (mkrugenzi) kutangaza matokeo tofauti ya jumla ya kura inavyo onesha
 • Kabla ya mchakato wa kuhesabu kura kuanza CDM iwe tayari ina matokeo na kujua mshindi. kama imeshinda imape taarifa wanachama wake. kundi la vijane likae nje ya ukumbi kwa utulivu huku likipenyeza maneno kwa askari, "tunajua tumeshinda kwa kura [.......]. tunasubiri atangazwe" . matokeo yakicheleshwa zogo lianza (Mz, Arusha model)
 • Kwenye chumba cha kuhesabu kura msimamizi ajulishwe matokeo mapema na kutishwa (kwa kuumwa sikio): "ukichakakachua tunakufa na familia yako popote itakapohamia
 • ...
4. Kuweka vituo hewa
 • CDM iwe na orodha ya vituo vyote iliyotolewa na msimamizi, ijue kila kata kuna vituo vingapi na idadi ya watu waliojiandikisha. ikatae kituo chochote hewa
5. WanaCCM kuingia na kura zilizo pigwa na kudumbukiza kwenye sanduku
 • Wakala wawe makini na wasikubali mtu aingie na mkoba. wahakikishe masanduku ya kudumbukiza kura kura yapo mahali wazi na yanaonekana vyema

6. Kuhamisha majina ya wapiga kura kutoka kituo/kijiji/kitongoji kimoja hadi kingine. Hii ndo njia hatari nayakutisha maana wapiga kura wengi ni rahisi kukata tamaa pale jina lake litakapo kosekana kwenye daftali katika kituo alicho jiandikisha. CCM inataraji kutumia njia hii hasa pale penye wanachama wengi wa chama pinzani.
 • Mpaka sasa sijui hili linaweza kutatuliwa kwa njia gani. Wadau naomba mchangie
Hizi tu ni baadhi ya mbinu za kuiba kura/kuharibu matokeo. Huenda zikawepo nyingine nyingi tena za kutisha zaidi. kama unafahamu mbinu yoyote inayotumiwa iweke hapa tuchangie mawazo jinsi ya kudhibiti. Hii si tu kwa uchaguzi wa Igunga bali sku za usoni pia.
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,515
11,824
kinachotakiwa watu wakisha piga kura,wasiondoke kituoni na wahakikishe kura zinahesabiwa mbele yao.kwani mbinu kubwa inayotumika huwa ni kubadilisha masanduku ya kura wakati yakipelekwa eti kituo cha kuhesabia.Pia kuhakikisha hesabu ina balance kati ya watu waliojoandikisha=waliopiga kura(jumla kura za wagombea wote walizopata+zilizoharibika)+wasiopiga kura
pili karatasi maalumu za kupigia kura toka china au south africa zinazotumiwa huwa ni kama litmus paper, ambapo ukipiga kura wino baada ya muda fulani hujifuta na kuhamia upande mwingine mbinu hii hutumiwa sana na ccm ndiyo maana tenda ya ku supply wino wa kupigia kura NEC huwa hawaitoi!!!
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Siri ipo kwenye ulinzi wa kura mpaka zitakapohesabiwa na kutangazwa mbele ya hadhara.

Tuige mtindo wa watu wa Mara kutoondoka kituoni zaidi tu ya kupiga hatua kumi nyuma. Jiulize unapoondoka kutuoni kura zako huwa unamwachia nani akulindie wakati tume, polisi na vyombo vingine vyote ni vya CCM.

Ulinzi na usalama wa kura ni haki ya msingi ya wapiga kura popote pale!!!!!!!!!!!!!!!
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,879
9,832
Kuna mbinu kadhaa vyama tawala Africa, hasa CCM, hutumia kuiba kura na au kubadili matokeo ili vishinde. Zifuatazo ni baadhi na mbinu CDM inaweza kutumia kukabiliana nazo

1. Kuhonga mawakala (poll agents) na kusaini matokeo feki, pia kupoteza fomu za matokeo. [Njia hii hutumika kama mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi ni wachache]
 • Jinsi ya kutatua: CDM inashirikiane na mgombea wa chama kisicho na nguvu ilmuwekee mawakala hivyo kuwa na wakala zaidi ya mmoja kila kituo. CDM inakikishe kila wakala analipwa na anatoka na fomu ya matokeo. Fomu zikusanywe na makamanda mara tu baada ya matokeo kutanganzwa. Kila kijiji kiwe na center ya kukusanya fomu hizo. Wapiga kura waambiwe kumdhibiti wakala yeyote wa CDM atakayetoka ndani ya kituo bila fomu ya matokeo

2. Msimamizi wa uchaguzi (MKurugenzi) kuwasilisha fomu feki za matokeo ya vituo kwa majumuisho.
 • CDM iandae E-xel sheet ya matokeo ya kila kata na vituo vyake. Matokeo ya kila kituo yanaposomwa wawakilishi wa CDM wawe makini kwa kulinganisha, yakisomwa tofauti waweke objection na kutaka kuiona fomu ya matokeo, kwa vile walikuwa tayari wana support ya mgombea mwengine walinganishe fomu zao na ya msimamizi , na wakatae matokeo hayo kuwa sio fomu halali
3. Msimamizi (mkrugenzi) kutangaza matokeo tofauti ya jumla ya kura inavyo onesha
 • Kabla ya mchakato wa kuhesabu kura kuanza CDM iwe tayari ina matokeo na kujua mshindi. kama imeshinda imape taarifa wanachama wake. kundi la vijane likae nje ya ukumbi kwa utulivu huku likipenyeza maneno kwa askari, "tunajua tumeshinda kwa kura [.......]. tunasubiri atangazwe" . matokeo yakicheleshwa zogo lianza (Mz, Arusha model)
 • Kwenye chumba cha kuhesabu kura msimamizi ajulishwe matokeo mapema na kutishwa (kwa kuumwa sikio): "ukichakakachua tunakufa na familia yako popote itakapohamia
 • ...
4. Kuweka vituo hewa
 • CDM iwe na orodha ya vituo vyote iliyotolewa na msimamizi, ijue kila kata kuna vituo vingapi na idadi ya watu waliojiandikisha. ikatae kituo chochote hewa
5. WanaCCM kuingia na kura zilizo pigwa na kudumbukiza kwenye sanduku
 • Wakala wawe makini na wasikubali mtu aingie na mkoba. wahakikishe masanduku ya kudumbukiza kura kura yapo mahali wazi na yanaonekana vyema

6. Kuhamisha majina ya wapiga kura kutoka kituo/kijiji/kitongoji kimoja hadi kingine. Hii ndo njia hatari nayakutisha maana wapiga kura wengi ni rahisi kukata tamaa pale jina lake litakapo kosekana kwenye daftali katika kituo alicho jiandikisha. CCM inataraji kutumia njia hii hasa pale penye wanachama wengi wa chama pinzani.
 • Mpaka sasa sijui hili linaweza kutatuliwa kwa njia gani. Wadau naomba mchangie
Hizi tu ni baadhi ya mbinu za kuiba kura/kuharibu matokeo. Huenda zikawepo nyingine nyingi tena za kutisha zaidi. kama unafahamu mbinu yoyote inayotumiwa iweke hapa tuchangie mawazo jinsi ya kudhibiti. Hii si tu kwa uchaguzi wa Igunga bali sku za usoni pia.

Duuh mkuu una strategies!! Ila sasa kumbuka kwamba vyama vyote visivyo na nguvu ni mateka wa CCM kwa hiyo si vya kutegemea saaaana!

Hiyo ya kupenyeza maneno na kuuma sikio si ndio mwanzo wa fujo!! Una maana hiyo strategy ndiyo iliyofanikisha CDM kunyakua majimbo ya Arusha na Mwanza. Sijui inaweza kuwa nzuri ama la. Lakini pia hujasema kama watakuwa wamejumlisha matokeo na kikuta wameshindwa iweje. Ningetegemea ungewashauri wawaambie pia makamanda wao kwamba tumeshindwa na tuondoke kwa amani.
 

ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,262
521
Sawa mkuu lakini kitu kitakachotumika hapo ni kua zile sehemu zote zenye upinzani mkali nguvu kali ya polisi itapelekwa hapo na itapita amri kuwa mtu ukishapiga kura afutike eneo la kura ama sivyo atakula maji ya kuwasha hiyo ndio itakua mbinu ya mwisho,angalia sasa sinema itakavyokua kama watakubali kuodoka ama kukataa kuondoka vyote vitakua ni faida kwa wizi wa kura,wakikubali kuondoka ina maana watawaachia nafasi nzuri ya kuloby na wale mawakala wa upinzani bila bugudha na kufanikiwa kuiba kura kama wapiga kura watagoma kuondoka pia ni faida manake itaanzishwa vurugu ya maana watu watakula mabomu ya machozi na maji ya kuwasha sasa kwa kupitia vurugu hiyo inakua rahisi kucheza mchezo mchafu faster manake kila mtu atakua anaconcetrate na kujiokoa hapohapo mchezo utachezwa.
Kwa hiyo mahali kama igunga itakua rahisi kwa chama tawala kushinda kwa sababu nguvu yote ya jeshi la polisi itapelekwa kule hivyo watasaidia sana ushindi wa chama tawala.
Mbinu nyingine ni kuwa zile sehemu zote zenye upinzani mkali kutapelekwa magari ya kusafirisha kura ambayo ni mabovu au mengine yatanyimwa mafuta ya kutosha,mbinu hii faida zake ni kuwa kama gari ikiaribika itachelewa kufikisha fomu za kupiga kura kituoni hivyo wapiga kura watasubiri watachoka wengine wataamua kuondoka hivyo kura pinzani zitakua zimepungua,upande wa pili wa shilingi wakati wa kusafirisha kura gari litaharibika nagari lingine la kufanya replace litachelewa kufika mbinu hii inasaidia sana kwa sababu wakati wa matengenezo ya gari inaweza kuchukua hata siku nzima hivyo italeta upenyo mzuri wa kuchakachua.
Mbinu ingine ambayo inafanyikaga ni mabalozi wotekuzunguka nyumba hadi nyumba kuandikisha watu na maswali ambayo wanaulizwa ni jina,namba ya kitambulisho cha kura na chama hii mbinu inasaidia sana huaga inafanyika mapema kabisa kabla ya hata kutangazwa uchaguzi,sasa basi inatumika hivii,kwa kua namba za vitambulisho vya kura vya watu wa vyama pinzani zimeshapatikana kitu kitakachotokea majina yao yote hayataonekana siku ya kupiga kura.
Nawasilisha.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
WATANZANIA TUJIONDOLEE ADHA ZA UCHAKACHUAJI KWENYE CHAGUZI ZETU KWANZA KWA KUANGAMIZA 'UJIMA' WETU WA KIMAWASILIANO NA KULINDA MAZINGIRA MAPYA TUYATAMANIYO KISHERIA

1. Wakala asikubali kupewa chakula, kinywaji wala msaada wowote ule na timu pinzani Watumewahi kulishwa madawa ya kulevya, kunyunyuziwa chlorofoam ili walale usingizi wa pono huku madudu yakifanyika.

2. Iwe ni jukumu la chama kulisha mawakala pale pale kituoni na wala si kwenda kutafuta chakula kwingineko.

3. Idadi ya mawaka isipungue wanne katika kila kituo. Na idadi hiyo iwe ikishika zamu kwa kuzingatia ratiba maalum inayopangwa na mkurugenzi wa uchaguzi wa chama na kupishana zamu kimaandishi mbele ya Kamanda Msimamizi wa chama katika ngazi ya kata.

4. Mawasiliano yaboreshwe zaidi na kutumika Satelite phones, kompyuta za mapajani zenye kutumia internet services zenye uwezo wa kutiririsha kila taarifa papo kwa hapo (ziwe zimewekewa zile programmes za kisasa zenye kuruhusu tu kuongea tu na maneno kubadilika maandishi) na radio calls za chama zenye kuruhusu minute-to-minute communication tangu ngazi ya kitongoji hadi makao makuu bila mawasiliano hayo kuingiliwa.

5. Haki ya raia kulinda kura zao kwa kuzingatia taratibu zilizowazi ihimizwe kisheria tangu sasa.

6. Kwa kuwa uchaguzi wa mwaka jana uliibwa katika ngazi ya kujumlisha kwenye kompyuta, fundisho hilo lituelekeze kudai haki ya vyama shiri vyote kuwa na ushiriki wa taarifa zote live kadiri zinavyoendelea kwenye tume ndivyo na wafwatiliaji kwenye makao makuu ya vyama husika wanavyoona.

Hili linawezekana kabisa sawa tu na taarifa za soko la fedha NASDAQ zinavyotiririshwa kutoka chanzo kimoja na washiri wote wa kwenye shughuli za soko hilo hufwatilia live kutoka majumbani mwao, barabarani na kadhalika.

Huo ndio msingi wa uwazi kwa kutumia teknolojia za kisasa kwenye uchaguzi - Tume ya Uchaguzi ya Taifa ibakie tu kwenye shughuli ya kuratibu mambo na wala SI KUHODHI TAARIFA AMBAZO KIMSINGI NI MALI YA WAPIGA KURA NA mali ya vyama shiriki.

Huo umangimeza wa Jaji Makame mpaka kujichagulia achakachue au la ni lazima tukaudhibiti kwa njia hii.

Yeyote anayeingiza taarifa zozote katika mfumo kama huo ni sharti

i. atambulike kisheria na kuweza kuwajibishwa kunapohitajika,

ii. alazimike kuingiza taarifa husika hadi mara tatu ili kusitokee madai ya kukosea kibahati mbaya,

iii. Kila mtu awe na uwezo wa kuona taarifa zote zinazohusiana na uchaguzi ila ngazi zitofautiane kwenye nani anaweza kubadilisha taarifa fulani kwenye system na mpaka akafanye hivyo ni sharti passwords wa wawakilishi wa vyama shiriki viwe vimesainishwa kila mtu kwa nafasi yake.

Computer expert wetu wanaweza kutengeneza kabisa programme kama hii ninayozungumza kama wazo haya.

iv. kwa njia hii Observers nao wanakua na nafasi zao humu.

NB: Siku zote CCM hutumia ujima wetu wa kimawasiliano kufanya madudu, let;s turn around the ballgame kwa faida ya wananchi walio wengi na wala si kwa ajili ya genge fulani tu.

Tundu Lissu tunahitaji mswada kuboresha sheria na taratibu za uchaguzi. Pia sheria itamke wazi kura kutunzwa na wapiga kura wenyewe mbele ya hadhara bila kufukuzwa mtu kituoni, muda gani matokea yatangazwe tangu mtu wa mwisho kutumbukiza kura yake, mambo gani yazingatiwe kikamilifu kwanza ndipo matokeo yatangazwe, nafasi na ushiriki wa vyombo vya habari katika kila hatua ya uchaguzi kuhakikisha HAKI NA UWAZI wakati wote.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Kama ni kura ndio silaha ya demokrasia kupatika kwa viongozi wa ngazi mbali katika basi hatuna kuelekeza nguvu zetu kufanya sheria na taratibu zote kuwa (1) Wazi zaidi, (2) Salama zaidi, (3) waa Haraka na wigo Mpana zaidi, (4) Shirikishi zaidi na (5) yenye kulindwa zaidi na sheria.
 

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,959
3,291
DIDIA,

Kumbe ndo maana jana majira ya saa 10:30 jioni raisi mstaafu, Benjamin William Mkapa, alipotua kwenye "air strip" ya mgodi wa Resolute alitamba ya kuwa "...anaenda Igunga kumaliza mechi...." Ama kweli sasa naamini bila ya uchakachuzi hakuna uchaguzi hawa jamaa (magamba) watashinda.

Kwavile kesho atatumia uwanja uleule wa Resolute ili kuruka na kurudi Dar, basi ntamuomba jamaa yangu amuulize (iwapo watashindwa). Je, kulikoni Mkuu mbona imekuwa kinyume huko Igunga?

Mkuu DIDIA weka na hizo zingine!!!!
 

samito

JF-Expert Member
May 16, 2011
631
175
big up DIDIA, umeeleza vema, hasa hilo la kumtisha mkurugenz mtangaza matokeo ni la msing mana hao ndio chanzo cha upotoshaji, nataman ningekuwa igunga nikafanikishe
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,940
Duuh mkuu una strategies!! Ila sasa kumbuka kwamba vyama vyote visivyo na nguvu ni mateka wa CCM kwa hiyo si vya kutegemea saaaana!

Hiyo ya kupenyeza maneno na kuuma sikio si ndio mwanzo wa fujo!! Una maana hiyo strategy ndiyo iliyofanikisha CDM kunyakua majimbo ya Arusha na Mwanza. Sijui inaweza kuwa nzuri ama la. Lakini pia hujasema kama watakuwa wamejumlisha matokeo na kikuta wameshindwa iweje. Ningetegemea ungewashauri wawaambie pia makamanda wao kwamba tumeshindwa na tuondoke kwa amani.

Hapa zinazungumziwa mbinu za uchakachuaji na namna ya kudhibiti huo uchakachuaji.

Suala la kukubali matokeo ya kushindwa kihalali halihitaji maandalizi kama unavyodhani ingawa kupitia utaratibu huo wa kudhibiti uchakachuaji kama wakishindwa watajua mapema tu.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Enyi MODS,

Sera, miongozo na taratibu za JK ziko wazi lakini mara nyingi mnaonekana kutokuzifuata ni kwa nini hasa??

Kwa mfano, kama huu uzi wala si uzi wa masuala ya siasa kiasi cha bkuondolewa kwenye ukurasa ule basi tuwekeeni wazi hapa jukwaani vigezo vipya mnavyotumia kuamua juu ya hilo na vigezo hivo vimetoka kwaa nani hasa??????? Inakera hivi.

Sisi ni wanachama na wamiliki wa miundombinu hii ya JF, Wliiam Malecela unanipata uzuri hapa, hatutaki kuhangaishwa wala kuonekana kama kwamba sisi ni wanachama BY INVITATION.

Tafadhali
MOD wa zamu jieleze kwetu kuhusu jinsi unavyotuhangaisha humu na THREADS mbalimbali - unafanya hivyo kwa manufaa ya nani wakati sisi wanachama wenyewe hatufurahishwi???????????
 

zamlock

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
3,841
650
wajemeni nimewai kukaa mahali nikasikia jinsi ccm walivyoiba kura kwenye uchaguzi mmoja wapo ambao ulishawai kufanywa hapo nyuma hakika nilichoka walitumia watu wa funguo za bandia kufungua chumba ambacho kilikuwa kimehifadhiwa kura na kilichofanyika ni kutoa baadhi ya masanduku na kuweka yale yaliyokuwa na kura za mgombea wa ccm hakika nilichoka sana na pia nashauri igunga chadema wawe makini na hii njia ccm wanaitumia sana
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
225
Wandugu wapenzi, hebu someni makala hii iliyotoka leo katika gazeti la The African on Saturday. Hawa NEC kweli ni wakorofi.
Igunga: NEC's fake Voters' Register will produce fake results

BY HILAL K. SUED

If they are to be raised from their graves, ancient Athenians would be infuriated to discover that the result of their efforts in ensuring mankind are governed justly, by elected representatives of their own choice had come to naught.

Indeed, how could they have known that what they concocted eons ago was set to tease mankind forever with the striking contrast between its ideals and its realities, between its heroic possibilities and its sorry achievements?

As our political leaders conduct political business, let us never forget that government means ourselves and not an alien power over us, as that ended half a century ago. The ultimate rulers of our democracy – if it is one at all – are not the President, MPs and government officials, but the voters of this country.

That, of course is what it ought to be – voters ruling over themselves, even though the correlation is always doused in deceit and hypocrisy. And the unlikelier place from where this happened is none other than the land that claims to be the world's greatest democracy – the US.

For it did not settle comfortably in George W. Bush – former US President' mind – when in 2003 he said he did not need approval from the UN to wage a war. If that's so it very well meant that he didn't need the approval of the American voters to become president, either. He only needed the 5-4 split decision of the Supreme Court to become one.

Let's leave GWB alone and concentrate on our own turf – our own version of democracy and the participation of the electorate – those listed in the NEC's so called Permanent Voters Register (PVR).

In fact there are more goings-on – or not going on – around and within that "permanent" register than what meets the eye. It appears the CCM government had caught opposition parties on wrong footing – or according to the popular Kiswahili slang – it struck them with a back heel goal (walipigwa bao la kisigino).

I will explain: When, before the 2005 elections opposition leaders shouted their heads off to have in place a Permanent Voters Register (PVR) it never dwelt upon their minds that they were in effect calling for "permanent theft register (PTR)." Now they do.

A permanent voter's register is nothing but a thieving concoction if its status remains permanent – that is without its being updatied – without incorporating new voters who every day attain the age of 18, and remove those deceased.

It's a continual process which the National Electoral Commission (NEC) has to undertake if it wants to brag of competence. That it doesn't. Even though they are not saying it, but it's to do with logistics, the money and manpower – all of which it has to plead for from the CCM government – itself a serious candidate in the country's electoral process.

For example, does "permanent" mean just that – permanent? It should, according to NEC, because on several occasions – Tunduru, Kiteto and Biharamulo – it conducted by-elections without updating its register that was compiled in 2005.

In the case of Tunduru a court case that was filed against NEC for doing so and which petitioned for the election to be stopped was dismissed on the first stages – it did not test the appeals court's opinion. And that was because the ruling came on a Friday with elections the following Sunday and therefore there was no time for preparations for appeal.

So it's the same old story for this weekend by-election in Igunga. Thousands of eligible voters will not take part in the by-election because the National Electoral Commission (NEC) has not updated the voters register. The register was last updated last year – months before the General elections.

Last week, in a briefing to reporters, the chairperson of Tanzania Civil Society Consortium on Election Observation (TACCEO) Martina Kabisama said failure to update the voters register will deny some Igunga residents their democratic right to elect their legislator.

So this means that the statistics for voters registered for last year's general election will be used in the Sunday by-election. It will be a fake voters' roll because it will list names of people who are deceased, and will miss out names of people who have attained the age of 18 in the last 12 months.

The roll will also carry the names of many eligible voters who will not vote for the reason that they lost their registration cards and were not availed the opportunity by NEC to be issued with replacements. So there will be no change on the number of voters or the number of polling stations – it's as if Igunga is still as it was twelve months ago. It's going to be a wonderful by-election whose results will therefore be fake results.

What is even more worse the election law is not clear on when the voters register should be updated as it only says "when it is seen necessary." So NEC did not see it necessary to update the Igunga Voters register, it does not matter to the electoral body to deny thousands of Tanzania eligible voters their democratic right under the Constitution.

There is a general acceptance, easily explained, that a huge voters turnout at elections does not sit well with the ruling party, whether at general elections or by elections. The percentage population of the country's fairly educated youth who are eligible voters (that is those between the age of 18 and 35) is estimated to be over 70%. Most of these, thrown into the streets from primary and secondary schools every year are futureless, except for one profession: street trading (umachinga).

So the less of these vote, the better for the ruling establishment. Last year's General elections had a worse voters' turnout in the country's post multiparty history – at 42 percent or 8 million of the 20 million plus registered voters according to NEC. It's believed of the 12 million who did not vote, 8 million were youths.

There were widespread reports of voters who did not see their names in the voters' rolls pasted only six days or so before voting day – very short a time to do anything, especially in the absence of clear-cut procedures from NEC on what to do.

Personally I went around various polling centres in Dar to view the list of names pinned up, which also listed the year of birth of each voter. I discovered that the nearest year of birth for many voters was 1988. Very few indeed were listed as having been born in 1989 or later (that is before 1992). That meant many of the 18-21 age group were missing. The reason could be that they were purposely deleted or, as many found out later, were posted at other polling stations.

In the by-elections of Mbeya rural and Busanda in 2009, the number of voters who turned up at polling stations did not even reach half the total number of the electorate registered in the respective constituency's voter registers.

More than 130,000 voters were registered in the NEC register in Busanda in the weeks running up to the by-election, but only about 55,000 voted.

In the Mbeya rural by-election in January 2009, only 44,855 of the 127,780 voters registered - or roughly 34 percent of registered voters - showed up at the polls.

And Busanda was the first time since plural democracy was ushered in the country when opposition leaders were awakened from their slumbers and questioned the habit whereby local functionaries of the ruling party conduct what is clearly an illegal exercise – that of registering voters.

The practice resurfaced in Igunga – one CCM Ten-Cell leader was last week caught conducting house to house visit in his area to register what he was convinced to be people who would vote for the party's candidate. He was doing this not by demanding/requesting the production of CCM membership cards which he was entitled to do -- but their voter's registration cards.

The reasons why these local CCM functionaries cannot get the details of their members from registers held by local party branches beats me – but could be because there are no such registers. These days strict card-paying membership hardly exists and this is true for both the ruling party and the opposition. There are only followers and/or supporters.

Voters' cards are a property of NEC, and by extension, the government, hence no party should have anything to do with them. I am not very certain whether or not collecting details of voters' cards by unauthorized people (i.e. non-NEC officials) is legal under the NEC or other laws.

Even if it is not illegal, it has elements of dishonesty, if not crookedness, as it amounts to discreet bullying and intimidation. It also provides avenue of outright illegal acts, hence giving credence to claims of card buying. All in all the perpetrators take advantage of the gullible and largely idiosyncratic rural population.
 

tzjamani

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
995
30
THermos ya chai yenye kura
Hoptop ya chakula yenye kura
Tricks za kuwazubaisha mawakala kwa utani au njia yeyote wakati wa kuhesabu ili kura feki ziwekwe
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,771
74,420
Wana jamvi ni vyema tukielimishana ni njia zipi wanazotumiaga kuiba kura na kujipatia ushindi?

Kima mdogo, jitahidi kila unapoandika ukumbuke kuto-ziweka hizo "ga" kwenye neno. Utaeleweka vizuri tu bila hizo "ga", unatuharibia lugha yetu tamu, umesikia Kima?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom