Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara

Je wewe uliwahi kupata mtaji kwa njia hizo ?? kuzungumza ni rahisi sana
Ndiyo Mkuu. Kwa kutumia ujuzi na elimu niliyopata ndiyo nilianza. Na hata baadae tukaungana na wahitimu wenzangu kuunda kampuni, mtaji wetu mkubwa ukiwa ni elimu tuliyopata badala ya kusubiri kuajiriwa tukajiajiri wenyewe. Na ss tumeajiri. Mtaji wa kusajili kampuni unaanzia 20,000/= usiogope kaka kutumia taaluma yako kujiajiri.
 
Kabla kufikikiria kupata mtaji wabiashara au waujasiriamali nilazima ujitafikari kwakina.
asilimia kubwa ya watanzania ni maskini(fukara) bila atawao kujifahamu. Kutoka kwenye umaskini sio simple kma muandika makala alivoandika
 
Kabla kufikikiria kupata mtaji wabiashara au waujasiriamali nilazima ujitafikari kwakina.
asilimia kubwa ya watanzania ni maskini(fukara) bila atawao kujifahamu. Kutoka kwenye umaskini sio simple kma muandika makala alivoandika
Heshima yako
Mkuu immu bin masoud rudia tena kusoma hiyo Makala nadhani utaielewa vema zaidi. Pili, njia zote hapo hakuna asieweza kuiweka kivitendo kwa sababu ni mambo ambayo tunaweza kutekeleza na yanatekelezeka ila hatuna uthubutu na hatupo 'smart' ktk kutoa vipaumbele vya msingi kwa mambo ya maana
Vlvl hii ni muendelezo wa makala na mada zangu ambazo huwa nazileta humu jukwaani. Kwa hy masuala ya kufanya tafakuri yalishajadiliwa kabla. Mfano mmojawapo huu hapa
Makala: Wazo la biashara na makosa yake
 
Habari wana jukwaa!
Napenda tujadili jambo linaloumiza vichwa vyetu la namna gani naweza kupata mtaji wa kubadilisha mawazo yetu na fursa za biashara na ujasiriamali na kuwa kipato halisi. Ntajitahidi kuielezea mada hii kwa kugusia dondoo muhimu ili tuweze kujikwamua kwa namna moja au nyingine katika jambo hili.
Dondoo muhimu ambazo twapaswa kuzifahamu kuhusiana na namna gani nitapata mtaji wa kuanzisha biashara au ujasiriamali ni kama ifuatavyo:
  • Mtaji ni nini?
  • Nahitaji kujua nini katika kupata mtaji
  • Njia zipi nitumie kupata mtaji
UTANGULIZI
Tumekuwa na kasumba ya kuwaza kuwa bila Mtaji (pesa) basi sio rahisi kufanya uwekezaji wowote. Lakini kimsingi utaona mtaji sio kipaumbele cha kwanza katika kufanya uwekezaji wowote. Ili uanze uwekezaji iwe biashara au ujasiriamali mambo muhimu ya awali ni 1. Wazo la biashara ambalo unaweza kuligeuza kuwa Fursa ya Biashara 2. Jitihada na uthubutu wa kufanya fursa ya biashara ilete mapato 3. Mtaji ambao unaweza kuwa katika muundo wa kirasilimali fedha au rasilimali nyingine wezeshi
  • MTAJI NI NINI?
Mtaji ni rasilimali unayowekeza ili kuikuza na hatimaye kupata faida kwenye uwekezaji (biashara au ujasiriamali) uliobuni na kuanzisha. Mtaji unaweza kuwa pesa taslim au rasilimali mbadala wa fedha
Aina za Mitaji
  • Rasilimali watu
  • Mtaji wa fedha
  • Kipaji, taaluma, ujuzi
  • Rasilimali binafsi unazomiliki
  • NAHITAJI KUJUA NINI KATIKA KUPATA MTAJI
Ni muhimu sana kujiuliza maswali haya kabla ya kuanza Uwekezaji (biashara/ujasiriamali) kwani yatakusaidia katika kujua kiasi halisi cha mtaji unaouhitaji
  • Kwa nini unataka kuanzisha uwekezaji?
  • Una utayari wa kufanya biashara/ujasiriamali unayotaka kuifanya?
  • Je una malengo gani na uwekezaji unaotaka kuufanya?
  • Je una ujuzi/elimu ya kuweza kumudu uwekezaji unaotaka kuufanya?
  • MTAJI kiasi gani nahitaji kupata ili kuanzisha uwekezaji.
  • Muundo gani wauwekezaji unaona wafaa katika kuanzisha uwekezaji huo? Ie Sole Proprietor, Partnership or Limited Company?
  • NJIA ZIPI ZA KUPATA MTAJI
Fedha kwa ajili ya mtaji unaweza kupata kutokana na njia mbalimbali, miongoni mwa njia hizo ni pamoja na
  • Kuweka akiba kutokana na kile unachopata
Jitahidi kuwa na bajeti ambayo unajibana na kubakiza japo kiasi kidogo katika matumizi yako. Matumizi mabovu ya fedha imekuwa changamoto kubwa katika kuweka akiba. Na hii akiba unayopata jitahidi kufanya yale unayoweza katika uwekezaji kwani tayari utakuwa unajua kiasi gani unahitaji kupata kuisimamisha biashara yako
  • Kupata mkopo kupitia “maandiko ya michanganuo” mbalimbali inayokopesheka
Kuna taasisi na mashirika ya serikali yasiyo ya kiserikali, yamekuwa yanatoa aina mbalimbali za mitaji kama ruzuku na mikopo myepesi kutokana na namna gani mtu mmoja au kikundi umeweza/mmeweza kuandaa andiko lenu. Changamoto kubwa ya kukosa pesa hizi ni kutokana na Maandiko yetu mengi yanalenga faida binafsi kuliko manufaa ya jamii ambayo jamii itapata hivyo kutokuwa na sifa
  • Mitaji kupitia michango
Unanufaika vipi kuwa katika magrupu mengi ya kijamii? Shawishi wanakikundi wenzako mchangiane japo kiasi kidogo kidogo kuwezeshana kiuchumi na sio muda wote kupiga porojo. Inaweza pia michango kutoka katika ngazi ya marafiki, ndugu, jamaa nk
  • Dizaini wazo ambalo ni jepesi kiutekelezaji
Fanya wazo lako la biashara liwe jepesi kuligeuza kuwa fursa ya biashara kwa kutumia zile rasilimali ulizonazo. Kadiri unapopata hela ndipo unapolitanua wazo lako kwa kuliboresha zaidi na zaidi
  • Fanya kampeni za kimasoko kwa huduma au biashara uliyobunu
Unaweza kuanza kufanya biashara au huduma kwa kutoa kidogo kidogo kwa wateja unawafuata walipo. Hii itakusaidia kutokuwa na gharama mbalimbali za kuendesha biashara. Hivyo pesa kidogo au taaluma uliyonayo ndiyo itakuingizia pesa ambayo taratibu utapata mtaji mkubwa
  • Kamisheni kutoka makampuni mbalimbali
Kuna baadhi ya makampuni yanatoa kamisheni kwa kuwa ajenti wao kwa kuuza au kutangaza bidhaa zao. Kadiri unavyouza zaidi bidhaa zao au huduma zao ndivyo unavyopata kamisheni yako zaidi. Kamisheni ajenti ni biashara kama biashara nyingine
Karibuni kwa mjadala kwa kuangalia njia nyingine zaidi kupata mtaji
Makala imejitosheleza. Wengi tunatamani kufanya biashara au ujasiriamali lakni hatujui hasa "vp tunaanza kuicheza ngoma"!
 
Ni taasisi gani zinatoa pesa kwa "michanganuo ya biashara"?........ una hoja nzuri hongera
Asante Mkuu
Cheki na SIDO, NEEC, Mashirika ya kimataifa kutokana na malengo ya mradi wako (jitahidi uwe na mtazamo wa kuisaidia jamii). Na websites nyingine nitazileta za mashindano ya uandishi wa Michanganuo ya biashara. (Hili litakuwa zoezi endelevu na itakuja kama MADA MPYA)
 
Habarini wanajamvi, Mimi kijana Mwenye Nia ya kujiajiri, nimemaliza chuo Mwaka Huu mwezi wa 8 Mara baada ya kumaliza masomo yangu niliamua kuanzisha biashara ya nafaka, nimeifanya baadae nikapata wazo la kuanzisha frame, lakini nikawa Sina uwezo wa kulipia frame Kulingana na ufinyu wa mtaji niliokuwa nao, Hivyo Kuna ndugu yangu nikamshurikisha kuhusu kuniongezea mtaji na yeye Akasema atanisaidia. Hapo ndipo nikapata matumaini ya kulipia frame na kupelekea upungufu Kwenye kimtaji nilichokuwa nacho. Bahati mbaya mpaka Sasa yapata wiki 1 huyu ndugu Napiga simu yake Hapokei Wala sms hajibu Ila nikimwangalia Whatsap yuko online, kwa ninavyomjua ameshindwa kuwa muwazi kwamba amekwama.
Mkataba wa frame unazidi kusoma, Leo nimekuja kwenu nikiamini JF ni jukwaa lenye lengo la kuelimishana, na kusaidiana kwa namna moja au nyingine Mwenye Mawazo, au namna Yeyote aweze kunisaidia, Nitashukru Sana kwa comment zenu zenye kunijenga na Mungu atakubariki.
 
Habarini wanajamvi, Mimi kijana Mwenye Nia ya kujiajiri, nimemaliza chuo Mwaka Huu mwezi wa 8 Mara baada ya kumaliza masomo yangu niliamua kuanzisha biashara ya nafaka, nimeifanya baadae nikapata wazo la kuanzisha frame, lakini nikawa Sina uwezo wa kulipia frame Kulingana na ufinyu wa mtaji niliokuwa nao, Hivyo Kuna ndugu yangu nikamshurikisha kuhusu kuniongezea mtaji na yeye Akasema atanisaidia. Hapo ndipo nikapata matumaini ya kulipia frame na kupelekea upungufu Kwenye kimtaji nilichokuwa nacho. Bahati mbaya mpaka Sasa yapata wiki 1 huyu ndugu Napiga simu yake Hapokei Wala sms hajibu Ila nikimwangalia Whatsap yuko online, kwa ninavyomjua ameshindwa kuwa muwazi kwamba amekwama.
Mkataba wa frame unazidi kusoma, Leo nimekuja kwenu nikiamini JF ni jukwaa lenye lengo la kuelimishana, na kusaidiana kwa namna moja au nyingine Mwenye Mawazo, au namna Yeyote aweze kunisaidia, Nitashukru Sana kwa comment zenu zenye kunijenga na Mungu atakubariki.
 
Back
Top Bottom