Njia mojawapo ya namna CIA inavyoandaa Vijana ambao mwisho wa siku huja kuwa Majasusi mahiri

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,518
2,000
Haya ni maelezo ya aliyewahi kuwa mfanyakazi wa CIA, ndg. Brad Robinson, Muhitimu wa University of California ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mchunguzi binafsi(private investigator) katika Taasisi ya Millennium Group huko Marekani.

Brad anazungumzia mazingira ambayo CIA walim-recruit mpaka kujakuwa jasusi mahiri wa shirika hilo.

Anasema, ilikuwa ni katika mwaka wake wa mwisho wa masomo katika chuo kikuu cha California(UCLA) alipokuwa anachukua degree ya Mahusiano ya Kimataifa(International Relations).

Alipata barua kupitia mailbox yake kwamba Mr. Smith ambaye ni muwakilishi wa CIA alikuwa ametembelea mji ambao chuo kipo na atakaa kwa siku kadhaa katika hotel fulani katikati ya mji.

Kipande cha karatasi kwenye mailbox yake kilisema kama yeye Brat atakuwa interested, apige namba ya simu ambayo ilikuwa imeandikwa kwenye kile kipande cha katarasi ili kupanga ahadi ya kukutana na Mr. Smith kwa mahojiano zaidi.

Japo alikuwa na mashaka, alifanya kama maelezo ya kwenye karatasi yalivyomuelekeza.

Siku ya siku alienda kukutana na Mr. Smith na mahojiano yao hayakuzidi hata dakika kumi.

Kwa kuwa hakuwa na uzoefu mkubwa wa kufanyiwa interview, siku alipoenda kukutana na Mr. Smith hakujiandaa kimuonekano. Hakwenda saloon kunyoa ndevu/nywele, hakuvaa suruali, alivaa kaptula. Kwa ujumla dress code yake haikuwa ya kupendeza.

Alifanya hivyo kwa kuwa hakuupa kipaumbele mikutano wake na Mr. Smith. alienda tu kama sehemu ya kupotezea muda(kuzuga).

Wakati wa mahojiano aliulizwa maswali mepesi sana. Aliulizwa kuhusu uzoefu wake wa kuajiriwa ambapo alijibu kwa kutoa maelezo kuhusu kazi yake ya kuwa muhudumu wa bar(bartender), pia aliulizwa ni kitu gani hupendelea kukifanya katika muda wake wa mapumziko, alijibu kwamba yeye hupendelea kushiriki katika mbio za magari za mitaani ambazo haziruhusiwi kisheria(illegal street racing).

Baada ya maswali hayo machache, mr. Smith alinyanyuka kumshukuru na kuagana naye.

Brat anasema alijuwa dhahiri shairi kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wa yeye kuwasiliana tena CIA. Moja kwa moja alijiweka katika fungu la kukosa. kumbe haikuwa hivyo.

Baada ya kama mwezi mmoja hivi kupita, alipokea barua kupitia Washington DC postmark, barua hiyo ilikuwa haina anuani ya kuonyesha ilipotoka.

Katikati ya barua hiyo kulikuwa na maneno machache tu ya kumpongeza ya "excellent". haikuwa na meneno mengine zaidi ya hayo.

Mwisho wa barua hiyo kulikuwa na namba ya simu ambayo alitakuwa kuipiga ili apewe maelezo zaidi kuhusu ajira yake na CIA.

Brad anasema huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari yake ngumu, ndefu na yenye changamoto kadhaa iliyopelekea kupata nafasi ya kujiunga katika mafunzo maalumu ya ujasusi katika spy academy ya CIA.

Kitu ambacho Brat alijifunza katika zoezi zima la kum-recruit ni kwamba watu kama Mr. Smith ni majasusi wastaafu waliokwisha fanyakazi na CIA kwa muda mrefu. Wamepewa jukumu la kusaka vijana wenye vipaji maalumu katika vyuo mbalimbali vya Marekani.

Pia alibaini kuwa, Mr. Smith tayari alisha kuwa na data muhimu huhusu yeye Brat kabla hata hajakutana naye. CIA inapata data hizo kupitia mawakala wao maalumu waliopo ndani ya idara za vyuo.

Pia alibaini kuwa miongoni mwa maprofesa waliomfundisha chuoni, ni agent wa CIA na ndiye aliyesabibisha akatumiwa barua kwenye mailbox yake iliyomtaka afanye mawasiliano ya kukutana na Mr Smith.

Ila mpaka leo hajaweza kutambua jina la profesa huyo.

Maelezo haya nimeyatafsiri kutoka katika mtandao wa Quora. karibuni kujadili.
IMG_20190215_214730.jpeg
 
Jang-Bogo

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
2,891
2,000
Recruitment za hawa wenzetu wa ulimwengu wa kwanza huwa ziko smart sana.Wewe kwako unaweza ukaona kama ni bahati nasib imekuangukia kumbe wao walisha kuchora zamaan kwenye radar zao mpaka wakakumaliza.Ila hiz hiz za kwetu sijui wanatumia aproach gan lakin most of the agents ambao nimekutana nao mara nying nakuta wana watu wenye uhusiano nao ndan ya idara may be ukoo mmoja hata kama ni undugu wa mbal.
 
hongera kwa kukutana na ma-agents wa CIA. uliwatambuaje?....wao wenyewe walijitambulisha kwako au kuna namna fulani uliweza kuwatambua?.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Haya ni maelezo ya aliyewahi kuwa mfanyakazi wa CIA, ndg. Brad Robinson, Muhitimu wa University of California ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mchunguzi binafsi(private investigator) katika Taasisi ya Millennium Group huko Marekani.

Brad anazungumzia mazingira ambayo CIA walim-recruit mpaka kujakuwa jasusi mahiri wa shirika hilo.

Anasema, ilikuwa ni katika mwaka wake wa mwisho wa masomo katika chuo kikuu cha California(UCLA) alipokuwa anachukua degree ya Mahusiano ya Kimataifa(International Relations).

Alipata barua kupitia mailbox yake kwamba Mr. Smith ambaye ni muwakilishi wa CIA alikuwa ametembelea mji ambao chuo kipo na atakaa kwa siku kadhaa katika hotel fulani katikati ya mji.

Kipande cha karatasi kwenye mailbox yake kilisema kama yeye Brat atakuwa interested, apige namba ya simu ambayo ilikuwa imeandikwa kwenye kile kipande cha katarasi ili kupanga ahadi ya kukutana na Mr. Smith kwa mahojiano zaidi.

Japo alikuwa na mashaka, alifanya kama maelezo ya kwenye karatasi yalivyomuelekeza.

Siku ya siku alienda kukutana na Mr. Smith na mahojiano yao hayakuzidi hata dakika kumi.

Kwa kuwa hakuwa na uzoefu mkubwa wa kufanyiwa interview, siku alipoenda kukutana na Mr. Smith hakujiandaa kimuonekano. Hakwenda saloon kunyoa ndevu/nywele, hakuvaa suruali, alivaa kaptula. Kwa ujumla dress code yake haikuwa ya kupendeza.

Alifanya hivyo kwa kuwa hakuupa kipaumbele mikutano wake na Mr. Smith. alienda tu kama sehemu ya kupotezea muda(kuzuga).

Wakati wa mahojiano aliulizwa maswali mepesi sana. Aliulizwa kuhusu uzoefu wake wa kuajiriwa ambapo alijibu kwa kutoa maelezo kuhusu kazi yake ya kuwa muhudumu wa bar(bartender), pia aliulizwa ni kitu gani hupendelea kukifanya katika muda wake wa mapumziko, alijibu kwamba yeye hupendelea kushiriki katika mbio za magari za mitaani ambazo haziruhusiwi kisheria(illegal street racing).

Baada ya maswali hayo machache, mr. Smith alinyanyuka kumshukuru na kuagana naye.

Brat anasema alijuwa dhahiri shairi kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wa yeye kuwasiliana tena CIA. Moja kwa moja alijiweka katika fungu la kukosa. kumbe haikuwa hivyo.

Baada ya kama mwezi mmoja hivi kupita, alipokea barua kupitia Washington DC postmark, barua hiyo ilikuwa haina anuani ya kuonyesha ilipotoka.

Katikati ya barua hiyo kulikuwa na maneno machache tu ya kumpongeza ya "excellent". haikuwa na meneno mengine zaidi ya hayo.

Mwisho wa barua hiyo kulikuwa na namba ya simu ambayo alitakuwa kuipiga ili apewe maelezo zaidi kuhusu ajira yake na CIA.

Brad anasema huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari yake ngumu, ndefu na yenye changamoto kadhaa iliyopelekea kupata nafasi ya kujiunga katika mafunzo maalumu ya ujasusi katika spy academy ya CIA.

Kitu ambacho Brat alijifunza katika zoezi zima la kum-recruit ni kwamba watu kama Mr. Smith ni majasusi wastaafu waliokwisha fanyakazi na CIA kwa muda mrefu. Wamepewa jukumu la kusaka vijana wenye vipaji maalumu katika vyuo mbalimbali vya Marekani.

Pia alibaini kuwa, Mr. Smith tayari alisha kuwa na data muhimu huhusu yeye Brat kabla hata hajakutana naye. CIA inapata data hizo kupitia mawakala wao maalumu waliopo ndani ya idara za vyuo.

Pia alibaini kuwa miongoni mwa maprofesa waliomfundisha chuoni, ni agent wa CIA na ndiye aliyesabibisha akatumiwa barua kwenye mailbox yake iliyomtaka afanye mawasiliano ya kukutana na Mr Smith.

Ila mpaka leo hajaweza kutambua jina la profesa huyo.

Maelezo haya nimeyatafsiri kutoka katika mtandao wa Quora. karibuni kujadili.
View attachment 1023595
Sijaona "njia" ya "kuandaa"! Nilichokiona ni njia " mojawapo" ya jinsi CIA wanavyo ajiri.(recruit).

Kulikoni?
 
kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,518
2,000
Sijaona "njia" ya "kuandaa"! Nilichokiona ni njia " mojawapo" ya jinsi CIA wanavyo ajiri.(recruit).

Kulikoni?
waulize moderators wa jf, wao ndio waliobadili tilte ya thread.

hapo awali haikuwa kama inavyosomeka sasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom