Njia nzuri ya kupata mafanikio

omben99

New Member
Jul 24, 2021
1
0
Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya na ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya pia ukitenda mazuri leo kesho yako hakika itakuwa nzuri yakupendeza na yenye kufurahisha kwa kila mwenye macho na maskio.

Hivyo basi okoa kesho yako leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa upendo,ushirikiano,imani na upendo kwa watu wote bila kujali hadhi, umri, kipato, rangi au kabila la mtu.Mungu ataleta mvua, jua na kuimarisha ustawi wa mazao yako.

Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, hata vitabu vya dini vinasema… MTU HUSIFIWA KWASABABU YA KINYWA CHAKE, LAKINI MTU ALIYE NA MOYO ULIOPOTOKA ATATENDEWA KWA DHARAU. Dumisha uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako,maendeleo yako naya wenzako, endelea kuwa mfano bora kwa watoto wako na jamii nzima inayokuzunguka, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.

Katika Maisha yetu ya kila siku tunahitaji mtu mmoja tuu wa kutuvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine lakini ni vigumi kujua mtu huyo ninani na yupo wapi.. hivyo basi, kuishi vizuri na watu ndio silaha ya kumpata mtu huyo, wakati mwingine baadhi ya watu huonekana kero na mzigo mzito katika Maisha yako lakini huwezi jua pengine huyo ndio yule mtu mmoja unaye mtafuta muda wote.

Muigizaji maarufu wa filamu kutoka nchini china JACKIE CHAN amewai kusema “mafanikio huja pale tu unapoacha kujali kipi watu wanaona juu yako na kujali kipi unaona juu yao…”na ukifanikiwa bas siku zote usiwe na dharau bali jitahidi kuwasidia nao wafikie malengo kama yako iwe ni mali na utajiri,elimu,nyazifa za uongozi,kazi,biashara hata katika Imani.

Hivyo ishi vizuri maisha yako,penda watu na ndugu zako,heshimu wakubwa kwa wadogo,ifikiri kesho yako na kuwa na hofu ya mwenyenzi mungu.
 
Back
Top Bottom