Njia mbili (2) za kustaafu ukiwa huru kifedha, ajira ina mchango mkubwa kustaafu mapema

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
239
Kustaafu ni kufikia uwezo wa kifedha wa kuweza kufanya chochote utakacho kulingana na kiasi cha utajiri wako.

Kwangu mimi kustaafu sio kuacha kufanya kazi (ajira au biashara). Neno kustaafu nimekutumia kwa lengo la kumaanisha kueleza hatua anayofikia mtu ya kifedha.

Sina maana uache kufanya kazi. Nina maana uweze kutengeneza kipato endelevu ambacho hata usipoingia kazini bado utakuwa na fedha ya kuweza kufanya chochote utakacho.

Kama utaweza kuwa na fedha za kutumia miaka yako inayobaki kuishi hapa duniani basi utakuwa umestaafu hata kama utaendelea kuwa kwenye ajira au biashara.

Hakuna kuacha kazi kwa mtu mwenye kusudi maalumu hapa duniani. Utatakiwa kubadili aina ya majukumu kulingana na kipato chako na nguvu ulinazo wakati husika.

Vitu viwili (2) ambavyo kila mmoja anaweza kufanya ili kuishi miaka mingi ni;-

✓ Kuendelea kufanya kazi au mazoezi bila kuacha kila siku au kwa siku sita za wiki.

✓ Kula chakula kinachojenga mwili na kwa kiasi.

Ukiacha kufanya kazi ni njia mojawapo ya kufupisha umri wa maisha yako. Hapa ninakushirikisha njia mbili za kustaafu mapema ukiwa huru kifedha.

Njia Mbili (2) Za Kustaafu.

(a) Kuwekeza kwenye hisa


Hapa unatakiwa kununua hisa kila mwezi kwa zaidi ya miaka kumi na kuendelea. Soko la hisa likianguka utaweza kupoteza sehemu ya uwekezaji wako.

Unaweza kustaafu kwa miaka 10, 20, 30 na kuendelea. Muda wa kustaafu inategemea na malengo yako na kiasi unachowekeza kila mwezi kwa kutumia mshahara wako.

Ni uwekezaji unaoshuka na kupanda thamani mara 16 ya uwekezaji kwenye viwanja na nyumba. Hii ina maana kuwa unaweza kupata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi wakati huohuo uwezekano wa kupata hasara ni mkubwa pia.

Unaweza kuanza kuwekeza kwenye hisa kwa kuchagua hisa za kampuni ambayo unaamini itakuwa na ukuaji mzuri.

Uwekezaji kwenye hisa utahitaji uwe na mshauri hasa mshauri aliyesajiliwa. Ukiingia tovuti ya soko la hisa na mitaji la Dar Es Salaam (Dar Es Salaam Stock Exchange) utaona orodha hiyo.

Vipande zinapanda thamani kila mwaka lakini vinapanda thamani kidogo kidogo. Unaweza kuwekeza UTT-AMIS kupitia ofisi zao zilizopo mkoani Mbeya, Dodoma, Mwanza, Arusha na Dar Es Salaam.

Pia, unaweza kuwekeza kupitia matawi yote ya benki ya CRDB Tanzania. Unaweza kuwekeza hata ukiwa nchi za nje.

UTT-AMIS wana aina sita za mifuko ya pamoja ya uwekezaji ambayo ni: mfuko wa umoja, Jikimu, Hatifungani, Ukwasi, Wekeza maisha na Watoto.

Unaweza kufuatilia ukuaji wake kwa kupakua taarifa za mifuko kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita kutoka kwenye tovuti ya UTT-AMIS.

(b) Nyumba za kupangisha

Ni njia ya pili ya kustaafu ukiwa huru kifedha. Njia hii humfanya mwekezaji kuendelea kuingiza kipato endelevu na kipato chanya kila mwezi.

Na mtaji fedha aliowekeza kwenye nyumba huongezeka thamani zaidi ya 10% kila mwaka kulingana na hali ya soko la viwanja na nyumba.

Nyumba za kupangisha hupanda thamani polepole na kwa uhakika. Ni vigumu kushuka kiasi cha kodi ya nyumba hata kipindi cha anguko la uchumi wa viwanja na nyumba (real estate crash).

Unatakiwa kufahamu kiasi halisi cha kodi inayotakiwa kuingia kila mwezi. Kisha kufanya makadirio ya jumla ya idadi za nyumba za kupangisha kulingana na malengo ya kodi unayotegemea kuingiza kila mwezi.

Kiasi cha kodi ya nyumba huongezeka kwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwenye nchi husika.

Utaendelea kuingiza kipato ambacho kinaweza kupunguza makali ya hali yako ya kifedha huku ukiendelea na mchakato wa kuwa kufikia uhuru wa kifedha.

Sababu za Kuchagua Nyumba Za Kupangisha Kama Njia Ya Kufikia Uhuru Wa Kifedha.

1. Udhibiti binafsi


Unapowekeza kwenye nyumba za kupangisha unakuwa na uhuru wa kuiongezea thamani nyumba na hatimaye kuongeza kodi ya kila mwezi.

Kwa udhibiti binafsi unaweza kuongeza thamani ya nyumba zaidi ya mara mbili ndani ya miezi 15 tu.

2. Kipato endelevu cha mwezi

Kila mwezi itakuwa inaingiza kodi ambayo inaweza kutumika kwa ajili ya kuwekeza tena na tena kwenye nyumba za kupangisha.

Kipato hicho kinaweza kutumika kutatua changamoto kubwa za kifedha ulizonazo bila kuathiri mtaji fedha uliowekeza kwenye nyumba husika.

Kipato endelevu unaweza kukitumia kununua au kujenga nyumba nyingine ya kupangisha na kuongeza zaidi kipato endelevu cha mwezi.

3. Kutumia kuombea mkopo wa majengo


Unaweza kutumia kuombea mkopo wa kununulia nyumba nyingine yenye kipato chanya pia.

Kwa kuombea mkopo unaweza kukuza uwekezaji wako kwa haraka zaidi tofauti na kwenye hisa ambazo huwezi kuombea mkopo wa biashara au uwekezaji.

4. Bima ya majengo


Ukimiliki nyumba za kupangisha unaruhusiwa kulipia bima ya majengo ambayo itakufanya uokoe sehemu ya mtaji fedha wako baada ya majanga au ajali kuharibu nyumba yako.

Lakini kwenye hisa, haiwezekani kulipia bima dhidi ya uharibifu wa hisa unazomiliki kwenye kampuni husika.

5. Kununua Kwa Bei Nafuu


Haiwezekani ununue hisa kwa bei ya punguzo kuliko bei iliyopo sokoni. Lakini kwenye kununua nyumba za kupangisha inawezekana kununua kwa bei ya punguzo.

Ni rahisi zaidi kununua nyumba ya kupangisha kwa bei ya punguzo kutoka kwa muuzaji aliyehamasika. Hivyo utakuwa unatengeneza zaidi ya 10% ya bei ya nyumba kulingana na hali ya soko na hamasa aliyonayo muuzaji wa nyumba husika.

Pia, unatakiwa kutengeneza faida ya 20% au zaidi wakati wa kujenga nyumba ya kupangisha.

Hivyo unaweza kutumia sehemu ya mshahara wako kuanza kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha na kufikia uhuru wa kifedha.

Mimi nipo kwa ajili ya kukusaidia uwekeze kwenye nyumba za kupangisha mpaka uwe huru kifedha. Karibu tufanye kazi pamoja.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp: +255 752 413 711
 
Nashukuru sana,

Naomba unisaidie kushare masomo yangu kwa watu wako wa karibu.

Rafiki yako,

Aliko Musa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom