Njia panda ya Rais Samia

Swali tu ni lazima awe rais?

Mambo mengine ni upuuxi Na ubatili mtupu. Oooh ondoa sukuma gang oooh wanamuhujumu ohhh shit. Hiyo ndo kazi yake sisi wapumbavu Ndo tunajifanya wajuaji wa mambo that’s stupidity. Hakuna urais rojooo hata alete watu toka wapi wezi hawakosekani. Chadema wenyewe wanaibiana ruzuku. Act wazalendo ndo hovyo kabsaa.

So let’s shut our mouths Na tumuache mheshimiwa rais atimize wajibu wake. Urais siyo lelemama Na hajalazimishwa.
 
Hao waliopiga pesa ndefu wizara ya fedha mbona ni wateule wake,kuanzia waziri na katibu mkuu. Hapo napo sukumagang.
Vipi bodi aliyoivunja ya TPA si zao lake?

Nitajieni rais aliyepita bila kupigia magoti sukumagang,ndo maana Hangaya Kona mbili anarudi Kanda ya sukumagang.
Chezea sukumagang ni Kama upepo huwezi kuuzuia.
Sukuma gang wanamtesa sana hajui awatose au aishi nao kwa akili.
 
Akiweza kuacha katiba mpya iliyo bora ndio itakuwa legacy yake.
Kitaalamu tunaiita MALALAMIKO KANTRI.
Wananchi wanalalamika TOZO, wananchi wanalalamika UMEME, wananchi wanalalamika MAJI, machinga wanalalamika biashara zao kuharibiwa na Rais analalamika anaangushiwa jumba bovu, nani wa kumfariji mwenzie katika nchi hii..Nchi ngumu sana hii

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ni dhahiri kuwa Uraisi sio kazi ndogo mara kadhaa Rais Samia amenukuliwa akiongea kwa upole na unyenyekevu(sijui kama unatoka moyoni) katika medani za kisiasa.

Mara ya mwisho aliwaasa wateule wake kuchapa kazi na kuwa hatatumia nguvu kuwasukuma
bali atatumia wino kuwanyoosha(akili).

Katika hali isiyotegemewa Rais Samia ameonekana kwa mara ya kwanza akifoka kwa jazba na kulaumu

Awamu zilizopita(kimsingi ni iliyopita kwa ushahidi wa mazingira) japo hakutaka kuweka wazi ni awamu ipi haswaa.

Kinachooonekana ni kuwa Rais Samia hana imani na viongozi wa awamu iliyopita na havutiwi nao hilo sio tatizo

Kwani marais wote huchagua safu ambayo itakuwa na mwelekeo na falsafa za awamu husika ambayo raisi atakuwa na imani nayo.

Tatizo ni kuwa Rais Samia anaonekana kuwa njia panda na hapa ndipo nikakumbuka play ya dillema of the ghost

Kwenye tamthilia hii kuna kijana(Ato Yawson) aliyeenda kusoma ulaya na kurudi na mlibwende afroamerica(Eulalie)

Kwa fahari kubwa huko kijijini kwao Ghana. Kwa masikitiko makubwa kijana huyu hakufikiria ni kwa jinsi gani mlimbwende huyu ataweza kuishi na kuendana na jamii na mazingira yake kitu kilichopelekea culture clush(a situation in which the diverging attitudes, morals, opinions, or customs of two dissimilar cultures or subcultures are revealed) kitu kilichopelekea kuvunjika kwa ndoa yao.

Ni wakati muafaka kwa Rais Samia kuchagua moja aachane na watangulizi wa Magufuli awe huru(huru kweli kweli)

Au akubali kuwa mtumwa wa Magufuli kuwaridhisha magufulist kwa kutenda kama Magufuli.
Kwa vyovyote vile Samia haonekani kuweza kuendelea kufanya kazi na Magufulist kama wafuasi wake watiifu isipokuwa kwa kutaka kulilidhisha kundi hilo tu. Hata kama Magufulist hawa watafanya kazi kwa kiwango gani.

Rais Samia haonekani kuwa na imani nao kwani inaonekana kunaajenda ziko nyuma yao.

Ni wakati sasa umefika kwa Rais Samia kuvuka mto ng'ambo ya pili na kuachana na mtangulizi wake ili aweze kuendelea na safari yake, ili aanze kutengeneza matatizo yake mwenyewe badala ya kuishi kuendelea na matatizo ya mtangulizi wake.

Sisemi kuwa wateule wa Magufuli walikuwa wabaya walikuwa wazuri na walimufaa Magufuli, Samia ni wakati wake wa kuchagua wateule watakao mfaa ili awe huru kuwajibika kwa wateule wake na si kuangushiwa jumba bovu tena.

Yawezekana magufulist(sukuma gang) wasimuelewe/tusimuelewe leo, kesho watamuelewa badala ya kustack sehemu moja.

Namtakia mafanikio mema katika safari yake mpya ninayotarajia anaenda kuianzisha.

NB: Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge.

Du, sema tu kazi ya urais ni ngumu kwa sababu sehemu kubwa ni watu wa ndani hukohuko. Yeye ataondoka na kuwaacha wakiendelea na kazi zingine.
 
Mbona mama ameshatoa mikeka ya kutosha tu ya mawaziri na manaibu hadi ya wakuu wa wilaya ametoa au na hao anowaweka siyo wa kwake na kama cyo wa kwake kwa nn anashindwa kutumia power yake
Hivi kumbe hawezi kutumia power yake kuwanyoosha watendaji walioteuliwa na mtangulizi wake? Maajabu haya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom