Njia ngumu kuelekea mfumo wa vyama vingi

PERECY

Member
Jan 11, 2012
29
0
Naamini kuna watu wengi sana wanahitaji mabadiliko ya kisiasa. Kuna watu wengi sana wameichoka CCM, walijenga matumaini kwa NCCR Mageuzi, wakati fulani wakakata tamaa. Wakajenga kwa CUF, TLP na baadaye CDM; lakini matumaini yanafifia kwa kasi kubwa.

Wenye historia nzuri wanakumbuka Tanzania ilipokea mfumo wa vyama vingi miaka ya mwanzoni mwa 1990. Nakumbuka orodha ya vyama vingi wakati huo vilisajiliwa vingi sana, wakiwepo akina James Mapalala. Nilikuwa darasa la 4, sikuwa nafahamu vizuri mfumo mzima kwa utaratibu mzuri.

Mwaka 1995 nikiwa kidato cha pili pale Tumaini sekondari - Kinampanda, Iramba-Singida, nakumbuka kushiriki kusukuma gari ya Mh. Lyatonga Mrema, akiwa NCCR Mageuzi katika kampeni za urais, kwenye mkutano uliofanyika Kinampanda. Nilikuwa nimejaa mhemko mkubwa kwamba sasa Tanzania inapata rais kutoka chama cha upinzani Mh. Mrema. Ajabu, matokeo yalijaa vituko vitupu. Matumaini ya watanzania waliotegemea mabadiliko kupitia NCCR Mageuzi yalififia. NCCR ilijaa migogoro mitupu, mpaka mwishoni tukasikia chama kimesambaratika kwenye kikao cha Hoteli ya Mkonge kule Tanga.

CUF na CDM ni vyama vya siasa imara (vya upinzani) ambavyo na vyenyewe vimekubwa na migogoro inayoelekea kuwaacha wapenzi wake midomo wazi. Mbinu chafu kila uchao zinavidhoofisha vyama hivi. Njia ngumu kuelekea mfumo wa vyama vingi Tanzania!

Kuna dhahania (assumption) sijui ni ya mtaani au laa, kwamb Tanzania ilikubali kuufuata mfumo wa vyama vingi kuyaridhisha mashirika makubwa ya kimataifa ambayo ni wafadhili wa bajeti za maendeleo za nchi yetu. Ili kuweka 'ulaji' sawa, wakachukuliwa makada maarufu wa CCM na kupewa nguvu ya kuanzisha vyama vya siasa vya upinzani, akina Mrema, Lamwai, Marando, Mbatia, n.k; ambavyo mara nyingi vimeonekana kufa inapoelekea uchaguzi wa kitaifa unaohusu uongozi wa vyama husika au uongozi wa serikali. Kama hivi ndivyo ilivyokuwa, sijui, lakini mazingira yanaonyesha baadhi ya makada wa CCM waliopewa fursa ya kuanzisha vyama hivi labda walipata akili, na kuona inawezekana kuwa wapinzani rasmi, jambo ambalo limeonyesha kwenda kinyume na matakwa ya upinzani wa kweli; tunabaki kuumizwa.

Kwa kuwa inaosewa kuwa kuna jitihada kubwa sana za CCM kuviangamiza vyama vya upinzani kwa propaganda chafu (kama ukabila, dini, ukanda, visu, ugaidi, kupandikiza mamluki katika nafasi za uongozi, n.k.);

Kwa kuwa wananchi kwa dhati kabisa wapo wanaoatafuta mabadiliko ya kweli ya mfumo wa kisiasa, na wameanza muda mrefu kuonyesha nia yao hiyo, lakini hujikuta wameduwazwa na mfumo wa upigaji kura na matokeo kwa ujumla;

Kwa kuwa kuna mambo mengi sana ya msingi ambayo serikali imeshindwa kuyasimamia kupitia viongozi wake wenye dhamana kubwa, katika wizara, idara na taasisis mabalimbali za serikali;

Kwa kuwa imeendelea kuonekana kwamba katika vyama vya siasa vya upinzani mamluki wa kubadilisha mwelekeo wa matumaini ya wananchi umetandaa na unatenda kazi yake vizuri hali inayaowakanganya wananchi kwa namna mbaya sana;

Maono yangu:

1. Wananchi wengi sana waliotegemea mabadiliko na inaonekana yanakwamishwa kwa makusudi, wengi watajichukulia sheria mikononi dhidi ya viongozi na taasisi zake; kutokana na matukioa mabaya ambayo CCM wanayasimamia hasa katika rasilimali za taifa (gesi, mafuta, madini, maliasili, na mashamba makubwa ambayo wamepewa wawekezaji), na ulipizaji wa kisasi wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, kuhusu Kampeni ya Operesheni Tokomeza Ujangili.

2. Viongozi wengi wanaotoka katika chama fulani cha siasa na kwenda chama kingine (iwe toka CCM, CDM, CUF, TLP, n.k na kwenda kwa chama kingine), watakutana na hatari kubwa ya kuuwa, kutekwa, kuchomewa mali zao, na matukio mabaya yatakowaondoa katika sifa walizozipata wakati wanaonyesha jitihada za mabadiliko wakiwa na vyama vyao. Kwa sababu imeonyesha hawana nia nzuri zaidi ya kuhangaika na sifa zao binafsi wakitumia siasa kuhongwa/kuhonga, n.k.

3. Katika CDM, mgawanyiko kuongezeka, lakini Zitto Kabwe na Mwigamba (na wafuasi wao) kujikuta katika hatari kubwa sana ya kupatwa na mabaya hasa kama wataamua na wataendelea na 'kile wanachokiita kujitetea mbele ya umma', au kuanzisha chama kipya cha upinzani, au kwenda kwenye chama chochote cha siasa kwa lengo la kupata uongozi na kuongea mabaya ya CDM.

4. Zitto kutokubalika sehemu nyingi za nchi (na kuonekana msaliti mkubwa) zaidi ya Kigoma (nyumbani kwake) na Katavi/Mpanda/Sumbawanga ambako kuna namna inaonekana anaungwa mkono na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CDM Bara, Mh. Said Arfi.

Hitimisho
Kwa kuwa kwa mwendo huu imeonekana NI NJIA NGUMU KUELEKEA MFUMO WA VYAMA VINGI, mtu yeyote atakayeanzisha chama chochote cha siasa, anapaswa kuwa na akili ya mwendawazimu. Hadi sasa waTanzania wamejeruhiwa vibaya sana kisaikolojia na mfumo wa siasa ambao unaonekana kukipendelea CCM katika namna zote. Msajili wa Vyama vya Siasa ni chaguo la Rais wa JMT, ambaye ni M/kiti wa CCM taifa chama kinachoongoza serikali. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, ni chaguo la rais kama hapo juu. Viongozi wote waandamizi wa vyombo vya usalama wa taifa ni chaguo la rais kama hapo juu. Wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, n.k. ambao wanatekeleza matakwa na kile kinachitwa 'ILANI YA CCM'.

Ili chama cha siasa kushinda uchaguzi na mamlaka za serikali iliyoko madarakani inahitaji kwenda kufanyia mbinu zake za ukombozi nje ya nchi (kama inawezekana) wakati huo wakisaidiwa kwa misaada mingi na nchi rafiki wa chama chao. Ila kwa mwendo wa upuuzi huu tunaouona wa Zitto, Mwigamba na Kitila, na msaada wao unaounganishwa na back-up za baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali na CCM; ni dhahiri CDM, CUF, TLP, NCCR Mageuzi, n.k; wako kwenye njia ngumu kufikia Ikulu ya Magogoni, hasa 2015. Mshtuko mkubwa ukiongezeka CDM kwa kupoteza viti vya ubunge, udiwani, na nafasi za serikali ya mitaa kama hawatapata mbinu mpya ya kuwaita wanachama wapya, kuyaeleza vizuri maamuzi ya Kamati Kuu ya chama kwa wananchi na kuzikabili mbinu zinazoelekezwa kwake. Ni kazi ngumu inayohitaji rasilimali watu isiyo na hila, fedha, magari, na mfumo mzuri wa ulinzi!

Tusubiri tuone hatma ya haya!

Perecy Ugula,
Iringa, Tanzania.
 
chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,296
2,000
Usikate tamaa ndugu hakuna wa kudhoofisha CDM kwa matakwa yake yeye ila tu mapenzi ya Mungu
 
chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,296
2,000
Pia nikuweke sawa kuhusu Zitto na Arfi huku kwetu Sumbawanga na Katavi, hakuna anyetaka kumsikia Arfi mpanda mjini na yeye anajua ndio maana alitangaza mapema kutogombea CDM, Sumbawanga hakuna mtu wanayemwona kama mkombozi wao zaidi ya Dr. Slaa na Mbowe kutokana na hotuba zao za kutoa matumaini, ila huyo Zitto hawezi kuja kuwashawishi wananchi wa huku wakamwamini maana habari za vijiweni kwa vijana ni kwamba wanamchelewesha kumvua uanachama
 
m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
Mleta mada anasema CDM inahitaji watu,fedia,magari nk,mbona vitu hivyo vipo! watu(makamanda) tupo,fedha tunazo kwani tupo tayari kukichangia chama chetu,magari,pikipiki tunazo! hao mamluki watu wadogo sana na hawana ubavu wa kupambana na jeshi kubwa kama CDM.Kuhusu huyo ARFI hana jipya kama tumesikia majuzi tu huko kwao mpanda wanacdm wamemkataa kwenye kikao wakishinikiza aondolewe chamani kwa kuwasaliti nadhani huyo ameshajimaliza mwenyewe! CDM BADO INA NGUVU SANA NA NDILO TUMAINI PEKEE LA WANYONGE.
 
Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
Naamini kuna watu wengi sana wanahitaji mabadiliko ya kisiasa. Kuna watu wengi sana wameichoka CCM, walijenga matumaini kwa NCCR Mageuzi, wakati fulani wakakata tamaa. Wakajenga kwa CUF, TLP na baadaye CDM; lakini matumaini yanafifia kwa kasi kubwa.

Wenye historia nzuri wanakumbuka Tanzania ilipokea mfumo wa vyama vingi miaka ya mwanzoni mwa 1990. Nakumbuka orodha ya vyama vingi wakati huo vilisajiliwa vingi sana, wakiwepo akina James Mapalala. Nilikuwa darasa la 4, sikuwa nafahamu vizuri mfumo mzima kwa utaratibu mzuri.

Mwaka 1995 nikiwa kidato cha pili pale Tumaini sekondari - Kinampanda, Iramba-Singida, nakumbuka kushiriki kusukuma gari ya Mh. Lyatonga Mrema, akiwa NCCR Mageuzi katika kampeni za urais, kwenye mkutano uliofanyika Kinampanda. Nilikuwa nimejaa mhemko mkubwa kwamba sasa Tanzania inapata rais kutoka chama cha upinzani Mh. Mrema. Ajabu, matokeo yalijaa vituko vitupu. Matumaini ya watanzania waliotegemea mabadiliko kupitia NCCR Mageuzi yalififia. NCCR ilijaa migogoro mitupu, mpaka mwishoni tukasikia chama kimesambaratika kwenye kikao cha Hoteli ya Mkonge kule Tanga.

CUF na CDM ni vyama vya siasa imara (vya upinzani) ambavyo na vyenyewe vimekubwa na migogoro inayoelekea kuwaacha wapenzi wake midomo wazi. Mbinu chafu kila uchao zinavidhoofisha vyama hivi. Njia ngumu kuelekea mfumo wa vyama vingi Tanzania!

Kuna dhahania (assumption) sijui ni ya mtaani au laa, kwamb Tanzania ilikubali kuufuata mfumo wa vyama vingi kuyaridhisha mashirika makubwa ya kimataifa ambayo ni wafadhili wa bajeti za maendeleo za nchi yetu. Ili kuweka 'ulaji' sawa, wakachukuliwa makada maarufu wa CCM na kupewa nguvu ya kuanzisha vyama vya siasa vya upinzani, akina Mrema, Lamwai, Marando, Mbatia, n.k; ambavyo mara nyingi vimeonekana kufa inapoelekea uchaguzi wa kitaifa unaohusu uongozi wa vyama husika au uongozi wa serikali. Kama hivi ndivyo ilivyokuwa, sijui, lakini mazingira yanaonyesha baadhi ya makada wa CCM waliopewa fursa ya kuanzisha vyama hivi labda walipata akili, na kuona inawezekana kuwa wapinzani rasmi, jambo ambalo limeonyesha kwenda kinyume na matakwa ya upinzani wa kweli; tunabaki kuumizwa.

Kwa kuwa inaosewa kuwa kuna jitihada kubwa sana za CCM kuviangamiza vyama vya upinzani kwa propaganda chafu (kama ukabila, dini, ukanda, visu, ugaidi, kupandikiza mamluki katika nafasi za uongozi, n.k.);

Kwa kuwa wananchi kwa dhati kabisa wapo wanaoatafuta mabadiliko ya kweli ya mfumo wa kisiasa, na wameanza muda mrefu kuonyesha nia yao hiyo, lakini hujikuta wameduwazwa na mfumo wa upigaji kura na matokeo kwa ujumla;

Kwa kuwa kuna mambo mengi sana ya msingi ambayo serikali imeshindwa kuyasimamia kupitia viongozi wake wenye dhamana kubwa, katika wizara, idara na taasisis mabalimbali za serikali;

Kwa kuwa imeendelea kuonekana kwamba katika vyama vya siasa vya upinzani mamluki wa kubadilisha mwelekeo wa matumaini ya wananchi umetandaa na unatenda kazi yake vizuri hali inayaowakanganya wananchi kwa namna mbaya sana;

Maono yangu:

1. Wananchi wengi sana waliotegemea mabadiliko na inaonekana yanakwamishwa kwa makusudi, wengi watajichukulia sheria mikononi dhidi ya viongozi na taasisi zake; kutokana na matukioa mabaya ambayo CCM wanayasimamia hasa katika rasilimali za taifa (gesi, mafuta, madini, maliasili, na mashamba makubwa ambayo wamepewa wawekezaji), na ulipizaji wa kisasi wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, kuhusu Kampeni ya Operesheni Tokomeza Ujangili.

2. Viongozi wengi wanaotoka katika chama fulani cha siasa na kwenda chama kingine (iwe toka CCM, CDM, CUF, TLP, n.k na kwenda kwa chama kingine), watakutana na hatari kubwa ya kuuwa, kutekwa, kuchomewa mali zao, na matukio mabaya yatakowaondoa katika sifa walizozipata wakati wanaonyesha jitihada za mabadiliko wakiwa na vyama vyao. Kwa sababu imeonyesha hawana nia nzuri zaidi ya kuhangaika na sifa zao binafsi wakitumia siasa kuhongwa/kuhonga, n.k.

3. Katika CDM, mgawanyiko kuongezeka, lakini Zitto Kabwe na Mwigamba (na wafuasi wao) kujikuta katika hatari kubwa sana ya kupatwa na mabaya hasa kama wataamua na wataendelea na 'kile wanachokiita kujitetea mbele ya umma', au kuanzisha chama kipya cha upinzani, au kwenda kwenye chama chochote cha siasa kwa lengo la kupata uongozi na kuongea mabaya ya CDM.

4. Zitto kutokubalika sehemu nyingi za nchi (na kuonekana msaliti mkubwa) zaidi ya Kigoma (nyumbani kwake) na Katavi/Mpanda/Sumbawanga ambako kuna namna inaonekana anaungwa mkono na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CDM Bara, Mh. Said Arfi.

Hitimisho
Kwa kuwa kwa mwendo huu imeonekana NI NJIA NGUMU KUELEKEA MFUMO WA VYAMA VINGI, mtu yeyote atakayeanzisha chama chochote cha siasa, anapaswa kuwa na akili ya mwendawazimu. Hadi sasa waTanzania wamejeruhiwa vibaya sana kisaikolojia na mfumo wa siasa ambao unaonekana kukipendelea CCM katika namna zote. Msajili wa Vyama vya Siasa ni chaguo la Rais wa JMT, ambaye ni M/kiti wa CCM taifa chama kinachoongoza serikali. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, ni chaguo la rais kama hapo juu. Viongozi wote waandamizi wa vyombo vya usalama wa taifa ni chaguo la rais kama hapo juu. Wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, n.k. ambao wanatekeleza matakwa na kile kinachitwa 'ILANI YA CCM'.

Ili chama cha siasa kushinda uchaguzi na mamlaka za serikali iliyoko madarakani inahitaji kwenda kufanyia mbinu zake za ukombozi nje ya nchi (kama inawezekana) wakati huo wakisaidiwa kwa misaada mingi na nchi rafiki wa chama chao. Ila kwa mwendo wa upuuzi huu tunaouona wa Zitto, Mwigamba na Kitila, na msaada wao unaounganishwa na back-up za baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali na CCM; ni dhahiri CDM, CUF, TLP, NCCR Mageuzi, n.k; wako kwenye njia ngumu kufikia Ikulu ya Magogoni, hasa 2015. Mshtuko mkubwa ukiongezeka CDM kwa kupoteza viti vya ubunge, udiwani, na nafasi za serikali ya mitaa kama hawatapata mbinu mpya ya kuwaita wanachama wapya, kuyaeleza vizuri maamuzi ya Kamati Kuu ya chama kwa wananchi na kuzikabili mbinu zinazoelekezwa kwake. Ni kazi ngumu inayohitaji rasilimali watu isiyo na hila, fedha, magari, na mfumo mzuri wa ulinzi!

Tusubiri tuone hatma ya haya!

Perecy Ugula,
Iringa, Tanzania.
namba 3 na 4 sijakuelewa kabisa. unatumia vigezo gani kusema eti Zitto hakubaliki sehemu nyingi nchi nzima? a day dreamer ms/mr Zittophobiasis.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom