Njia rahisi inayokuwezesha kujua kama mtoto ni wako au sio wako

TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
811
968
Unaweza kujua mtoto sio wako kwa jaribio rahisi tu. Nalo ni kutumia blood test. Angalia chati hii:

Paternity_Blood_type_Chart-590.jpg


Kutoka kwenye blood group chart:

1. Kama ukipima na kukuta group la mtoto linaendana na magroup ya damu ya wazazi, sio guarantee kuwa mtoto ni wa kwako. Kwa sababu kuna uwezekano wa mwanaume mwenye group la damu kama yako au jingine ambaye akizaa na mkeo mtoto ataonekana ni wa kwako. Baada ya matokeo haya, kupata uhakika kama mtoto ni wako au sio, nenda kafanye DNA test. DNA test hutoa majibu ya uhakika kwa 99.9%.

2. Ukikuta group la mtoto haliendani na ya wazazi, jua 100% mtoto sio wako.

Kufanya blood group test, nenda hospitali, wewe, mama na mtoto, utatozwa kiasi cha TZS 10,000 - 15,000 kwa kila mtu.

Majibu ya kweli ya njia hii, ni yale yanayodisapprove kuwa mtoto sio wako, yaani namba 2 kama nilivyoeleza hapo juu.

Unaweza kuwa tayari una majibu ya blood group la mama kwa kutumia kadi ya kliniki, na unaweza kuwa ulipima na kujua blood group lako, kwa hiyo hapa kazi iliyobaki ni kujua blood group la mtoto na kuangalia hiyo chati.

Ukikuta mtoto sio wako mlee, lakini ukweli utakuwa umekuweka huru.
 
Upo sawa. Lakini tahadhari itolewe kuhusu matatizo yanayoweza kutokea kama vile mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi. Pia kupata shinikizo la damu na matatizo ya kiafya baada ya kugundua ukweli kuhusu mtoto. Wahenga walituasa, kitanda hakizai haramu. Kuna busara na hekima katika huo msemo huo.
 
Upo sawa. Lakini tahadhari itolewe kuhusu matatizo yanayoweza kutokea kama vile mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi. Pia kupata shinikizo la damu na matatizo ya kiafya baada ya kugundua ukweli kuhusu mtoto. Wahenga walituasa, kitanda hakizai haramu. Kuna busara na hekima katika hilo msemo huo.

Ni kweli, lakini ukweli utakuweka huru. Leo hihii ukiamua, na Mungu akawa upande wako, namaanisha namba 2 ikatiki, utajua mtoto si wako.
 
Kwahiyo unafikiri ukijua ndio utakuwa huru,au ndio umefumua matatizo!labda kama mkeo mlishachokana hivyo unamtafutia sababu muachane, ukumbuke ukikuta sio wako kitakachofuata ni kutomuamini mkeo tena. Wewe mwenyewe utaanza kupata mateso ya kuchomoa upendo wako kwa mtoto ambaye uliamini ni wako na yeye alijua wewe ni baba yake, hii nayo itakutesa sana, jiandae kisaikolojia kuumia kwa kujua kuwa marafiki na ndugu pia nao sasa watajua kuwa kumbe mkeo kachezewa sana bila ya wewe kujua...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Umeishamlea Kiumbe kwa zaidi ya miaka 18 halafu, sijui unatafuta nini, unagundua kuwa sio mwanao!
So? Unamuambia kuwa mimi sio baba yako?

Unafahamu athari ya hili kwa Kiumbe ambacho toka kianze kupata ufahamu duniani kinajua kwamba wewe ndiye Baba yake?

Kitanda hakizai Haramu. Endelea kulea Kiumbe maana hana Kosa lolote katika hili na Dhambi iache kwa aliyeuza Mechi hadi yakayokea hayo...!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana nawe kabisa.
DNA ya asili na ya uhakika ni kupitia Dada zako, Shangazi zako au mama zako wakimuona mtoto tu watakwambia kama ni wako au la! Hafu kwa uzoefu nilionao mtoto kama ni wako utaona zile force of attraction kati ya mtoto na baba mzazi
 
Back
Top Bottom