Njia sahihi ya kutimiza ndoto

smartdunia

Member
Jul 29, 2021
12
9
Imeandikwa Na Smartdunia.

Nasikitika kusema,huu ni ukweli unaoumiza, lakini wenye uwezo wa kukubadilisha kabisa.

Hebu tuanze na kauli hizi tulizozizoea Kisha tujue madhaifu na mazuri yake yote.

"Tafuta pesa ili watoto wako wasikae kwenye vijiwe kubishana kuhusu Diamond na Harmonize"

"Tafuta pesa ili ukienda ukweni, usipewe kazi ya kupasua kuni na Mama mkwe wako"

"Tafuta pesa ili jumapili isiwe siku ya kufua,badala yake iwe siku ya outing"

"Tafuta pesa ili mkeo asikuambie nipishe nivae"

Hizi ni kauli chache ambazo zinashika kasi mno katika kizazi hiki cha what's up status,lakini cha ajabu na cha kusikitisha huenda hata aliyeanzisha kauli hii,alifanya hivyo kwa ajili ya kufurahisha umati tu,huku hata yeye akijiunga na kundi la watu wengi ambao hawajachukua hatua kuelekea kutimiza ndoto zao za mafanikio.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kua asilimia zaidi ya tisini ya watu ambao hawajafanikiwa, wana ndoto za mafanikio,lakini ni asilimia kumi tu ya watu hao ambao wanaonesha dalili za kusogea kuelekea ndoto hiyo.

Kuna mzazi mmoja, aliwahi kuwauliza watoto wake swali kwamba, kama ufaulu wa darasani sio kipimo sahihi cha akili, je kipimo sahihi cha akili ni kipi?

baada ya kimya cha dakika moja, mmoja akajibu.

"Pesa nyingi mzee, ndio kipimo sahihi".

Mzee akatikisa kichwa kwa masikitiko na kumuuliza Tena.

"Ina maana Mimi baba yenu nisiyekua na pesa za kutosha na ninayewasomesha kwa shida sina akili?".

Wote wakabaki wakiangaliana,Kisha mmoja akadakia.

"Hapana mzee hajamaanisha hivyo, kwani kipimo sahihi ni kipi?".

"Ni usahihi wa mbinu unazotumia kila siku kupiga hatua kuelekea ndoto zako", mzee akamaliza utata kwa staili hiyo.

Hivyo basi,kama una ndoto kubwa ya maisha yako, jiulize

"Leo nimechukua hatua gani ambayo ni hatua ya uhakika kuelekea kwenye hiyo ndoto yangu?".

Kama jibu ni.

"Bado nasubiri mambo yaende sawa" au

Umefanya kitu kingine ambacho hakiendani na ndoto zako,basi ujue Bado una safari ndefu.

Unachopaswa kujua ni kwamba,haijalishi umepiga robo hatua,nusu hatua,robo tatu au hatua nzima,cha msingi upo kwenye uelekeo wa ndoto yako na haijalishi safari yako ni ndefu kiasi gani,ukiweza kupiga hatua ndogo kila siku,basi jipongeze sana kwa sababu ipo siku utafurahia matunda yake kwani hicho ndicho kipimo sahihi cha akili.

Kumbuka hata kuuliza undani wa kile unachokiota maishani ni hatua, kwani hapo tayari umeshaanza utekelezaji.

Unaweza ukawa mmoja wa wanaoumiza kichwa sana na kushindwa kujua ni wapi pa kuanzia,kumbe hilo ni swala dogo sana,na jibu lake ni kwamba,unaweza kuanzia hapo hapo ulipo wala hakuna sehemu nyingine ya kuanzia.

Unachotakiwa kukiepuka ni uoga wa kufeli,kutokuogopa mwanzo mgumu na wenye kukatisha tamaa,kutojali maneno ya marafiki au watu wa karibu kama ndugu wenye mtazamo wa tofauti na kile unachokiamini, kujihusisha na marafiki sahihi ni jambo la msingi mno,amini siku zote njia ya mafanikio ni ngumu hivyo kukata tamaa ni mwanzo ya kupunguza idadi ya watu waliopangiwa kuyafikia mafanikio yoyote.

Kuna msemo wa waswahili usemao,

"Tumia kidogo ulichonacho kupata kikubwa ambacho huna".

Ni dhahiri kwamba huwezi kutumia kitu ambacho huna kupata kitu ambacho huna,na unapozidi kusubiri kesho hakikisha unajua kwamba kesho ni siku ambayo haijawahi kufikiwa tangu dunia ianze.

Zaidi ya yote unatakiwa kujua kua,hakuna aliyeumbiwa mafanikio wala kufeli, juhudi zako ndizo huamua kundi gani kati ya hayo mawili ni kundi lako sahihi, tajiri na masikini wanatofauti kubwa mno, lakini tajiri na masikini asiyekata tamaa tofauti yao ni ndogo mno, yaani ni muda tu waliopangiwa kufanikiwa, na hii ndio sababu masikini na masikini asiyekata tamaa wana tofauti kubwa kuliko vile unavyodhani.

Mwisho nipende kukujuza ndugu msomaji kwamba,watu waliofanikiwa husema, muda mzuri wa kupanda miti ni miaka kumi iliyopita na muda mwingine mzuri ni sasa, hivyo hujachelewa kuifuata ndoto yako isipokua usipoanza leo.

Nikutakie maisha mema na yenye mafanikio.

images%20(3).jpg
 
Back
Top Bottom