Njia moja ya kumsaidia Mh. Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia moja ya kumsaidia Mh. Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Boss, Feb 7, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,944
  Trophy Points: 280
  Kwa mimi ninae amini Mungu yupo na ana nguvu....

  Siku zote huwa naamini mtu akifanya maombi maalum bila kujali dini yake, Mungu humsaidia huyo mtu.

  Lakini ni lazima huyo mtu ajifunze yeye mwenyewe namna ya kuzungumza na mungu wake... sio kuombewa wala kusaidiwa kwa maombi. Ni lazima yeye mwenyewe ajifunze namna ya kumuomba mungu akiwa peke yake...

  Ukiangalia historia ya viongozi mbalimbali na hata mitume na manabii.... utakuta wakati wa hard times, viongozi walitakiwa kuongoza maombi maalum kumuomba Mungu.

  Ukweli ni kuwa Kikwete anahitaji spiritual guidance ya namna fulani, binafsi namuona Kikwete yuko mbali sana na Mungu. Na mambo yakiendelea hivi, the worst is yet to come...

  Anahitaji god's favour ili kuvuka na kuwavusha salama anao waongoza... hana ujanja binafsi wa kuvuka mengi yaliyo mbele yake....

  Tatizo ni kuwa viongozi wengi wa dini wa siku hizi nao ni wasanii sana. Ukiangalia BAKWATA ndo kabisa, hakuna watu serious wanaoweza kumsadia Kikwete spiritually....

  What makes a great leader?

  Mimi naamini kuongoza watu zaidi ya milioni 40, ambao kati yao wapo wengi waliokuzidi
  akili, elimu na kadhalika... you need god's favour to succeed......

  Tatizo sio watu wengi wanao amini hivi.......
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,141
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ameen
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye nyekundu mimi naamini hivyo Mkuu
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,944
  Trophy Points: 280
  bubu..
  Kikwete anatakiwa kuzungumza
  na mungu wake na kumuomba
  ampe muongozo.....
  huwezi ongoza watu milioni 40
  kwa ujanjaujanja.....
  lazima awe honest na aombe msaada
  kwa mungu.....
  mimi naamini hivyo......
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mkuu, umeongea jambo ambalo pengine wengi tulikuwa hatuliwazi. Ni kweli kiongozi akikaa karibu na Mungu atapata mwanga na hekima ya jinsi ya kuongoza watu wake. Hayo nidyo aliyoyaomba mfalme Suleimani wa Agano la Kale. Anapaswa kumtanguliza Mungu katika shughuli zake kwa hakika.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Mkuu Boss, sijui hili la kuongea na Mungu kama litawezekana. Kuna kipindi Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu walitoa kauli moja kwamba nchi inaenda mrama na kwa maoni yangu wakati ule ulikuwa ni wakati muafaka wa Kikwete kuongea na Mungu wake lakini sidhani kama alifanya hivyo maana bado anaendeleza usanii tu na kutudanganya Watanzania kila kukicha tena bila hata woga. Kwa mfano hili la kutaka zijengwe flyovers wakati tuna matatizo makubwa katika mashule yetu, katika mahospitali yetu kwanini asiyape haya kipaumbele kwanza kabla ya hizi flyovers. Ni msanii tu wala sijui kama anamuogopa Mungu yuko tayari kusema lolote lile ili Watanzania wampe KULA hata kama ni uwongo.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,944
  Trophy Points: 280

  nionavyo mimi hana choice......
  akiendelea hivi.......
  sipati picha hali itakavyokuwa......
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Not as per sheick Yahya Hussein,kumpinga JK ni kumpinga Mungu,na ukijaribu kumpinga utakufa,so sioni kwanini JK awe na wasiwasi kama wananchi walio wengi wanamwamini Sheick Yahya.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  I salute u for ur wisdm Boss!
  Viongozi wa siku hizi sijui kama wanatambua kuwa Mungu ndio "huwaweka madarakani" kwani mamlaka yeyote huwekwa na MuNGU na pia wanahitaji kila mara kumwendea kuomba msaada! It looks theoretical but its very true!NAKUMBUKA baba wa Taifa alimuweka Mungu mbele sana hata kama alikuwa na mapungufu yake.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Hapo ndiyo maana huwa namkumbuka sana Nyerere maana hakuwahi kutudanganya hata siku moja kuahidi yale ambayo alikuwa anajua yalikuwa hayawezekani.
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,316
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  But the man has all confidence with his perfomance and that is why he looking for the second term. What makes you think that things are not going right? Just ask Makamba, you will get right opinion.

  Boss, this is Tanzania!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Hali itakuwa mbaya sana kuliko ilivyo sasa, angekuwa na mapenzi ya kweli na nchi yetu basi angetangaza kutogombea tena 2010 ili CCM imsimamishe mtu mwingine, lakini na yeye ni lazima akae awamu mbili hata kama utendaji wake ni sifuri.
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Tuacheni haya mambo ya kufikirika jamani!Mungu anamuweka nani madarakani?Au mnaconfuse taifa la Israel vs TZ?Ningeshukuru kupata ufafanuzi.

  Off Topic;btw nimeipenda hiyo avatar yako,kama ni picha yako unalipa mama no doubt.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Mhhhhh! ;) Kazi na dawa EBO!
   
 15. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #15
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Unajua BAK inaezekana kabisa JK haelewi chochote, hapa ndio tatizo , just imagine unampa kichaa mrusha mawe chupa ya chai au glass!!

  JK yuko dunia ya kwake kabisa, haishi Tz hii! wala hajui chochote kinachoendelea kwake yeye watanzania na Tanzania ni kama kuangalia film.

  Ndiyo maana juzi kaamka na kusema madaraja yajengwe, miezi miwili kabla ya uchaguzi ataagiza maziwa ya ng'ombe yatoke kila bomba Tanzania!

  ndiyo maana mtoa maada anasema njia ya kumdaidia JK , lile ni sikio la kufa!!
   
 16. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Yale ya shekhe yahaya si maombi ule ni utabiri wa kutumia mizimu, ni kweli rais Kikwete anahitaji kuwa karibu na Mungu wake na si kutegemea washauri wake ambao wengi wao wanampoteza anamhitaji Mungu ili amuongoze kuwafahamu wanaompoteza vinginevyo nani atamshauri kuwa washauri wake ndiyo wanaomponza? ni Mungu pekee.
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,944
  Trophy Points: 280
  sasa hili la mungu kuwa ndie aliewaweka
  madarakani nahisi halija click vizuri
  kwenye vichwa vyao.....
  naona wanajiona wana mbinu na wajanja
  na ndio maana wanaposhindwa kama hivi
  hawajui cha kufanya.
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,944
  Trophy Points: 280
  wewe jiulize hili......
  kwa nini Kikwete ndie rais???
  ana akili sana??no.
  amesoma sana??no
  anachapa kazi sana??no.
  so why????

  kwanini waliomsaidia awe rais,wao wenyewe hawawezi kuwa marais????

  mwisho utaona mungu anahusika kwa namna fulani..
  na ni mungu huyo ataweza kumsaidia iwapo atajifunza namna ya ku ask god's favour katika uongozi wake.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Kiongozi anachaguliwa na watu,watu wanamwomba Mungu wanayemwabudu ili awape hekima ya kumchagua kiongozi anayewafaa,hayo ni sahihi kwa upande wa wenye imani.

  Lakini mimi sikubaliani na nyie kwa upande mwingine,wananchi watumie facts pale inapokuja kwenye kumchagua kiongozi,na siyo kupiga kelele wee!Halafu mwishowe mnamwachia Mungu....Mungu hawezi kufanya miujiza ya kukusaidia namna ya kuishi,always kuna principles zinazo guide maisha ya watu...Sisi watanzania tuna tamaduni ambazo zimetupa mixture mbaya sana iliyopelekea matokeo tuliyonayo sasa.

  Wananchi should ask the elected leaders if they upheld with their promises na si kusema eti Mungu atamsaidia this time,ama sasa amwombe Mungu ili aweze kutimiza ile ahadi ya "Maisha Bora kwa kila Mtanzania" .....Akili kumkichwa.

  Tufanye mambo kwa reality na dini zitusaidie kufikiria kwa makini zaidi na kila mtu kwa imani yake apige dua ili akumbuke kuuliza maswali muhimu kabla ya kumchagua kiongozi.....Na pia kujiuliza kama kweli kiongozi huyo amefanya yale aliyowa ahidi, na siyo kufanya mambo kama tuna work out graph ya piece wise function....Ni muhimu tuwe consistency na si kumwachia Mungu mwishoni kwani ndiyo yale ya kuja kuambiwa ni "Chaguo la Mungu" Kiongozi akitaka kuchaguliwa tena tunarejea ahadi alizotoa na kuona kama ametufikisha wapi and if he deserves re election or not.
  Ama kweli dunia tambara bovu.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Unajua shida ni kwamba tunapomzungumzia Rais,sometimes tunamweka kwenye position ambayo ina mfit alien tu.....Yani ni kiumbe ambacho ni tofauti kabisa na sisi...Ni Mungu tuu!
  Tunacheza na mustakabali wa Taifa kwa misingi hii,unaambiwa serikali haina dini lakini watu watumie misingi hiyo hiyo ya kiimani inapokuja kwenye viongozi?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...