Njia rahisi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara

Kama kichwa cha habari kinavyosema

Ukiachana na hizi njia ambazo wengi wetu tunazijua za kupata mtaji kama kukopa,Mali kauli(nauza nitaleta ela) kutumia ajira yaan mshaara,kuweka rehani kitu Fulani cha thamani,kuuza kitu Fulani mfano nyumba.wengine wanaolewa kwa lengo la kupata mtaji hahahah..yote sawa!!

Swali unakumbuka jinsi ulivyoanzisha biashara na njia gani ulitumia na kama unamshauri mtu ungemshauri atumie njia gani???

Naomba kuwasilisha.
 
Njia rahisi ni kuanza biashara ndogo na kuikuza kidogo kidogo mpaka baada ya miaka kadhaa inakuwa ishajizidisha mara 10, mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe
Iyo biashara ndogo mtaji wake ndo swali lilipo.... maana hata laki moja inatosha kuanzisha biashara ndogo.unaanza na laki tuseme unatoa wap??
 
1. Mtaji namba moja ni akili/ubunifu na plans za aina ya biashara yenye unafikiria kuifanya.
2. Mtaji namba mbili ni nguvu, ili uweze kufanya kibarua chochote halali ili uweze kupata fedha ya kuanzisha aina ya biashara unayo ifikiria.
3. Mtaji namba tatu ni Nidhamu na Bidii.
 
Iyo biashara ndogo mtaji wake ndo swali lilipo.... maana hata laki moja inatosha kuanzisha biashara ndogo.unaanza na laki tuseme unatoa wap??
Waweza dunduliza kwenye kibubu (kujinyima), kopa marafiki, omba kwa wanafamilia wenye uwezo mfano wazazi ndugu wa karibu au mpenzi, omba kwa wafadhili watu wenye pesa zao kama kina mengi huwa wanasaidia wajasiriamali wadogo
 
1. Mtaji namba moja ni akili/ubunifu na plans za aina ya biashara yenye unafikiria kuifanya.
2. Mtaji namba mbili ni nguvu, ili uweze kufanya kibarua chochote halali ili uweze kupata fedha ya kuanzisha aina ya biashara unayo ifikiria.
3. Mtaji namba tatu ni Nidhamu na Bidii.
Thanks..
 
1. Mtaji namba moja ni akili/ubunifu na plans za aina ya biashara yenye unafikiria kuifanya.
2. Mtaji namba mbili ni nguvu, ili uweze kufanya kibarua chochote halali ili uweze kupata fedha ya kuanzisha aina ya biashara unayo ifikiria.
3. Mtaji namba tatu ni Nidhamu na Bidii.

Naunga mkono hasa point ya kwanza. Kwa mtajo wako wa akili hamna atakae kufilisi wala kukuibia. Utachimba kima chako mwenyewe ideas na nini vha kufanya mpama hesabu isimame.

Nitarudi
 
Habari wana jukwaa!
Napenda tujadili jambo linaloumiza vichwa vyetu la namna gani naweza kupata mtaji wa kubadilisha mawazo yetu na fursa za biashara na ujasiriamali na kuwa kipato halisi. Ntajitahidi kuielezea mada hii kwa kugusia dondoo muhimu ili tuweze kujikwamua kwa namna moja au nyingine katika jambo hili.
Dondoo muhimu ambazo twapaswa kuzifahamu kuhusiana na namna gani nitapata mtaji wa kuanzisha biashara au ujasiriamali ni kama ifuatavyo:
  • Mtaji ni nini?
  • Nahitaji kujua nini katika kupata mtaji
  • Njia zipi nitumie kupata mtaji
UTANGULIZI
Tumekuwa na kasumba ya kuwaza kuwa bila Mtaji (pesa) basi sio rahisi kufanya uwekezaji wowote. Lakini kimsingi utaona mtaji sio kipaumbele cha kwanza katika kufanya uwekezaji wowote. Ili uanze uwekezaji iwe biashara au ujasiriamali mambo muhimu ya awali ni 1. Wazo la biashara ambalo unaweza kuligeuza kuwa Fursa ya Biashara 2. Jitihada na uthubutu wa kufanya fursa ya biashara ilete mapato 3. Mtaji ambao unaweza kuwa katika muundo wa kirasilimali fedha au rasilimali nyingine wezeshi
  • MTAJI NI NINI?
Mtaji ni rasilimali unayowekeza ili kuikuza na hatimaye kupata faida kwenye uwekezaji (biashara au ujasiriamali) uliobuni na kuanzisha. Mtaji unaweza kuwa pesa taslim au rasilimali mbadala wa fedha
Aina za Mitaji
  • Rasilimali watu
  • Mtaji wa fedha
  • Kipaji, taaluma, ujuzi
  • Rasilimali binafsi unazomiliki
  • NAHITAJI KUJUA NINI KATIKA KUPATA MTAJI
Ni muhimu sana kujiuliza maswali haya kabla ya kuanza Uwekezaji (biashara/ujasiriamali) kwani yatakusaidia katika kujua kiasi halisi cha mtaji unaouhitaji
  • Kwa nini unataka kuanzisha uwekezaji?
  • Una utayari wa kufanya biashara/ujasiriamali unayotaka kuifanya?
  • Je una malengo gani na uwekezaji unaotaka kuufanya?
  • Je una ujuzi/elimu ya kuweza kumudu uwekezaji unaotaka kuufanya?
  • MTAJI kiasi gani nahitaji kupata ili kuanzisha uwekezaji.
  • Muundo gani wauwekezaji unaona wafaa katika kuanzisha uwekezaji huo? Ie Sole Proprietor, Partnership or Limited Company?
  • NJIA ZIPI ZA KUPATA MTAJI
Fedha kwa ajili ya mtaji unaweza kupata kutokana na njia mbalimbali, miongoni mwa njia hizo ni pamoja na
  • Kuweka akiba kutokana na kile unachopata
Jitahidi kuwa na bajeti ambayo unajibana na kubakiza japo kiasi kidogo katika matumizi yako. Matumizi mabovu ya fedha imekuwa changamoto kubwa katika kuweka akiba. Na hii akiba unayopata jitahidi kufanya yale unayoweza katika uwekezaji kwani tayari utakuwa unajua kiasi gani unahitaji kupata kuisimamisha biashara yako
  • Kupata mkopo kupitia “maandiko ya michanganuo” mbalimbali inayokopesheka
Kuna taasisi na mashirika ya serikali yasiyo ya kiserikali, yamekuwa yanatoa aina mbalimbali za mitaji kama ruzuku na mikopo myepesi kutokana na namna gani mtu mmoja au kikundi umeweza/mmeweza kuandaa andiko lenu. Changamoto kubwa ya kukosa pesa hizi ni kutokana na Maandiko yetu mengi yanalenga faida binafsi kuliko manufaa ya jamii ambayo jamii itapata hivyo kutokuwa na sifa
  • Mitaji kupitia michango
Unanufaika vipi kuwa katika magrupu mengi ya kijamii? Shawishi wanakikundi wenzako mchangiane japo kiasi kidogo kidogo kuwezeshana kiuchumi na sio muda wote kupiga porojo. Inaweza pia michango kutoka katika ngazi ya marafiki, ndugu, jamaa nk
  • Dizaini wazo ambalo ni jepesi kiutekelezaji
Fanya wazo lako la biashara liwe jepesi kuligeuza kuwa fursa ya biashara kwa kutumia zile rasilimali ulizonazo. Kadiri unapopata hela ndipo unapolitanua wazo lako kwa kuliboresha zaidi na zaidi
  • Fanya kampeni za kimasoko kwa huduma au biashara uliyobunu
Unaweza kuanza kufanya biashara au huduma kwa kutoa kidogo kidogo kwa wateja unawafuata walipo. Hii itakusaidia kutokuwa na gharama mbalimbali za kuendesha biashara. Hivyo pesa kidogo au taaluma uliyonayo ndiyo itakuingizia pesa ambayo taratibu utapata mtaji mkubwa
  • Kamisheni kutoka makampuni mbalimbali
Kuna baadhi ya makampuni yanatoa kamisheni kwa kuwa ajenti wao kwa kuuza au kutangaza bidhaa zao. Kadiri unavyouza zaidi bidhaa zao au huduma zao ndivyo unavyopata kamisheni yako zaidi. Kamisheni ajenti ni biashara kama biashara nyingine
Karibuni kwa mjadala kwa kuangalia njia nyingine zaidi kupata mtaji
 
Upo Sawa sana mkuu, ingawa kunatofauti kubwa pale linapo fikia kufanya kwa vitendo. Hapo ndio huwa tunagundua kwamba kumbe maharage ni mbegu na sio mboga.
 
Upo Sawa sana mkuu, ingawa kunatofauti kubwa pale linapo fikia kufanya kwa vitendo. Hapo ndio huwa tunagundua kwamba kumbe maharage ni mbegu na sio mboga.
Utofauti unakuja kutokana na kutokuwa na mpangokazi wa kufikia malengo. Tumekuwa na tatizo kubwa la mtu akipata wazo la biashara moja kwa moja anataka kulitekeleza. Hakai chini na kufanya tafakuri jadidi na kupata majibu ya kama niliyoainisha hapo juu ktk makala. Nadhani ktk jamii umewahi kutana na watu anakwambia mimi nikipata hela ndiyo ntaamua nifanye nini au biashara gani? Hili nalo kosa maana hata akipata hiyo pesa bila kuwa na mpango kamambe aliojiwekea kabla wa matumizi ya fedha (proper financial management) ataishia kuimaliza pesa yote bila kufika malengo tarajiwa
 
Back
Top Bottom