Njia rahisi ya kufika home

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108


Kuna watu wameomba niwaelekeze Temeke nilipo naomba ufuate maelekezo nyoosha na hii barabara moja kwa moja





<tbody>
</tbody>
Mbele utakuta mama lishe wanapakuwa chakula waache sogea kidogo

<tbody>
</tbody>
utakuta toroli limebeba matenga ya nyanya msubiri apite na wewe upite

<tbody>
</tbody>
ukivuka tu utakuta choo kinazibuliwa sogea mbele

<tbody>
</tbody>
utakutana na choo hiki kata kushoto

<tbody>
</tbody>
Mbele utaona uchochoro halafu kuna maji machafu yanakatisha ufatishe moja kwa moja

halafu ukiona wazungu wawili wanaingia kwenye mgahawa anza kuhesabu nyumba ya tano kutoka hapo natumai tutakuwa tumeelewana mpaka hapo
Ramadhani njema wadau.
 
huku ndo kule ukifika stendi usiondoke kaa hapo hapo nakuja kukuchukua zaidi ya hapo utajuta kwanini ulienda kuitafuta nyumba..
 
Huku ndo home mzizi?? Chondechonde ndugu yangu hama huko haraka!huko ndiyo makao makuu ya kipindupindu,usisubiri uanze kuharisha kwa mdomo mheshimiwa
 
Uswazi bwana, mtu utakuta anasema "mtaani kwetu watu wanakera sana....", sasa hebu fika huko kwao uone kama utaona hata huo mtaa, ni mrundikano wa nyumba zilizojengwa kiholela tu.
 
huku ndo kule ukifika stendi usiondoke kaa hapo hapo nakuja kukuchukua zaidi ya hapo utajuta kwanini ulienda kuitafuta nyumba..

kuna mtu kwao msasani bonde la mpunga, nilikuwa namsubiria ccbrt. Nishamrudisha kwao na kuwatembelea zaidi ya mara 5. Ila njia siijui. Funniest part ni kuwa na kurudi barabarani ilikuwa inabidi nipewe mtoto wa kunipeleka manake nisingetokezea. Im glad ndugu yangu aliachana na yule bwana, mweh!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom