Njia rahisi za kupeleka hela katika mifuko ya Watanzania wote

SOPINTO

Member
Oct 19, 2020
61
150
Kwa kipindi cha miaka mitano asilimia kubwa ya watanzania katika ngazi mbalimbali yaani kuanzia ngazi ya wafanyakazi wa sekta binafsi , wamiliki wa sekta binafsi, wafanyabiashara, watumishi wa umma, wajasiriamali mpaka wanafunzi wa vyuo vya Juu makundi yote haya ilikuwa kila kukicha kauli kubwa ni hali mbaya ya kiuchumi, lakini kwa wakati huohuo wakati wananchi wanalalamika juu ya hali mbaya lakini kwa upande wa serikali mambo safi yaani inachanja mbuga ujenzi wa madaraja, ununuzi wa ndege, ujenzi wa njia za kisasa za reli ya mwendokasi, ujenzi wa viwanja vya ndege bila kujali nini kinaendelea kwa raia wake.

Mapema tu baada ya kukatika kwa serikali ya awamu ya tano na kuingia awamu ya sita , Rais wa awamu ya sita katika hotuba zake akatoa kauli mbalimbali za kutia moyo wananchi hususani kwa swala zima la kiuchumi na wananchi kwa ujumla wao wamefarijika japokuwa bado mambo hayajaanza.

Sasa tukiwa tunasubiri mambo yaanze tutambue kuwa kila upande unajukumu lake kwa mfano kwa upande wa mwananchi huyu Mtanzania ni lazima kila mmoja afanye kazi kwa kuzingati mambo mbalimbali mfano kufanyakazi kwa bidiii, maarifa, juhudi bila kukata tamaa, ubunifu na weledi na kulipa kodi stahiki ikiwa pamoja na kutunza chochote unachopigania tusitegemee hela zitakuja mfukoni huku unaangalia Tv nyumbani.

Pili kwa upande wa Serikali ni vyema sasa ikapunguza kodi zisizo na ulazima , mfano kodi kwa wafanyabiashara ziangaliwe upya , kodi kwa mtumishi wa umma ziangaliwe upya hususani kodi ya TIN iliyoanzishwa na awamu ya tano, jambo lingine ni kuongeza miashara kwa watumishi wa umma tumbuke hawa watumishi wamefunga mikanda miaka mitano bila kupandishwa mshahara wakati mfumo wa maisha umeendelea kubadilika siku hadi siku.

Watumishi wa umma ni njia nzuri sana ya kupeleka pesa kwa wananchi ukitakakujua fanya utafiti mdogo ifikapo mwisho wa mwezi au mtumishi akipata mshahara hali inavyokuwa, pia serikali sasa ikakaribisha wawekeza bila masharti ya kuvunja moyo tuachane na zile kasumba za kusema mabeberu hizi ni fikra za wivu na umasikini zilizoambatana na ushamba wa maisha yaani lack of life exposure .

Aksanteni .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom