Njia na Mkakati Rahisi Zaidi Ili Kufuta Umasikini Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia na Mkakati Rahisi Zaidi Ili Kufuta Umasikini Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SolarPower, Jun 17, 2012.

 1. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania,

  Naomba kama Taifa na katika ngazi za familia zetu, Vijiji na Vitongoji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa tuwekeze sana katika VITABU ambavyo vinatupa ujuzi, Maarifa Zaidi na mbinu mbalimbali za uzalishaji mali na mbinu bora zaidi za kuboresha maisha yetu. Pendekezo langu ni kuwa kila familia iwekeze na kununua angalau kitabu kimoja cha namna hiyo kila mwezi na kukisoma kwa ukamilifu wake. Na pia serikali iwe na bajeti maalum ya kununua vitabu vya namna hiyo ka ajili ya watu wa nchini. Bajeti hii ya serikali kwa mwaka inapendekezwa isipungue shilingi bilioni 75 kila mwaka.
   
Loading...