Njia Nne Za Uhakika Za Kufikia Utajiri, Angalizo: Ajira Sio Mojawapo

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,070
Fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Hii ni kwa sababu fedha ndio inatuwezesha kupata mahitaji yote ya msingi kwenye maisha. Hivyo ili kuwa na maisha bora ni muhimu sana kuwa na fedha za kutosha.

Kwa kifupi inabidi uwe na fedha za kukutosheleza au kwa kutumia neno rahisi ni muhimu wewe kuwa tajiri. Au kama hupendi kutumia neno tajiri kwa kufikiri sio neno zuri basi ni muhimu wewe kuwa na uhuru wa kifedha.
Utakuwa na uhuru wa kifedha pale ambapo fedha inakuwa sio hofu tena kwako. Na ili kuweza kufikia hatua hii kuna njia ambazo ni muhimu kupitia.

Leo tutajadili njia nne za uhakika za kufikia utajiri na jinsi unavyoweza kuzitumia. Kwa bahati mbaya sana katika njia hizi ile ambayo inapendwa na watu wengi haipo. Njia hiyo inayopendwa na watu wengi na ambayo haiwezi kukufikisha kwenye uhuru wa kifedha au utajiri ni ajira. Baadae tutaona ni kwa nini ni vigumu sana kufikia uhuru wa kifedha kupitia ajira.


Zifuatazo ni njia nne za uhakika za kufikia utajiri;

1. Biashara.

Hii ni njia ya kwanza ya uhakika ya kufikia uhuru wa kifedha. Katika biashara unaweza kutengeneza au kutafuta soko la bidhaa, huduma au hata mawazo yanayoweza kuboresha kitu. Biashara inakuwezesha wewe kutumia nyenzo ya muda wa watu wengine, fedha za watu wengine na hata utaalamu wa watu wengine kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Aina ya biashara tunayozungumzia hapa ni biashara kubwa ambayo haikuhitaji wewe kila mara ndio iweze kwenda vizuri.

Kama bado hujaingia kwenye biashara anza sasa mchakato wa kuangalia ni biashara gani unayoweza kufanya. Kabla hujaingia kwenye biashara yoyote hakikisha ina uwezo wa kukua na kuendeshwa bila ya wewe kuwepo moja kwa moja.

2. Uwekezaji

Hii ni njia nyingine muhimu ya kuweza kujitengenezea kiasi kikubwa cha fedha na hivyo kufikia uhuru wa kifedha. Katika uwekezaji unaweza kuwekeza fedha zako katika hisa, vipande na hata mifumo mingine ya uwekezaji wa fedha. Uzuri wa uwekezaji ni kwamba wewe unawekeza tu fedha zako na kuwa mfuatiliaji, huhitaji kufanya kazi moja kwa moja, bali fedha yako ndio inakufanyia kazi.

Kila mtu anaweza kuwa muwekezaji mzuri kama atapata elimu husika juu ya uwekezaji. Kama hujui uanzie wapi tembelea UWEKEZAJI TANZANIA ili uweze kujifunza mambo muhimu kuhusu uwekezaji.

Kuona nguvu ya uwekezaji kwa kuanza na kiasi kidogo soma; Hivi ndivyo unavyoweza kutajirika kwa kuanza na shilingi elfu moja.


3. Umiliki wa mali.

Njia nyingine unayoweza kuitumia kufikia utajiri ni umiliki wa mali. Unaweza kununua ardhi na kukaa nayo na jinsi siku zinavyokwenda thamani yake inaongezeka. Pia unaweza kujenga nyumba kwa ajili ya biashara yaani kuuza au kupangisha. Kwa njia hizi unatumia mali unazomiliki kutengeneza fedha zaidi.

4. Intaneti.


Najua unaweza kushangaa intaneti inawezaje kukufanya wewe kuwa tajiri. Ukweli ni kwamba intaneti imetengeneza matajiri wengi sana na hata wewe unaweza kuwa mmoja wao. Intaneti ina njia nyingi sana unazoweza kuzitumia kutengeneza fedha. Unaweza kutangaza biashara zako mwenyewe, unaweza kuanzisha blog au website yenye kutoa taarifa muhimu na kutengeneza wafuasi ambao unaweza kuwatangazia biashara za watu wengine na ukalipwa fedha nyingi.

Uzuri wa intaneti hasa huku kwenye nchi zetu za kiafrika bado ni changa sana na hivyo kuna nafasi kubwa ya kuweza kunufaika. Na pia intaneti ni nzuri sana kwa sababu mtu yeyote mwenye juhudi na maarifa hata kama hana mtaji kabisa anaweza kuanza kutengeneza fedha kupitia intaneti.

Hata wewe unaweza kuanza safari yako ya utajiri kwa kutumia intanet. Kujua pa kuanzia pata kitabu JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Ni kitabu ambacho kitakupatia misingi mizuri ya kuweza kufanya biashara kwa kutumia intaneti. Kitabu kipo kwenye soft copy na kinatumwa kwa email. Kukipata tuma fedha tsh elfu kumi kwenye namba 0717396253 / 0755953887 na kisha tuma email yako halafu utatumiwa kitabu hicho.

Angalizo muhimu kwa njia hizi nne;

Sio kwamba ukishaingia tu kwenye moja ya njia hizi nne basi tayari wewe ni tajiri. Unahitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa na pia unahitaji uvumilivu mkubwa kwa sababu changamoto ni nyingi sana na zinaweza kukukatisha tamaa.

Pia jinsi unavyoanza mapema ndio unavyojiwekea nafasi nzuri ya kufikia utajiri mapema. Mtu anayeanza biashara au uwekezaji akiwa na miaka 30 ni tofauti kabisa na mtu anayeanza akiwa na miaka 40 au 50. Jitahidi uanze sasa bila ya kujali umri ulionao.

Muhimu zaidi ni kwamba unaweza kuzitumia njia zote. Sio kwamba ukishatumia njia moja basi nyingine huruhusiwi, hapana, unaweza kutumia zote unavyotaka mwenyewe. Kwa mfano unaweza kuwa na biashara ambayo pia umeiweka kwenye mtandao na faida unayopata kwenye biashara zako unaiwekeza kwenye biashara hiyo na kwenye aina nyingine za uwekezaji na pia unanunua mali zaidi.

Kwa nini ajira haiwezi kukufikisha kwenye utajiri?

Naamini mpaka sasa utakuwa umeshajua kwa nini ajira haiwezi kukufikisha kwenye utajiri. Kama bado hujajua sababu ni kwamba kwenye ajira kipato chako kinaamuliwa na watu wengine. Hata ukifanya kazi kwa juhudi na maarifa kiasi gani bado kipato chako huwezi kuamua mwenyewe.

Sababu nyingine inayofanya ajira isiweze kukufikisha kwenye utajiri ni kwamba kwenye ajira unatumia muda wako tu ili kupata fedha. Wakati kwenye biashara na uwekezaji mwingine unaweza kutumia muda wa watu wengine kujizalishia wewe fedha. Jinsi unavyoweza kuwatumia watu wengi zaidi kukuzalishia ndivyo unavyoweza kufikia utajiri mapema.

CHUKUA HATUA.

Chagua leo ni njia ipi utakayoanza kuifanyia kazi ili uweze kufikia uhuru wa kifedha. Maamuzi unayafanya leo na kuanza kuyatekeleza, usingoje tena mpaka mambo yawe vizuri kwa sababu nakuhakikishia hayatakuwa vizuri. Na pia kumbuka kwamba jinsi unavyoanza mapema ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kufikia mafanikio. Anza leo kwa kupata kitabu kinachoelezea kuhusu biashara kwa njia ya intaneti na anza kujifunza.

Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia utajiri na uhuru wa kifedha.

TUPO PAMOJA.


Kwa ufafanuzi na uchambuzi zaidi kwenye njia hizo nne za kufikia utajiri na wapi pa kuanzia tuma email kwenda ushauri@kisimachamaarifa.co.tz
 
Ujumbe mzuri sana. Hakika tutaufanyia kazi, hata hivyo "uhuru wa kifedha" unaleta maana nzuri zaidi ya "utajiri" coz sio wote wenye ndoto za kuwa 'matajiri' bali wanahitaji kuwa huru kifedha.
 
Ahsante kwa bandiko, hata hivyo mkuu bandiko linakua jepesi usipoweka Elimu, Elimu inakupa Maarifa inasimama nyuma ya hivyo vi4 ulivyovitaja, though sometime inaweza simama independent, unless concept ya kuwa na fedha/utajiri ni static, ila kama ni relatively, kuna watu they are rich because they have education, hujaitendea haki Elimu...
 
njia za kuweza kukupa kipato kikubwa, zipo nyingi mno, ajira yenye mshahara mkubwa ni njia moja rahisi na isiyo na risk sana kufikia utajiri,ilq kqma ilivyoelezwa hapo juu elimu ina nafasi kubwa kwenye eneo hili,pia sababu nyingine ambayo ni kwa nafasi ndogo mno ni ile ya kuzaliwa kwenye familia tajiri,unabii pia siku hizi umekuwa biashara inayolipa sana tu,kama una sauti kubwa na blah blah mingi fungua kanisa!! kanisa halimtupi nabii wake.
 
njia za kuweza kukupa kipato kikubwa, zipo nyingi mno, ajira yenye mshahara mkubwa ni njia moja rahisi na isiyo na risk sana kufikia utajiri,ilq kqma ilivyoelezwa hapo juu elimu ina nafasi kubwa kwenye eneo hili,pia sababu nyingine ambayo ni kwa nafasi ndogo mno ni ile ya kuzaliwa kwenye familia tajiri,unabii pia siku hizi umekuwa biashara inayolipa sana tu,kama una sauti kubwa na blah blah mingi fungua kanisa!! kanisa halimtupi nabii wake.

Mark my words, sijasema njia za kukupa kipato kikubwa nimesema njia za kukupa uhuru wa kifedha.
Nakubaliana na wewe kwamba kuna ajira zenye kipato kikubwa sana. Kwa mfano tuseme mtu analipwa milioni kumi kwa mwezi, ikitokea leo amefukuzwa kazi au kastaafu au hawezi tena kuendelea na kazi yake anaweza kusurvive miaka mingapi kwa maisha hayo anayoishi sasa? Huu ndio tunaozungumzia hapa, uhuru wa kifedha, hata usipofanya kazi moja kwa moja bado una njia zinazokuzalishia.
 
hakuna lolote njia ni moja tu piga kazi na tunza hela yako fulk stop acha hizo propaganda za watu wanaouza vitabu vya kuwa tajiri huku wenyewe wakiwa maskini
 
asante sana mkuu nitafanyia kazi mawazo yako.... sema tukumbushane na ufalme wa mbinguni udumuo milele nao unatafutwa kwa juhud hvo hvo,so next time tupia hata mbili sio lazma nne ka hzo itakuwa imekaa vema pia,thanks in advance!!
 
Bila hekima na maarifa ya MOLA haiwezekani kudumu katika utajiri.
Elimu ya chanzo cha mapato ni ufunguo wa kufanikiwa.
 
Mark my words, sijasema njia za kukupa kipato kikubwa nimesema njia za kukupa uhuru wa kifedha.
Nakubaliana na wewe kwamba kuna ajira zenye kipato kikubwa sana. Kwa mfano tuseme mtu analipwa milioni kumi kwa mwezi, ikitokea leo amefukuzwa kazi au kastaafu au hawezi tena kuendelea na kazi yake anaweza kusurvive miaka mingapi kwa maisha hayo anayoishi sasa? Huu ndio tunaozungumzia hapa, uhuru wa kifedha, hata usipofanya kazi moja kwa moja bado una njia zinazokuzalishia.

Hii Ya Kwako Ni Oversimplification Na Generalization Iliyopitiliza,those Who Know How To Get Rich Are Buzy Making Themselves Rich,not Preach How To Be Rich.
 
Hii Ya Kwako Ni Oversimplification Na Generalization Iliyopitiliza,those Who Know How To Get Rich Are Buzy Making Themselves Rich,not Preach How To Be Rich.

Wewe naye mbumbumbu kumbe hujui lolote... Hebu Google uone matajiri wa dunia wanavyopreach kuhusu unavyoweza kufanya na ukawa tajiri kama anavyozungumzia mtoa mada... Warren Buffet,Bill Gates, wote wanatoa sana hayo mafundisho na a lot more inspirational speech... Watu mnaelimishwa mnaleta kujua wkat hamna mnachojua..
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom