Njia kumi za kumtambua mtu anayesema uongo wakati unaongea naye.

Wengi hawajaielewa hii mada, wanajibu kwa hisia, wewe unaweza kujiona ni bingwa wa kusema uongo na kukausha lakini ukikutana na watu wenye professional yao wanakujua ndani ya dakika 1 tu, hata utoe macho, ukaze sauti lakini bado huwezi kuficha vitu fulani ambavyo kiuhalisia hata wewe hujui kama unavionesha.
 
Kukosekana mahusiano ya maneno na vitendo; kwa hali ya kawaida mtu akiulizwa swali na akatakiwa kujibu ndio au hapana kama ni ndio atatikisa kichwa kwenda juu na kama sio kweli atatikisa kichwa kwa pembeni sasa mtu akiulizwa swali akadanganya ataenda tofauti na hali ya kawaida mfano ukimuuliza kwamba ulienda kazini? atajibu ndio huku anatikisa kichwa kwenda pembeni bila yeye kutambua kwamba ulimi wake ndio unakubali lakini mwili wake umekataa.
The language of your body speaks louder than the mere words of your mouth.
 
NJIA KUMI ZA KUMTAMBUA MTU ANAYESEMA UONGO WAKATI UNAONGEA NAYE.

kuna msemo unasema kwamba kila mtu ni muongo hapa duniani yaani , hakuna mtu ambaye ameshawahi kuishi bila kusema uongo kabisa..

kitaalamu mtu akiulizwa swali akajibu uongo, hali ya mwili hubadilika yaani mapigo ya moyo hukimbia, presha hupanda na anaweza hata kutokwa jasho.


kipimo cha polygraphy hutumia njia hii kufahamu kama mtu anadanganya au vipi kwa kuangalia mabadiliko ya mfumo wa mwili pale anapokua anaulizwa maswali, mara nyingi kipimo cha polygraphy hutumika na askari polisi kwenye nchi zilizoendelea kuwagundua wahalifu lakini pia baadhi ya vipindi vya mahusiano kwenye tv huweza kuwapima wapenzi au wanandoa kujua kama mmoja wao sio muaminifu.

sasa katika njia za kijasusi, inawezekana kujua mtu, rafiki yako, ndugu yako, mpenzi wako au mke wako anakudanganya kwa kuangalia vitu muhimu wakati wa kumohoji muhusika bila kua na mashine na kujua kwamba anakudanganya kama ifuatavyo.

Kuchelewa kujibu swali ; ukimuuliza mtu swali akachelewa kujibu kuna uwezekano mkubwa anadanganya lakini inategemea na aina ya swali ulilolo muuliza, kwa mfano ukimuuliza sikukuu ya christmas mwaka 2005 ulikua wapi? kwa hali ya kawaida lazima atafikiria kabla ya kutoa jibu na hatatoa jibu la uhakika sana lakini ukimuuliza miaka mitano iliyopita ulinisaliti na mwanaume mwingine kama hakukusali atajibu haraka kwa mshangao kwamba sio kweli lakini kama ni kweli alikusaliti akili yake itaanza kuwaza huyu mtu kajuaje na atachelewa kujibu kisha baada ya muda atatoa jibu la kukana au atadanganya.
Kukosekana mahusiano ya maneno na vitendo; kwa hali ya kawaida mtu akiulizwa swali na akatakiwa kujibu ndio au hapana kama ni ndio atatikisa kichwa kwenda juu na kama sio kweli atatikisa kichwa kwa pembeni sasa mtu akiulizwa swali akadanganya ataenda tofauti na hali ya kawaida mfano ukimuuliza kwamba ulienda kazini? atajibu ndio huku anatikisa kichwa kwenda pembeni bila yeye kutambua kwamba ulimi wake ndio unakubali lakini mwili wake umekataa.
Kukohoa kidogo au kumeza kabla ya kujibu; mtu akipata wasiwasi baada ya kuulizwa kitu ambacho kimemkosesha amani kitaalamu mfumo wa mishipa ya fahamu kama sympathetic pathway unakua umefanya kazi hivyo mate yatakauka mdomoni na kwenye koo hivyo kuondoa hiyo hali atakohoa kidogo au kumeza mate kabla hajajibu ili kupata muda zaidi wa kutafuta cha kudanganya.
Kuficha macho au mdomo kwa kutumia mikono ; hii hutokea bila yeye kufahamu kitaalamu kama subconcious level yaani kibinadamu anashindwa kuuvumilia ule uongo anaosema hivyo atajikuta mwenyewe anaweka mikono sehemu hizo bila kujua ila wewe unayemuuliza maswali ndio utagundua kwamba anadanganya.
Kushika shika sana sehemu za kichwa chake; kama nilivyosema hapo juu, mfumo wa sympathetic system ukianza kufanya kazi mishipa ya damu huanza kujikunja hasa na sehemu zinazokosa damu hasa usoni huanza kuwasha kwa mbali na kua tofauti hivyo muongo atajikuta anakuna pua, anakuna sikio na hata viganja vya mikono.
Kuhangaika mazingira yanayomzunguka ; mtu anayedanganya akiulizwa swali anaweza kuanza kuanza kurekebisha vitu ambavyo viko sahihi kwa mfano kurekebisha tai, miwani, kuchomekea vizuri...kama ni mwanamke muongo ataanza kuweka nywele vizuri na kurekebisha sketi yake kabla ya kujibu kumbuka kama akifanya vitu hivyo baada ya kujibu sio muongo au unamuuliza mtu swali amekaa mezani ghafla kila kitu kimebadilika sehemu kilipokuwepo yaani kahamisha glass ya maji, funguo zake, simu na kadhalika.
Kushindwa kukuangalia usoni; unaweza ukaanza kumuuliza vitu vya kweli kabisa huku mnaangaliana lakini ghafla chomeka swali la tofauti ambalo unataka kujua kama ni kweli au sio kweli basi utaona anaanza kungalia pembeni na kushidwa kuangalia usoni na wakati mwingine kijasho chembamba kitamtoka.
Kuwa na maneno mengi sana; unaweza ukampigia simu ukamuuliza mtu kwamba yuko wapi akakujibu nilienda hospitali kuona mgonjwa njiani kidogo ningatwe na mbwa afu nimechoka sana ntajitahidi leo nilale mapema na kadhalika...huyu anaweza kua medanganya kitu sasa anajaribu kukificha na maneno mengi ili usimjue lakini ukute kwa hali ya kawaida angesema niko hospitali kisha akakaa kimya.
Kupunguza sauti; mtu kama huyu unaweza kaunza kumuuliza mambo anayofahamu kwa uhakika mfano jina lake, miaka yake, anaishi wapi au kama ni mchumba wako unaweza kumuuliza rafiki yake anaitwa nani, anafanya kazi gani na hapo atakua mchangamfu na kujibu vizuri kisha ghafla ukamuuliza nasikia umelala na mwanaume fulani hapo sauti itakua ndogo na atakataa kwa sauti ya chini.
Kuapa mara nyingi ; mtu muongo hujitahidi sana kujitetea aonekane hana kosa yaani kila baada ya muda ata apa kwa mungu, atakua na kauli kama 'ukweli kutoka moyoni", atasema hichi nachokisema hapa ni kweli kabisa lakini mtu mkweli anaweza kusema kitu mara moja hata usipomuamini hatajali sana na ataendelea na mambo yake.
Kuna Ukweli kiasi chake, utafiti mzuri huu
 
Mi naongeaga uwongo sana..ila ninachokosea ni kucheka...yaani nikikupiga fix alafu ukaingia king...hapo hapo nacheka kinoumaaa mpaka machozi
 
sio rahisi kunidanganya najua apoapo na hua sisaau(hii n kwa matumizi ya bdae)
ukiona nmepiga kimya haimaanishi sjakustukia ni baada ya kuchekecha madhara.....

napendaga nijue sababu ya kunidanganya na hii huwezi ijua mapema ila nitajua tuu

*kudanganya sio kizuri kunaondoa trustness na uaminifu ukishakua f, mausiano yenu hayatakua the same tena
 
Back
Top Bottom