Njia rahisi ya kutumia simu au laptop kujiajiri kwa wanachuo na kuajiri wengine

Jul 14, 2021
5
13
MBINU ZA KUJIAJILI KWA WANACHUO NA KUAJILI WENGINE

Njia Bora na rahisi kwa VIJANA waliokosa ajira na wamemaliza vyuo vikuu au vyuo vya Kati KUJIAJILI

Nchini Tanzania ajira imekua changamoto kubwa Sana kwa vijana wengi na wengine kujikuta wameingia katika makundi ya kihuni na kupoteza malengo yao lakini kuna njia tofauti tofauti za kujiajiri kwa mtaji mdogo au hata PASIPO mtaji kabisa kinachotakiwa ni akili na ubunifu tu ili uweze kujitofautisha na wengine

Nchi zilizoendelea zimeweza kupambana na suala la ajila kwa vijana kwa kutumia technolia pamoja na kuwahamasisha vijana kutumia technolojia Kujiajili na kuajili wengine

1.NJIA YA KWANZA NI KUTENGEZA BLOG

vijana ambao wamesoma elimu ya juu Kama shahada na sitashahada au vyuo vya kawaida wanaweza Kujiajili kwa KUTENGEZA blog yaaani mtandao wa kuchapisha maudhui Kama vile habari za michezo,siasa,uchumi au masuala ya technolojia na urembo

a) Kupitia blog unaweza kupata matangazo kutoka Google na ukaanza kulipwa na Google kupitia mfumo wao wa Google AdSense pale unapo chapisha matangazo yao kwenye tovuti yako na watu wakaangalia hayo matangazo au kuwatembelea watangazaji hivyo utatengeneza kipato kupitia mfumo wa matangazo wa Google

b) unaweza kupata ubalozi wa makampuni Kama vile vodacom,betx,biko na kadharika na ukachapisha matangazo yao na wakakulipa kiasi Cha fedha kutoka na makubaliano yenu na ukubwa wa tovuti yako hivyo ukajipatia fedha
Mfano djmwanga.com anatengeneza kiasi kizuri Cha fedha kutoka kwa watangazaji wa matangazo Kama vile bikosport lakini pia millardayo.com pia anajitengezea kiasi Cha fedha kutoka kwa watangazaji
Kumbuka kuwa hakuna kitu chepesi kila kitu kinaugumu wake hata hii kazi inaugumu wake hivyo mkiwa kama team mtaweza kugawana majukimu na kufanya kazi nzuri ya kukusanya maudhui ya kuchapisha kijana usikae bila kazi

2.NJIA YA PILI NI KUFUNGUA TELEVISHENI YA MTANDAONI( YOUTUBE CHANNEL)

unaweza kutumia simu yako KUFUNGUA TELEVISHENI ya MTANDAONI yaani youtube channel na ukajiajili na kuajili wengine ni rahisi Sanaa Wala haihitaji utaalam au vifaa vikubwa kinachohitajika ni simu yako au laptop na ubunifu unapofungua kituo chako Cha mtandaoni unatakiwa kuwa mbunifu kwa kuandaa maudhui yatakayo vutia watazamaji na kufanya waendelee kufuatilia kituo chako
Mfano unaweza kupakia maudhui ya urembo au kutoa elimu MBALIMBALI kwa wafuatiliaji wako
Unawezaje kupata faida? Ukiwa na TELEVISHENI yako ya mtandaoni na ukafikisha vigezo Google wataanza kukulipa kupitia mfumo wao wa matangazo wa Google AdSense hivyo matangazo ya Google yatakua yakionekana kabla ya video yako kuanza kucheza na wafuatiliaji wako wakiangalia unalipwa
Pia unaweza kulipwa na wafanya biashara au kampuni ambazo zinapenda kutangaza bidhaa au huduma zao kupitia kituo chako hivyo watakulipa kiasi ambacho mtakua mmekubaliana

Kila hatua ya kazi inachangamoto zake lakini unapofanya kitu kwa moyo na kujituma unaweza kubadirisha maisha yako na ya wengine wewe Kama kijana usikubali kukaa bila kazi pambana ili ujiajiri na uajiri wengine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom