Jinsi ya kuandika Tangazo lako la biashara mtandaoni

Long plan ahead 6months up to 2 yrs ya mwanzoni atleast kuanza kupata effectively kile unachotaka bila kusahau low expectaction,nimeona lots of startups zikifa coz ya high expectation
Upo sahihi mkuu.

Ukiweza tamaa mbele online huwezi kufika mbali hata kidogo.

Utakata tamaa mapema sana.
 
Mkubwa nakusalimia, na hongera kufungua uzi huu tuongee kwa dakika chache.

mbinu za kuwajua wateja wa biashara yako.png

Kama mfanya Biashara kuna mambo huwa unafanya tu lengo kuu likiwa ni kuuza bidhaa au huduma yako. Siyo mbaya, ni vizuri.

Lakini, ulishawahi kujiuliza bidhaa yako watumiaji wake ni watu gani haswa?

Au tuanzie kwanza kwenye uelewa wako kuhusu bidhaa au huduma unayotoa.

Ni kwa kiwango gani unaielewa biashara yako? Unafahamu ni kwa kiwango gani biashara yako inatatua matatizo ya watu?

Hiyo siyo mada ya leo, ila chukua kama homework katika kutafakari.

Njoo kwenye kipengele cha watu unao walenga katika biashara yako.

Mkubwa, hawa watu unawafahamu kweli? Au unafanya matangazo kwa kila mtu halafu unajisemea moyoni, yeyote atakayekuja ni sawa tu.

Sasa ebu jaribu kukaa kisha jiulize maswalli haya yatakusaidia kupunguza kazi kubwa unayoifanya bila matokeo mazuri kwenye biashara yako mtandaoni na nje ya mtandao.

1. Hivi wateja wangu ni watu walio na umri wa kuanzia miaka mingapi hadi ngapi?

2. Wateja wangu watakuwa wanaishi wapi haswa? Nchi gani? Mkoa gani? Jiji gani?

4. Hali ya kiuchumi ya wateja wangu iko vipi? Ni wale wenye vibunda au wa hali ya kawaida?

5. Hawa wateja wangu ni changamoto gani haswa wanapitia katika maisha yao ya kila siku?

6. Wateja wangu ni watu wanaopenda vitu vya aina gani? Je, ni kundi la vijana wanaopenda mambo ya kula tunda kimasihara au ni watu ambao mambo hayo hawana time nayo?

7. Hawa watu wangu ni mambo gani yana wapa hamasa katika maisha?

Sasa tafuta sehemu tulivu ukiwa peke yako na kalamu na karatasi kisha anza kujibu hayo maswali taratibu.

Ukishamaliza na kupata majibu basi tumia majibu hayo kama MUONGOZO MKUU katika kufanya biashara na matangazo yako mtandaoni na hata mtaani.

Ni hayo tu mkubwa, unaweza kuendelea na safari ya kuperuzi JF, ila hakikisha unafanya jambo la tofauti kwenye biashara.

Mr. Purpose: 0752026992
 
Mkuu kwema?

Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa Elimu kuhusu matumizi ya mitandao katika kuanzisha na kukuza biashara au brands.

Weka swali lolote kuhusu Digital marketing na nitakupa Ufafanuzi kadiri ya uelewa wangu hapa.

Nina uzoefu wa miaka minne naelekea wa 5 (2023) kwenye ulimwengu wa kujifunza, kufundisha na kufanya biashara mtandaoni.

Twende kazi.
 
Una faida ya wazi inayoonekana Kwa macho na nyama kupitia Digital marketing?. Naamini swali limeeleweka sitegemei maneno mengi bila ushahidi wa jinsi ulivyofaidika na mada Yako mkuu
 
1. Naendesha maisha yangu kupitia ujuzi wa Digital Marketing kwa kuuza ujuzi na digital products.

2. Nimeweza kutengeneza connection na watu ambao kama nisingekuwa na uelewa wa matumizi sahihi ya mtandao pengine ingenichukua muda mrefu San kufahamiana nao.

3. Sijawahi tumia vyeti vyangu kuomba Ajira popote tangu nimejifunza digital Marketing badala yake nashirikiana na makampuni katika kufanya kazi.

Karibu kwa swali tena mkuu.
 
Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa Elimu kuhusu matumizi ya mitandao katika kuanzisha na kukuza biashara au brands.

Weka swali lolote kuhusu Digital marketing na nitakupa Ufafanuzi kadiri ya uelewa wangu hapa.

Nilitegemea utatoa hiyo elimu kupitia swali langu lakini badala yake umejibu majibu marahisi ambayo hayana uzani sawa na utambulisho wako mkuu.
 
Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa Elimu kuhusu matumizi ya mitandao katika kuanzisha na kukuza biashara au brands...
Kuuliza swali ukiwa na majibu yako kichwani siyo njia nzuri ya kujifunza.

Swali lako halikutaka Maelezo mengi na mwenyewe umekiri hilo.

Karibu kwa swali lingine.
 
Kuuliza swali ukiwa na majibu yako kichwani siyo njia nzuri ya kujifunza...
Nia ya Uzi ni kutatua changamoto ya upatikanaji wa Elimu kuhusu matumizi ya mitandao katika kuanzisha na kukuza biashara au brands.

Sioni wapi umetatua changamoto,vipi kukuza biashara kupitia Digital marketing?
 
Weka swali lolote kuhusu Digital marketing na nitakupa Ufafanuzi kadiri ya uelewa wangu hapa.
  1. Ni nini maana ya digital marketing na kwa nini ni muhimu katika biashara ?
    -Chukulia muuliza swali ni mklima, na hajui chochote zaidi ya kusikia sikia kwa watu.

  2. Je! Ni njia gani za kawaida za digital marketing na ni ipi inafaa kwa biashara ya matunda na mboga mboga?
    - Hapa chukulia muuliza swali ni mfanya biashara mdogo wa matunda na mboga mboga katika soko ilala, mkoani Dar.

  3. Je! Kuna changamoto gani za digital marketing na jinsi ya kuzitatua?
==
My take
- Uzi ni mzuri, tuendelee kupeana elimu,
 
Mkuu unaweza ukaongeza nyama kidogo bila shaka hizi ndio angle zako
 
  1. Ni nini maana ya digital marketing na kwa nini ni muhimu katika biashara ?
    -Chukulia muuliza swali ni mklima, na hajui chochote zaidi ya kusikia sikia kwa watu.

  2. Je! Ni njia gani za kawaida za digital marketing na ni ipi inafaa kwa biashara ya matunda na mboga mboga?
    - Hapa chukulia muuliza swali ni mfanya biashara mdogo wa matunda na mboga mboga katika soko ilala, mkoani Dar.

  3. Je! Kuna changamoto gani za digital marketing na jinsi ya kuzitatua?
==
My take
- Uzi ni mzuri, tuendelee kupeana elimu,
Shukrani kwa maswali mazuri. Naomba kujibu kama ifuatavyo:-

SWALI LA 1.

Ni nini maana ya digital marketing na kwa nini ni muhimu katika biashara ?
-Chukulia muuliza swali ni mklima, na hajui chochote zaidi ya kusikia sikia kwa watu.

MAJIBU:

Kwanza kiswahili cha neno Digital Marketing ni Utafutaji wa Masoko kwa njia ya kidigitali (mtandao).

Hivyo Digital Marketing ni ile hali ya kutumia majukwaa mbalimbali ya mtandaoni kutafuta masoko.

Na majukwaa haya yanaweza kuwa mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Jamii Forums, Twitter na aina nyingine ya mitandao ya kijamii na pia matumizi ya Tovuti (Websites).

Faida za Digital Marketing:

A. Ni njia rahisi ya kufikia wateja wengi kwa gharama ndogo.

B. Ni njia rahisi ya kujenga brand (Jina lako au biashara yako) na kujenga uaminifu mkubwa kwa wateja.

C. Ni njia rahisi ya kutambulisha biashara yako na kufahamika na wengi.

D. Inaongeza mauzo zaidi katika biashara yako ukilinganisha na kukaa tu hapo sokoni ukitegemea wateja wa hapo tu.

E. Inarahisisha ukuaji wa biashara yako.

SWALI LA 2:

Je! Ni njia gani za kawaida za digital marketing na ni ipi inafaa kwa biashara ya matunda na mboga mboga?
- Hapa chukulia muuliza swali ni mfanya biashara mdogo wa matunda na mboga mboga katika soko ilala, mkoani Dar.

MAJIBU.

Moja kati ya kitu muhimu sana kwa mteja linapokuja kwenye kufanikisha biashara Yake mtandaoni ni kufahamu kundi la wateja anao walenga.

Hapa ni kuanzia kipato, umri, sehemu walipo wateja anao walenga, Jinsia, Kiwango cha Elimu, Changamoto zao na Vitu ambavyo wanapendelea zaidi.

Kwa mfanya biashara mdogo wa matunda na mboga mboga pale Soko la Ilala mkoa wa Dar-es-Salaam anaweza kutumia njia ifuatayo kufikia wateja wengi mtandaoni:

Huyu anapaswa kutumia mitandao ya kijamii tu.

Kwasababu haina gharama kubwa na pia ni rahisi kwake yeye kuisimamia baada ya kueleweshwa vitu vichache kama vile, Jinsi Ya kupost picha za bidhaa yake, wakati gani apost, post zake azipangilie katika utaratibu gani mzuri ili kuepuka kuwachosha wafuasi wake, na namna nzuri ya kupangilia ukurusa wake (settings nzuri za Bio & Profile).

Mitandao ya kijamii ambayo inaweza kumfaa ni kama vile WhatsApp, Instagram, Twitter na Facebook.

Ambayo atapendelea yeye kutegemeana na aina ya watu anao walenga basi ataitumia.

Na wakati wa kuanza ni muhimu kuchagua mtandao mmoja kwanza kisha unaweza kuongeza mtandao mwingine hii ni kwasababu ukitumia mitandao mingi mwanzoni itakuwa ngumu kwako kuzikuza na kuzisimamia inavyotakiwa.

Pia anaweza kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram (Hapa anapaswa kupata muongozo ili kukamilisha vizuri). Ina matokeo mazuri sana ukiandaliwa tangazo na mwenye uzoefu.

SWALI LA 3.

Je! Kuna changamoto gani za digital marketing na jinsi ya kuzitatua?

Changamoto zipo, pamoja na kwamba faida ni nyingi.

A. Inahitaji kuwa na ujuzi wa kidigitali katika kuendesha na kusimamia majukwaa yako ya biashara mtandaoni.

Hapa kuna kufahamu jinsi ya kusoma data za matokeo ya ukurasa wako ili kufahamu mwenendo wa ukuaji wako mtandaoni.

Wapo watu wanaoweza kukufundisha na ukaepukana na changamoto hii.

B. Uaminifu hasa mwanzoni unapoanza.

Unahitaji kuwa mvumilivu mwanzoni kwasababu ndiyo muda wa kuonyesha unachokifanya na wakati huo hupati wateja kwasababu bado wana kusoma kwanza ili kukufahamu ndipo waanze kuja kununua.

Hatua hii inabidi uwe mvumilivu, weka picha zako ukiwa na wateja wako, weka picha kuonyesha ukiwa na bidhaa zako unazipanga.

Na pia weka shuhuda za wateja ambao umewahudumia.

Hizo njia zitakusaidia kujenga uaminifu mtandaoni hivyo kumuondolea mteja wasiwasi wa kutapeliwa.

C. Inahitaji uvumilivu mwanzoni unapoanza.

Digital marketing ni njia nzuri ila siyo rahisi mwanzoni unapoanza.

Ili kuitambulisha biashara yako mtandaoni mwanzoni Utahitaji kuwa na mpango mkakati mzuri na kufanya kazi kubwa ya kutekeleza.

Inaweza kuchukua kuanzia miezi mitatu kuanza kupata matokeo mazuri ila tu kama utakuwa unapost mara kwa mara katika akaunti yako.

Karibu kwa maswali zaidi kama kuna kipengele hakijaeleweka.
 
Hizo njia zitakusaidia kujenga uaminifu mtandaoni hivyo kumuondolea mteja wasiwasi wa kutapeliwa
hapa kuna swali la msingi linajitokeza.
Ni njia gani za kuepuka udanganyifu mtandaoni katika digital marketing?
 
Digital marketing huijui ndugu ulichoongelea hakisawiri hasa kuhusu Digital marketing nivyema ukaeleza part unayoielewe kuhusu digital marketing kuliko kuzungumzia kipande kimajumui Kama dhana ya digital marketing
 
Kabla ya kununua bidhaa kwa mtu hakikisha umemfuatilia kwanza na kufahamu ofisi ilipo, akutumie sample ya kazi zake au bidhaa, akupe shuhuda za watu aliowahudumia ikiwezekana akupe namba ya simu uwapigie kuuliza.

Angalia mpangilio wa kurasa na post zake utagundua kama ni mtu yupo serious au ni janja janja.

Kama yupo sehemu mkoa ambao mnaweza kukutana basi kutana naye na mfanye biashara.

Kama upo mbali basi tafuta mtu aliye karibu ambaye anaweza kuonana naye.

Hizo ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kuepuka udanganyifu na kutapeliwa.

Ingawa kwasasa watu wamekuwa wajanja sana katika kutapeli hivyo siyo njia zote zitaweza kutumika katika kila biashara na badala yake unapaswa kuwa makini sana unapo nunua chochote mtandaoni.
 
Digital marketing huijui ndugu ulichoongelea hakisawiri hasa kuhusu Digital marketing nivyema ukaeleza part unayoielewe kuhusu digital marketing kuliko kuzungumzia kipande kimajumui Kama dhana ya digital marketing
Ni mjadala, hivyo unaweza kuongezea pale penye mapungufu.

Tupo kujifunza na siyo kuonyesha nani anajua au nani hajui.
 
Digital marketing huijui ndugu ulichoongelea hakisawiri hasa kuhusu Digital marketing nivyema ukaeleza part unayoielewe kuhusu digital marketing kuliko kuzungumzia kipande kimajumui Kama dhana ya digital marketing
What is your input in the context and purpose of this thread? Please share your thoughts.
 
Baadhi ya wafanya biashara huwa wanadhani ukianza kutumia mtandao Kutangaza Biashara yako basi utapata wateja kwa haraka.

Kitu ambacho wengi hawakielewi ni kwamba, jinsi ambavyo maisha ya kawaida mtaani yalivyo, hakuna kinachopatikana kiurahisi.

Kutangaza Biashara au Kipaji Mtandaoni Unahitaji:-

1. Mpango mkakati ulio imara na wa kueleweka.

2. Utayari wa kuwa mwanafunzi. Yaani ukubali kujifunza na kufundishwa.

3. Uvumilivu. Ondoa mategemeo ya kupata wateja kwa haraka.

4. Kujituma na kujitoa kwa hali na mali.

6. Kuwa na mbinu bora za kivita. Muhimu tu usifanye vitu vya ajabu mtandaoni ili kupata attention.

Jifunze techniques zinazoendana na malengo yako.

Ongezea zingine kwenye comment.

View attachment 2545867
 
Back
Top Bottom