Njia tofauti za kupata mtaji wa biashara

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Naomba leo tuzungumze namna tofauti Za kupata mtaji kwakuwa kuna changamoto Sana kwa Wau wengi wanaotaka kufanya biashara kupata fedha Za kuanzia. Napenda tuangalie namna na mbinu unazoweza kuzitumia kufikia malengo yako Ya biashara

Mbinu ya Kwanza naweza kuelezea ni ni kuhifadhi pesa hii ni hasa kwa wale ambayo wanachanzo kingine cha kukuingizia kipata unachotakiwa hapa ni kuweka malengo je unahitaji kiasi gani kukusanya na kwa muda gani pia. Yaaani kwa wiki Au mwezi unataka ujiwekee akiba kiasi gani na mwisho kufika malengo yako

Namna ingine ni kuongeza kipato kwa kutumia ujuzi wako skill money exchange mfano Fundi cherehani nk. Katika njia hii unaamua kutumia ujuzi wako ili ulipwe pesa unazohitaji kwa ajili kuanza kitu unachokusudia mfano wakina mama unajua kusuka ukitoka kazini unaweza pata zuada Ya kipato. Hii njia itakuingizia kipato utachoanza kukitunza kama mtaji wako

Njia ingine ni kukopa

Hii ni njia ya mwisho baada hizo zingine hii iwe mwisho kabisa baada zile zingine kukosekana na eneo la kwanza kabisa la kukopa ni kwa familia na marafiki hapa ni eneo zuri kwakuwa apatakuwa na riba ni uaminifu wako ndio utakao kuwa unaitajika tu umeishi vipi na Watu Au kwenda vyama vyakijamii yaaani vicoba na sacos ambazo lazima uwe mwanachama Kwanza napo unapata kiwango chá mkopo kadri unavyochangia Sasa hapa ilo kufanikisha lengo lako inabidi uchange kutoka na malengo yako katika mtaji wa biashara unayotaka kuja kufanya

Asanteni kwa leo naishia hapo mnaweza kushare kama imekupendeza ishi kwa malengo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom