Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara

mtaji wa No 1 ni kuwa na fikra/wazo sahihi juu ya jambo au shughuli unayotaka kuifanya, pesa ni matokeo na dhamira katika jambo ' fedha si msingi wa maendeleo' - JK nyerere. tunao waibu wa kutumia raslimali watu,elimu, afya na nafasi tulizonazo kuanzsha shughuli za kutuletea maendeleo.
 
@wote mliosema hii kitu inawezekana na ni rahisi, naombeni mnikopeshe tsh 500,000 each nifanye biashara na hapo hapo nichunguze kwa kuanzia humu kama hili jambo linawezekana au lah.
 
Hili swala ni very practicle. Cha kuongeze ni kwamba mkakati wenyewe wa kuraise hiyo milion 10 inabidi uupe muda kama miezi 15 hivi.
Vilevile ni vyema ukawa unaomba support badala ya kukopa kwa sababu huwezi kuwa na uhakika lini utapata full capital ya kuanzisha biashara. Kama idea ni nzuri watu watakuchangia tu. Na usiweke kiwango rasmi cha mtu kuchangia, take michango from as many people as possible.
Halafu maisha yako unayoishi kila siku yaonekane kweli ni mtu unayetafuta pesa kwa ajili ya shughuli fulani Watu hawawezi kukuchangia kama wanaona wewe unaendelea na starehe zako kama kawaida.

Ni mtu gani atakae kuchangia tu kiivyo ulivyoelezea kirahisi?
 
ni mtu gani atakae kuchangia tu kiivyo ulivyoelezea kirahisi?

tatizo si kirahisi, ni ambie mtu anavyo taka kuchangiwa harusi huwa anatoa maelezo gnai ya ziada mpaka achangiwe pesa nyingi hivyo?

- tatizo ni wivu na unafiki, ndugu, jamaa na marafiki wako tiyali kukusapoti kwa jambo ambalo wanafahamu halitakufaidi kamwe halitabadilisha maisha yako zaidi ya kukustarehesha na maanisha harusi

- ndugu kwenye harusi huchanga si kwa sababu wanakupenda sana, no ni kwa sababu wanajua hizo pesa wanazo changa zitaliwa siku ya harusi na ndo itakuwa mwisho wa story
- ndugu, jamaa na marafiki hawako tiyali kuchangia kitu ambacho kitaenda kubadilisha maisha yako na hata kuwapita mbali
 
@wote mliosema hii kitu inawezekana na ni rahisi, naombeni mnikopeshe tsh 500,000 each nifanye biashara na hapo hapo nichunguze kwa kuanzia humu kama hili jambo linawezekana au lah.

tatizo letu watanzania vitu vya muhimu tunaingiza uatani mwingi sana na kukatishana tamaa, si zani kama mwanzisha thread alieleza michango ichangwe kutoka humu jf.

- tatizo watanzai tunapenda kuchangishana kwenye harusi tu watu wanataka wachangie kile ambacho watafaidi na wao,
kitu ambacho atafaidi mwingine hakuna aliye tiyali
 
Ni ngumu sana siku hizi kumkopa mtu hata 50000 .00 kila mtu analalamika pesa ngumu
 
Ni ngumu sana siku hizi kumkopa mtu hata 50000 .00 kila mtu analalamika pesa ngumu

Naomba nikuunge mkono 10% only. Kuna Watz wengi wenye hela. Tatizo tunaohitaji hela zao zitusaidie hatujajenga hoja nzito na zilizojaa ushawishi ili hela hizo wazitoe kwetu. Mimi niko field (ktk project kama tatu hivi) naona vijana/wazee walivyo na hela za nguvu. Lakini hao hao tukiwa mjini utawasikia ktk simu kwa jamaa zao wakilalamika kuwa hela hakuna.

Tujenge hoja za nguvu ambazo hazina chembe ya hofu, huku tukiweka vitendo mbele kwa kupunguza maneno,tutachangiwa tu. Mbinu za kuwachangisha ni lazima ziwe za kisasa zaidi.

Siku hizi hata makanisani, ukiomba mchango usio na maelezo unatoka kapa.
 
tatizo letu watanzania vitu vya muhimu tunaingiza uatani mwingi sana na kukatishana tamaa, si zani kama mwanzisha thread alieleza michango ichangwe kutoka humu jf.

tatizo watanzania tunapoona opportunity ambayo tunaweza elezea shida zetu na kusaidiwa huwa tunaambiwa hatupo serious. Mwanzisha thread kasema unaweza kuomba kwa watu wote unaofahamiana nao hata jf, facebook etc. Soma tena topic yake.
 
Ni ngumu sana siku hizi kumkopa mtu hata 50000 .00 kila mtu analalamika pesa ngumu

nakuunga mkono asilimia 99. Ni ngumu sana tena kuna wengine ukitaka mvunje mawasiliano au mahusiano yenu kama ya undugu au urafiki jaribu kumwomba hela.
 
tatizo watanzania tunapoona opportunity ambayo tunaweza elezea shida zetu na kusaidiwa huwa tunaambiwa hatupo serious. Mwanzisha thread kasema unaweza kuomba kwa watu wote unaofahamiana nao hata jf, facebook etc. Soma tena topic yake.

mkuu ni kwa watu unao fahamiana nao, sasa mfano mimi nikuombe pesa nakufamu? Au kisa nakutana na wewe humu ndo nikuombe pesa?
Mimi nimesema mtu unaye fahamina nae yaani mnajuna si mtu mlie kutana nae facebook au members wa jf ukimbilie kumwomba pesa,
 
. Mimi niko field (ktk project kama tatu hivi) naona vijana/wazee walivyo na hela za nguvu. Lakini hao hao tukiwa mjini utawasikia ktk simu kwa jamaa zao wakilalamika kuwa hela hakuna.
umeona hapo? Mtu unayemfata akusaidie anakwambia hana hela, hiyo hoja nzito utaijenga sa ngapi? Hata kama ulishaijenga na yeye hayupo tayari kusikiliza hoja zako utamlazimisha? Jamaa zako ni mifano mizuri inayoonesha kuwa hili jambo ni gumu.
Kuna watu wana hela haswa ila ndio wanaongoza kwa kulalamika wana shida ikiwa ni kivuli cha kuepuka kusaidia wengine.
 
mkuu ni kwa watu unao fahamiana nao, sasa mfano mimi nikuombe pesa nakufamu? Au kisa nakutana na wewe humu ndo nikuombe pesa?
Mimi nimesema mtu unaye fahamina nae yaani mnajuna si mtu mlie kutana nae facebook au members wa jf ukimbilie kumwomba pesa,

watu wanafahamiana kupitia sehemu mbali mbali. Kuna watu wamekutana humu humu wameanzisha saccos, partnership na maprojects kibao ya kuingiza pesa.
 
Naomba nikuunge mkono 10% only. Kuna Watz wengi wenye hela. Tatizo tunaohitaji hela zao zitusaidie hatujajenga hoja nzito na zilizojaa ushawishi ili hela hizo wazitoe kwetu. Mimi niko field (ktk project kama tatu hivi) naona vijana/wazee walivyo na hela za nguvu. Lakini hao hao tukiwa mjini utawasikia ktk simu kwa jamaa zao wakilalamika kuwa hela hakuna.

Tujenge hoja za nguvu ambazo hazina chembe ya hofu, huku tukiweka vitendo mbele kwa kupunguza maneno,tutachangiwa tu. Mbinu za kuwachangisha ni lazima ziwe za kisasa zaidi.

Siku hizi hata makanisani, ukiomba mchango usio na maelezo unatoka kapa.

Umenichekesha sana! Mkuu, hata huyo mwenye hela nyingi anayo mambo yake mengi tu kapanga kufanya. Kama alikuwa anakaa nyumba ya kupanga anataka akae nyumba yake mwenyewe, kama watoto wake walikuwa shule za kata anapenda wakasome international, kama alikuwa na RAV4 angependa amiliki V8. Hivyo usitegemee kupata hela kirahisi.
 
umeona hapo? Mtu unayemfata akusaidie anakwambia hana hela, hiyo hoja nzito utaijenga sa ngapi? Hata kama ulishaijenga na yeye hayupo tayari kusikiliza hoja zako utamlazimisha? Jamaa zako ni mifano mizuri inayoonesha kuwa hili jambo ni gumu.
Kuna watu wana hela haswa ila ndio wanaongoza kwa kulalamika wana shida ikiwa ni kivuli cha kuepuka kusaidia wengine.

Nashukuru umekubaliana nami kwamba wapo jamaa zetu wana hela za kutosha kabisa, na kwamba tabia ya kusaidiana miongoni mwetu kama jamii haipo.

Sasa mbinu za kuzitoa fedha toka kwa jamaa zetu ndio mtihani mkubwa. Ukimpa wazo lako atakukatisha tamaa, na baadae analichukua yy.
 
Heshima kwenu wadau,
Kibiashara kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara hasa kwa zile zinazoanza ingawa nyingi kati ya hizo ni NGUMU sana, hivyo kupelekea watu wengi kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini hushindwa kuyafanikisha kutokana na mitaji. Kwa mtazamo wangu, naona kama ukitumia njia ya kuomba fedha kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi walio karibu yako, wanaokuamini, kukuheshimu, kukufahamu na wenye uwezo kiasi itakuwa njia rahisi ukilinganisha na mikopo kutoka taasisi za kifedha ambapo utajikuta unafanya biashara kwa presha na hofu ya kurejesha deni. unaweza kufanya kama ifuatavyo kwa kuchukulia uhitaji wa mtaji wa Tsh 10,000,000:

1 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 100,000 kutoka kwa watu 100 = Tsh 10,000,000
2 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 200,000 kutoka kwa watu 50 = Tsh 10,000,000
3 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 350,000 kutoka kwa watu 30 = Tsh 10,000,000
4 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 500,000 kutoka kwa watu 20 = Tsh 10,000,000
5 - kuomba / kuazima / kukopa Tsh 1,000,000 kutoka kwa watu 10 = Tsh 10,000,000

NB: - Naamini tunafahamiana na watu wengi sana tangu mtoto unakua hadi hapo ulipo, kuanzia uliocheza nao, marafiki wa primary, sekondary, vyuo, kazini, majirani, ndugu, jamaa, marafiki, marafiki uliojuana nao kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter nk..nina hakika hutakosa watu wasiopungua 100 wenye nia, uelewa na uwezo wa kukufanikishia hili.
- Uhitaji, madhumuni ya kuomba, muda wa kurejesha, malengo ya matumizi inategemea na makubaliano yako na unayemuomba, na si lazima hao watu utakao waomba wajue kusudio lako la njia hii ya kupata mtaji, pia usiombe kama msaada, omba kama mkopo ili baada ya muda mfupi kama miezi miwili ama mitatu uahidi kurejesha.
- Nina imani kiasi cha Tsh 10,000,000 ni mtaji tosha kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Mfano: jiko la baa, kibanda cha chips, salon ya kiume, stationary, internet cafe, duka la jumla, duka la kawaida, genge, grecery, bajaji, duka la nguo hasa mitumba bomba nk.. ambapo itakuwa rahisi kwako kwa muda wa miezi mitatu kuweza kurejesha fedha ulizoomba.

Nawasilisha.

Mjomba bora ukope mil 10 sehemu moja kuliko kwa sehemu 100! Hevu fikiria deni la mtu/taasisi moja linavozingua.
Sasa kwa design hiyo ya kwako ina maana timbwili la kudaiwa linakuwa kwa watu tofauti na kila mmoja na design yake ya kudai kama ambavyo mlikubaliana!

Kwa kifupi utapata stres ambazo hutokaa uzisahau katika maisha yako!!
 
Labda usingizie harusi ha[o utapata pesa ila hivi hivi tu kwa hawa wabongo sahau
 
capital financing= owners equity+loan financing

maana
mtaji unatokana na hela yako na ya kukopa.

ukiwa na milioni sita kopa milioni nne iwe kumi.

sio vizuri kufanya biashara bila kukopa. kukopa kunakufanya uwe makini na mirradi yako ukiogopa kufulia.

ukiwa na mkopo mkubwa kupita hela yako ni hatari. pia ukiwa mradi wako mi.10 zote ni za kukopa benk, hapo ndipo watu hukimbia mji......
 
kuna kitu wanaitaga starting capital without capital, yaan unatengeneza mtaji pasipo mtaji, natamani kupata mtu wa kunielimisha kuhusu hili, niliwah kuhudhuria semina moja ya wajasiramali walikua wanalizungumzia jinsi ya kutengeneza mtaji pasipo kuhitajika kuwa hata na shilingi., sasa nlikua nimechelewa kidogo hata vipeperush hawakua navyo na kila nliemuomba anielekeze alisema hajaelewa... mpaka leo bado linaniumiza kichwa sana wadau, naomba mwenye uelewa na hili anisaidie jamani,.,Ntashukuru sana maana natamani kushare hili na vijana wenzangu lakini sina uelewa wa kutosha kuhusu hili suala.Ahsanteni
 
Back
Top Bottom