Njia kuu mbili anazoweza kuzitumia Rais Magufuli kubaki madarakani zaidi ya miaka 10: Tuko macho hatukubali

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
1.Kutangaza hali ya hatari na kuahirisha uchaguzi 2025

Hili limo ndani ya katiba ya sasa, kwa mujibu wa katiba, pindi inapotokea hali ya hatari rais amepewa uwezo wa kuahirisha uchaguzi mpaka hali itengamae, kwa mfano nchi inapokuwa katika vita, au pindi inapotokea hali ya sintofahamu nchini kiasi kwmba kurudisha order ikawa ndiyo priority basi uchaguzi unaweza kuahirishwa mpaka hali itakapokaa sawa, katika kipindi hiki rais aliyeko madarakani ataendekea kuongoza mpaka utakapoitishwa uchaguzi mwingine.

Sasa swali ni je what if Magufuli akaitisha hali ya hatari kisha asiiiondoe ni kitu gani kitafanyika?, Ofcourse ataatawala lakini hali ya uchumi itakuwa fyongo mno maana hakuna investor atakayeinvest katika nchi yenye tangazo la hali ya hatari juu yake

2. Njia ya pili ni kuja na Katiba mpya kabla ya miaka yake 10 ofisini kutimia

Kwa sasa Magufuli ameiweka kapuni katiba mpya, mchakato wa katiba mpya ulikuwa umefikia hatua ya kuhitaji kura za maoni za wananchi ili waikubali rasimu ya Chenge iwe katiba mpya au la.
Magufuli aliikataa mchakato wa katiba mpya kistratejia kwa sababu Ingemfanya awe aina ya rais ambaye hana nguvu kama zile walizokuwa nazo watangulizi wake.

Lakini at one point in the future, Katiba mpya inaweza kuwa fimbo ya yeye kubaki madarakani kwa muda mrefu.
Kwa mfano ikitokea akatawala kwa katiba hii ya mwaka 1977 mpaka mwaka 2023, kisha mwaka huo akajifanya anaipenda sana katiba mpya, akaamua kuichukua rasimu ya Chenge na kuwapigisha watu kura za maoni na kuagiza Itumike kuanzia 2024, na uchaguzi akauitisha mwaka 2024 badala ya mwaka 2025 JE NI KIFUNGU GANI KWENYE HIYO KATIBA MPYA KITAMFUNGA ASIGOMBEE TENA?.

3. Kuibadiri katiba ya Sasa na kuongeza muda wa yeye kukaa madarakani
Hii siyo popular, lakini siyo kwamba haiwezekaniki 100%, kupitia njia hii ni kugumu sana kwa sababu atatumia nguvu nyingi mno kuiwezesha na hata akishafanikiwa, kuongoza nchi kutamuwia vigumu sana na atakuwa na reputation isiyopendeza kabisa ndani ya nchi na nje ya nchi na huenda hatma yake iwapo ataamua kupitia njia hii itakuwa siyo njema kwake (Rejea sababu za mwalimu kung'atuka)

CHAMBO YA KATIBA MPYA vs KUONGEZA MUHULA

Rais Magufuli anajua kuwa wananchi na vyama vya upinzani vinataka katiba mpya, Je yuko Tayari kufanya deal na wananchi hawa kuwa Nipeni Muhula zaidi wa uongozi in exchange niwape katiba mpya mnayoitaka?. Kama hamtaki nawaachia katiba hii hii inayowapigeni nyundo!. Je Rais Magufuli yuko tayari kuitupa Chambo na ndoano hii ya Katiba mpya lakini yenye kumruhusu yeye kugombea mihula kadhaa mbele?. Je Wapinzani wako tayari kufunika kombe mwanaharamu apite?, Je Wapinzani wako tayari kuwa wacha Tumvumilie atawale muda wake anaotaka ukiisha angalau tutakuwa na katiba nzuri kuliko ya mwaka 1977?

Hata hivyo hili nalo wapinzani inabidi wawe Sceptical maana what if wakakubali halafu baada ya kutawala kwa miaka baadae akaamua kuibadili tena katiba kurudisha awamu mbili za miaka mitano mitano ili asiingie kwenye historia mbaya ya kubadiri utaratibu alioukuta wa watangulizi wake?

VIGINGI VILIVYO MBELE YAKE
1.NCHI WAHISANI
Tukubali tusikubali, nchi yetu bado inategemea misaada, bila misaada hatutoboi mambo mengi mno, mfano mzuri tu ni hizi sheria kwa mfano za takwimu, mabinti wenye mimba wasiendelee na shule etc. Kutokana na kibinyo cha Hawa wahisani na mashirika ya mikopo ya ulimwengu, ndipo serikali yetu ikabadiri mambo mengi la sivyo serikali hii ilishafumba macho. Iwapo Wahisani wataweka msimamo wa kutomuunga mkono Magufuli kwenye kujiongezea muda haitomzuia kujiongezea muda lakini ataongoza nchi kwa shida na kubwa sana kiuchumi. Rwanda ni tofauti na TZ, Kagame pamoja na kuongoza nchi yake kwa mkono wa chuma International community ilimfumbia macho tu kwa sababu kwanza inamuona kama mtu aliyestabilize lile eneo, Bado wana Guilty consciousness kwa kutofanya vya kutosha kuzuia mauaji yale ya mamilion ya watu. Kwa hiyo Kagame wanampa free pass katika suala hilo.
Hii ni tofauti na TZ, Tanzania imekuwa relatively peaceful and stable kwa miaka mingi, Wahisani wamekuwa wakiitolea mfano TZ katika suala hili. Sasa iwapo Magufuli ataibadirisha huenda wasimpe ushirikiano kabisa na kujikuta anaendesha nchi kwa tabu tabu mno

2.PRECEDENCE ILIYOPO ITAMSUMBUA
Kitendo cha watangulizi wake kama vile Mwinyi, Mkapa na JK kutawala kwa kuheshimu katiba na kung'atuka baada ya muda kufika ni precedence inayoishi, imeshakuwa utamaduni wa mtanzania, yaani imeshakuwa kama nguzo kuu ya amani na utulivu katika nchi, kubadirishana madaraka kwa amani ni jambo ambalo limeshaingia katika akili za watanzania na limeshajulikana hivyo. Kwa hiyo mtu ambaye atajaribu kubadiri utamaduni huo ataonekana Kivuruge, Na kwa kweli itakuwa ni vigumu mno kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi labda alete mabomba yanayotoa asali nchi nzima.

3.ZANZIBAR INA TURUFU KUU
As long as lazima apate 2/3 ya kura za Wazanzibar bungeni kwenye kubadiri katiba ya sasa na as long as anahitaji wananchi wa Zanzibar kwenye kura ya maoni waikubali rasimu mpya basi kazi hapa anayo.
Maalim Seif ameshaliacha Lori la mafuta la CUF, Laiti angeendelea kubaki ndani ya CUF, Basi lori lile lilikuwa liungue na mafuta yake huku likiwaunguza akina Maalim, lakini kwa akili ya hali ya juu wamechomoka na wanaendelea na Safari.

CUF ya Lipumba ingekuwa ni kete muhimu ya kuzuia ushawishi wa wazanzibar kuzuia move hii, lakini sasa hivi Maalim na kundi lake wana jukwaa jipya la kutafuta wawakililishi na wabunge ambao ni kete muhimu ya kupitisha au kuzuia katiba mpya namabadriko ya katiba ya zamani pia

4. CCM ASILI
Pamoja na kwamba CCM ni Mwenyekiti wake, lakini Zipo siasa ndani ya CCM ambazo siyo nyepesi, pamoja na ukimya wa wakongwe lakini ule waraka wa makatibu wakuu wastaafu umetusaidia kutuonyesha kuwa ndani ya CCM kuna fukuto la kutokubaliana Mwenyekiti wao katika ishu kadha wa kadha za msingi. Pia kauli za Wana CCM wakongwe za wiki hii kama vile Msekwa, Warioba, Jakaya na Membe ni meseji kuwa kuna aina ya uongozi na utendaji wa serikali hii hawapendezwi na unavyofanywa, Kwa hiyo kutegemea kwamba CCM hii itakubali kubariki mabadiriko ya mihula ya urais bila watu kukunjana mashati mle siyo rahisi. Iwapo hawa CCM Kongwe wataamua kuungana na Wapinzani kupinga hili suala basi ni dhahiri move ya kubadiri katiba kuongeza Mihula halitofanikiwa hata kidogo.
 
Magufuli ni Magufuli tu,
kila mwananchi anamsifia kwa kazi na miradi anayoanzisha na miradi hiyo inakamilika na matunda yanaonekana.
Sema tu kuna watu kadhaa wanajaribu sana usiku na mchana kumchafua rais wetu wa muungano wa Tanzania, lakini hawafiki mbali.
Yote aliyoahidi, yamefanikiwa,
Mengine kwa asilimia 50,
Mengine kwa asilimia 70,
Mengine kwa asilimia 90
Mengine kwa asilimia 100.
Kitu ambacho viongozi wengine waliopita hawakufanikiwa.
Mimi mpaka sasa niko upande wa Magufuli.
 
Magufuli ni Magufuli tu,
kila mwananchi anamsifia kwa kazi na miradi anayoanzisha na miradi hiyo inakamilika na matunda yanaonekana. Sema tu kuna watu kadhaa wanajaribu sana usiku na mchana kumchafua rais wetu wa muungano wa Tanzania, lakini hawafiki mbali. Yote aliyoahidi, yamefanikiwa, Mengine kwa asilimia 50, Mengine kwa asilimia 70, Mengine kwa asilimia 90 Mengine kwa asilimia 100. Kitu ambacho viongozi wengine waliopita hawakufanikiwa. Mimi mpaka sasa niko upande wa Magufuli.
Tumbo Linadhalilishaaaa.

Daaaah
 
Magufuli ni Magufuli tu,
kila mwananchi anamsifia kwa kazi na miradi anayoanzisha na miradi hiyo inakamilika na matunda yanaonekana.
Sema tu kuna watu kadhaa wanajaribu sana usiku na mchana kumchafua rais wetu wa muungano wa Tanzania, lakini hawafiki mbali.
Yote aliyoahidi, yamefanikiwa,
Mengine kwa asilimia 50,
Mengine kwa asilimia 70,
Mengine kwa asilimia 90
Mengine kwa asilimia 100.
Kitu ambacho viongozi wengine waliopita hawakufanikiwa.
Mimi mpaka sasa niko upande wa Magufuli.
Ishu hapa ni Magufuli kubaki madarakani siyo kafanikiwa kwa asilimia ngapi.
 
Ishu hapa ni Magufuli kubaki madarakani siyo kafanikiwa kwa asilimia ngapi.
Tunafanya uchaguzi ili tupate viongozi watusaidie kutatua matatizo na changamoto zote zilizopo katika jamii.
Magufuli ametatua changamoto zote na matatizo yote katika jamii,
Kwa maana hiyo ataendelea kuwa madarakani mpaka pale atakapoona inamtosha kuwa madarakani.
Asante.
 
Tunafanya uchaguzi ili tupate viongozi watusaidie kutatua matatizo na changamoto zote zilizopo katika jamii.
Magufuli ametatua changamoto zote na matatizo yote katika jamii,
Kwa maana hiyo ataendelea kuwa madarakani mpaka pale atakapoona inamtosha kuwa madarakani.
Asante.
Una matatizo ya akili wewe...!! Changamoto zote za chato labdaa...leo hii bado kuna watoto wanasoma chini ya mitii unaleta ungese hapa na matatizo katika jamii yameongezeka zaidi watu Hawana amani hawan uhuru wa kuongea wala kuhoji watu wanauliwa ovyoo...wanatekwa wanapotezwa alafu wewe falaa mmoja unaleta ushabiki maandazi hapa.
 
Tunafanya uchaguzi ili tupate viongozi watusaidie kutatua matatizo na changamoto zote zilizopo katika jamii.
Magufuli ametatua changamoto zote na matatizo yote katika jamii,
Kwa maana hiyo ataendelea kuwa madarakani mpaka pale atakapoona inamtosha kuwa madarakani.
Asante.
Unajua umuhimu wa katiba.
 
Bashite alimtaka Mungu amshukuru jiwe, na jiwe akawa anachekelea kama zuzu kwa kupenda sifa, kwa hiyo hakuna cha ajabu
 
Wachawi ni watu wabaya sana.sisi tunajenga nyinyi mnawaza ujinga tu.
Shame on you

Magu yupo na ataendelea kuwepo maana watanzania tunamuombea kwa sana.

Nyinyi mnaowaza madaraka mtateseka sana hadi hiyo 2025 na bado .......
Anakuja majaliwa kassim majaliwa
 
Wachawi ni watu wabaya sana.sisi tunajenga nyinyi mnawaza ujinga tu.
Shame on you

Magu yupo na ataendelea kuwepo maana watanzania tunamuombea kwa sana.

Nyinyi mnaowaza madaraka mtateseka sana hadi hiyo 2025 na bado .......
Anakuja majaliwa kassim majaliwa
Bora majaliwaa hajimwbafy...
 
Back
Top Bottom