Njia rahisi ya kupunguza ufisadi hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia rahisi ya kupunguza ufisadi hii hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  • Ufisadi - tatizo sugu na hatari linalodidimiza maendeleo ya Afrika kumbe linaweza kupunguzwa kwa kutumia njia rahisi tu. Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia unaonyesha kwamba serikali zenye wanawake wengi madarakani (mf. Wabunge, Mawaziri) zina viwango vidogo vya ufisadi ukilinganisha na zile zilizosheheni wanaume. Rwanda - nchi ambayo inaongoza duniani kwa kuwa na wanawake wengi bungeni na serikalini inatajwa sana kuwa mfano wa kuvutia kuhusu suala hili. Ni kwa sababu hii kujitokeza kwa wanawake wengi kugombea ubunge na uwakilishi kule Haitikatika uchaguzi wa mwaka huu kumeleta matumaini makubwa kwamba pengine ufisadi utapungua.

  • Tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba wanawake wana huruma kuliko wanaume, wana moyo wa kujinyima, wanaaminika zaidi na ni wepesi wa kuona na kukiri makosana hatimaye kuomba msamaha. Pengine ni kutokana na sababu hizi wanawake pia wana uwezekano mdogo wa kuiba mamilioni ya pesa za umma na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka (wengi wao wanawake wenzao; na watoto).

  • Serikali zenye wanawake wengi madarakani pia zina uwezekano mkubwa zaidi wa kuendeleza sera imara zenye kumakinikia sekta za afya na elimu ya watoto, usawa kwa wanajamii wote na kuendeleza uchumi imara.
  [​IMG]

  • Pengine nasi inabidi tuige mfano wa Rwanda ili tuone kama visa vya ufisadi vitapungua. Utafiti huu wa Benki ya Dunia unapatikana hapa.
   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mzizi sijui kama hii itakuwa kweli kwa Tanzania. Sote tunajua jinsi wanawake wa hapa bongo kama kina Blandinda Nyoni, Mongela, Maria Kijo walivotuingiza kingi bila kutarajia. Sasa hv ufisadi upo kwa jinsia zote labda tukodishe wanawake toka Rwanda na sio kuwaamini hawa wakibongo!.
   
 3. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sawa, lakini wanapesa za kununua wapiga kura?
   
 4. R

  RMA JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja hiyo ya wanawake kuwa wengi serikalini haina ukweli hata kidogo! Hizi ni propaganda nyingine za CCM kutaka kuwahadaa wananchi kwamba ni zamu ya wanawake ili waendelee kuficha uozo chini ya mwavuli wa wanawake. Spika wa bunge mkasema ni zamu ya wanawake, na hivi amewasaidia kweli kuwahifadhi mafisadi. Kwa vile mlifanikiwa kuficha uozo kwenye kiti cha spika, sasa mnataka muendeleze uozo huo kwenye kiti cha rais! Watanzania bado tuna safari ndefu!!

   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mkuu thread haihusiani na chama ha CCM kama unavyodai wewe hebu soma kichwa cha habari ya Thread hii nakuwekea hapa chini (Njia rahisi ya kupunguza ufisadi hii hapa.) Usilete chuki zako hapa tuzungumzie Ufisadi unaofanywa na Viongozi Wanaume ukilinganisha na viongozi wa kike ni tofauti kabisa karibu viongozi wengi

  waliopo kwenye dunia hii ni wanaume wengi ndio wasiokuwa na huruma na Walala hoi ukitofautisha na viongozi wa kike waliopo katika dunia yetu ni waliokuwa na huruma juu ya walala hoi haswa katika bara letu hili la

  Afrika. Wanawake tumewaweka kama ni akina mama wa nyumbani sisi Waafrika wake zetu tumewaweka nyuma kimaendeleo ukitofautisha na nchi zilizoendelea wanawake na wanaume ni kitu kimoja, na

  wanafanya kazi pamoja utakuta nchi za ulaya wanawake wanafanya kazi kama wanavyofanya kazi wanaume. Sisi Waafrika bado tupo nyuma kabisa kimaendeleo tunamchukulia Mwanamke kuwa ni mama wa

  nyumbani akupikie akufulie nguo na akustareheshe kama mke wako tu. Katika kazi za Maendeleo ya nchi hatumuweki mbele Mwanamke ila tunamuweka mwanamke nyuma je tujiulize tukifanya hivyo Je tutaendelea kweli kiuchumi na kimaisha yetu ya baadae? Future Life itakuwepo wapi?
   
 6. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  China, Marekani, Malaysia n.k zimeendelea kwa ajili ya wanawake?. Kamwe sikubaliani na idea yoyote ile kutoka Bretton Woods institutions, kuna ajenda ya siri hapa. Wanataka kuzisoften serikali za nchi zinazoendelea. Kwa taarifa yako Rwanda inaongozwa na mkono wa chuma wa Kagame. Hizo zote zingine ni politic tu
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Wanawake wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu tukiongozwa nao? Tuwaache Mafisadi wa kiume kulididimiza kimaendeleo Taifa letu hili changa?
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mkuu umewataja hao Viongozi wa kike wanaofika 4 kama sikosei nanukuu (Blandinda Nyoni, Mongela, Maria Kijo) Nakuuliza swali moja Tangu tupate

  Uhuru nchi yetu inafika miaka 50 Je kuna Viongozi wangapi Wa kiume walio mafisadi? Tena mpaka sasa wapo Serikalini wanatuongoza na kuididimiza nchi yetu hii na kuwaumiza Walala hoi ? Hao Viongozi kike wa 4 unawafafananisha na viongozi wa Serikali wa kiume walio wengi kwenye Madaraka, wapo wangapi

  Wanaume walio mafisadi wa nchi hii yetu ? Tangu tupate Uhuru toka kwa Waingereza tuna Viongozi wangapi wa kiume Mafisadi? naomba jibu toka kwako?
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kwani kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa wananchi mpaka utoe Rushwa?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Dawa ya kwanza ni kuiondoa CCM madarakani na kukifanya chama cha upinzani.
  Dawa ya pili ni kuimarisha nguvu ya bunge na kuhakikisha CCM haina nguvu tena.
  Dawa ya tatu ni kubadili sheria nyingi za kikoloni, za kijamaa na zile za mlengo wa chama kimoja.
  Dawa ya nne ni kuimarisha shule zakata ziwe za kiwango cha A Level ili Watanzania wote wasome na hivyo kuwa na kundi kubwa la wanawake wenye uwezo wa kuongoza katika kila ngazi.

  Janga lililopo limeletwa na sera Mfu za wafu wa CCM si uwingi wa wanaume katika uongozi.
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Sawa Mkuu nakuunga Mkono. Je Wa Tanganyika Mtaweza kuiondowa CI CI CI CI CI M? katika Uongozi?
  JE CHURA ATAWEZA KUMLA NYOKA?


  [​IMG]

  [​IMG]

  Wanafunzi wa darasa la Nne wa Shule ya Msingi Muhogwe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora wakiwa na mwalimu wao akifundisha huku wanafunzi hao wakiwa wanaandika wakiwa wamekaa chini. Shule hiyo inaupungufu wa madawati 70.


  [​IMG]
   
 13. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Mzizi mkavu, sijasema kuwa wanawake watarudisha nyuma maendeleo hilo unasema wewe. Pia vilevile pamoja na huruma waliyonayo wanawake kama ulivyosema, wanawake pia ni waoga. Naomba hapa dada zangu watanisamehe sio kuwa niko gender biased, I am very sinsitive in this issue. Uoga wa wanawake umeonekana kwenye mambo mengi, ikiwa pamoja na kuendesha magari na vitu vingine vya moto. Linganisha idadi ya ajali zinazosababishwa na wanawake ni chache sana licha ya kwamba kuna evolution kubwa ya akina dada kuendesha magari. Pia vilevile nature ya uoga ya uwanawake haimaanishi wako makini sana. Nakupa mfano huohuo wa gari, angalia umakini wa mwanamke kwenye service ya gari. Wanaume wengi watakubaliana na mimi kuwa dada zetu, sometime hata coolant tu ya gari inaweza kuwa imeisha au maji ya wiper tu, wala wanakuwa huwa hawana habari na hilo. Kwa hiyo basi wanawake wanafaa sana kutuongoza nchi ikiwa kwenye calm situation kama nchi za Scandinavia hivi, kwani kwa moyo wao wa huruma wanaweza kusaidia kuwagawa raslimali za taifa kwa usawa. Nchi zilizo kwenye turbulance, spanner mkononi kama kawaida nchi nyingi zinavyoendelea, hiyo hali inahitaji roho ngumu sana kuongoza, kama sio roho mbaya. Ni maoni yangu tu hayo lakini
   
 14. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwepo au kutokuwepo kwa ufisadi inatokana na mfumo wa chama kinachoongoza serikali iliyopo madarakani. Siyo suala la wanaume wala wanawake. Acha kudanganya watu na siasa zako za ubabaishaji.
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  mbona JESUS hakuwateua kwenye mitume wake?
   
 16. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Haitawezekana. Maneno yatakuwa yale yale.

  Behind a successful woman, there will be a man. Kama ilivyo sasa: Behind any successful man, there is a woman.
   
 17. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hakuna muarobaini. dawa ni kuwa na 'checks & balance' kwenye katiba na sheria zetu ili ufisadi usipate nafasi.
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  umefikiria vizuri kweli? Nyerere J.K. na KATIBU MKUU WA AFYA aliyeng'olewa nani mwenye huruma?
   
 19. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  BOLD: Sina hakika kama hapo ni sahihi, maana kuna mama mmoja hapo wizara Afya kasababisha sekeseke kubwa na madaktari na bado hajaonyesha hizo dalili ulizozisema.
   
Loading...